Padre afariki akiendesha Ibada ya Mazishi Mtwara

"Mmoja wa madaktari wa Hosptali hiyo ya Ndanda ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye vyombo vya Habari (Dr Venance Chingwile) amethibitisha kupokelewa mwili wa Mchungaji Milanzi"
Kazi kweli kweli, yaani Dr. Venance Chingwile hakupenda Jina lake litajwe kwenye vyombo vya habari!
 
Kombora hilo dadekii

Tatizo hawa watawa wakishapangiwa majukumu ya kiroho ktk kanda husika

Huwa wanajisahau sana

Waruhusiwe kuoa tu
 
Wengi wameshangaa lakini nadhani ni kwamba hilo si jina lake sahihi huyo dokta, ndio wakalieka kwa mabano ila amesahau kuandika kwamba sio jina lake
 
"Mmoja wa madaktari wa Hosptali hiyo ya Ndanda ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye vyombo vya Habari (Dr Venance Chingwile) amethibitisha kupokelewa mwili wa Mchungaji Milanzi"
😂😂😂😂
 
Kama kafia makaburini wangemzika tu hapo hapo yaishe. Mawazo ya pombe
 
Wengi wameshangaa lakini nadhani ni kwamba hilo si jina lake sahihi huyo dokta, ndio wakalieka kwa mabano ila amesahau kuandika kwamba sio jina lake
Sasa kuna haja gani ya kuandika jina ambalo sio sahihi?

Kwani angesema tu hakutaka jina lake litajwe kuna shida gani?
 
Makamu wa Askofu wa Jimbo katoliki la Mtwara amekanusha hiyo habari.
"Ni upuuzi,upotoshaji na kukosa weledi. Mpaka sasa na tarehe tajwa hakuna Padri wa Jimbo la Mtwara aliyefariki. Aidha hakuna Padri mwenye jina la Laurence Millanzi katika jimbo la Mtwara.Ni taarifa inayomfurahisha mwandishi mwenyewe na aibu yake. Lakini pia ni chukizo kwa wapendao ukweli.
Vicar General, Mtwara."
 
Ni Mchungaji au Padre mbn haieleweki?
 
Inasadikika kuwa huyu mchungaji aliliponda Kanisa kwa kukataa kuendesha ibada ya kumzika marehemu kwani alikuwa hashiriki kikamilifu; so katikati ya ibada ya mazishi, huyu mchungaji yakamkuta yaliyomkuta.
 
Hii taarifa mbona ina mkanganyiko! Maana Kanisa Katoliki lina Mapadre/Makasisi! Na siyo Wachungaji.

Lakini pia makao ya Padre, au utambulisho wake ni Parokiani! Padre fulani wa Parokia ya...., Jimbo Katoliki la....!! Na wala siyo Kijiji cha.....!

Sasa huyu Mchungaji wa Kanisa Katoliki, Kijiji cha.......! Mbona taarifa inachanganya.

Anyway, Rest in peace Mchungaji wa Kanisa Katoliki Kijiji cha Liputu huko Mtwara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…