Padre afariki akiendesha Ibada ya Mazishi Mtwara

Padre afariki akiendesha Ibada ya Mazishi Mtwara

Mchungaji wa Kanisa Katoliki kijiji cha Liputu, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Laurence Milanzi amefariki Dunia maeneo ya makaburini alipokuwa akishiriki mazishi ya mwanakijiji mwenzao aitwae Daudi Veno

Untitled-3_0.jpg

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mchingaji huyo alianguka ghafla wakati akiwaasa watu kutosusia misiba kwa mtu asiyehudhuria Nyumba za Ibada.

Kifo cha Mchungaji huyo kimetokea kwenye Kijiji hicho Julai 19 mwaka huu, saa 5:00 asubuhi kwenye eneo linalotumika mahususi kwa mazishi ya watu wanaofariki dunia.

Mwili wa Mchungaji huyo umehifadhiwa katika Hosptali ya Mission ya Ndanda, Wilaya ya Masasi ukisubiri taratibu za mazishi yanayotarajiwa kufanyika Kijiji hapo, baada ya kukamilika kwa taratibu zote.

Baadhi ya mashuhuda walioudhuria mazishi ya Daudi Veno, wameeleza kwamba, Mchungaji Milanzi amekutwa na umauti huo, alipokuwa anatoa sala na kuwasihi viongozi wenzake wa Dini kuacha tabia ya kutohudhuria mazishi kwa Binadamu mwenzao asiyeshiriki masuala ya Ibada.

Mchungaji Milanzi alisema kitendo cha kususa kumuombea marehemu kwa kuwa hakuwa anashiriki kwenye Nyumba za Ibada, Kanisani na misikitini ni kwenda kinyume na maagizo ya mwenyezi Mungu alivyoagiza mtu anapofariki ni muhimu akazikwa na sio kumuacha kwani uharibu hali ya hewa kutokana na harufu mbaya kutoka kwake.

“Baada ya kueleza hayo, tukamuona mwenzetu akidondoka chini kisha kupoteza fahamu” Walieleza Joseph Michael na Samwel Chindonga. Aidha,mashuhuda hao wamesema kwamba baada ya Mchungaji huyo kudondoka chini walimchukuwa na kumkimbiza Hosptali ya Ndanda na kuelezwa na madaktari kuwa alishafariki

Mmoja wa madaktari wa Hosptali hiyo ya Ndanda ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye vyombo vya Habari (Dr Venance Chingwile) amethibitisha kupokelewa mwili wa Mchungaji Milanzi, na kuhifadhiwa chumba cha maiti (Mochwari) ukisubiri taratibu za mazishi.

Chanzo: EATV
Tukio kama hili lilitokea miaka michache iliyopita bapo mchungaji alifariki akiendesha sala ya maziko makaburini.
 
Mmoja wa madaktari wa Hosptali hiyo ya Ndanda ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye vyombo vya Habari (Dr Venance Chingwile) amethibitisha kupokelewa mwili wa Mchungaji Milanzi, na kuhifadhiwa chumba cha maiti (Mochwari) ukisubiri taratibu za mazishi.

Hii ni Kali ya kumuaga IGP Simon Sirro
 
Mfumo wa mwili wa mwanadamu, ni sawa na mfumo wa gari; breakdown inaweza kutokea muda wowote bila kujua.
Kama nakuelewa vile........kwa hiyo engine kwenye gari inafanana na kiungo gani kwa binadamu?
 
Uandishi wa hovyo kabisa yani daktrari ambaye hakutaka jina lake litajwe , then kwenye mabano mnaweka tena jina lake , haya mambo haya yanashida sana
 
Habari ya uongo hii hajafa kiongozi yeyote wa kanisa katoliki huko kusini
 
Aliyefariki ni mchungaji wa makanisa ya kilokole, marehemu alikataliwa kuzikwa na kanisa la RC
 
Kanisa katoliki kina mapadre. RIP, kaz ya Mungu Haina makosa
 
"Mmoja wa madaktari wa Hosptali hiyo ya Ndanda ambaye hakupenda jina lake litajwe kwenye vyombo vya Habari (Dr Venance Chingwile) amethibitisha kupokelewa mwili wa Mchungaji Milanzi"
"Kifo cha Mchungaji huyo kimetokea kwenye Kijiji hicho Julai 19 mwaka huu, saa 5:00 asubuhi kwenye eneo linalotumika mahususi kwa mazishi ya watu wanaofariki dunia."
 
Back
Top Bottom