Padre aliyeongoza misa kumuaga Jenista Muhagama asikitika 'nilijiuliza ni kwanini kifo chake kitokee wakati huu?'

Padre aliyeongoza misa kumuaga Jenista Muhagama asikitika 'nilijiuliza ni kwanini kifo chake kitokee wakati huu?'

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Akizungumza wakati wa Misa Takatifu ya kuuaga mwili wa marehemu Jenista Mhagama, Padre Emmanuel Mtambo, Baba Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledóchowska, Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma, leo Desemba 13, 2025, amesema alipokea taarifa za kifo hicho kwa huzuni kubwa.

Padre Mtambo amesema siku chache kabla ya kifo chake walikuwa pamoja wakizungumza na marehemu, ambaye wakati huo alikuwa katika hali nzuri kiafya, hali iliyomfanya kushangazwa na taarifa ya kifo chake.

"Nilipokea taarifa ya kifo cha Mh. Jenista Mhagama kwa huzuni kubwa. nilijiuliza ni kwanini kifo chake kitokee wakati kama huu? Kwangu ni huzuni kufiwa na muumini mzuri wa namna hii lakini pia ni huzuni kwa sababu kwangu huu sio wakati wa kupata msiba wa namna hii katika parokia yetu.

Juzi kati baada ya kupata ombi la familia kuhusu misa hii nijawa na hofu kubwa sana nikijiuliza maswali mengi sana kwa sababu nilijua tatizo la afya yake halikuwa kubwa mno na nilifikiria kwamba halikuwa hatarishi kwa maisha yake. Lakini pia hofu yangu kubwa ni kuwa nisingependa kuwa mwenyeji wa msiba mkubwa wa namna hii hapa parokiani."



 
Sijui lengo la mtumishi ni nini lakini kwenye suala la kifo hakuna foleni ya umri au hadhi. Sote tutaondoka pale ambapo Mungu aliyetupa pumzi atakaposema imetosha. Ndio maana wapo wanaokufa wakiwa na masaa tu duniani. Kujiuliza kwanini aondoke wakati huu kunaleta maswali ambayo hakuna majibu.

Amezungumzia ugonjwa ambao haukuwa hatarishi kwa mgonjwa bila kuutaja. Watu wanaomsikiliza wanapimaje uhatarishi au kutokuwa hatarishi kwa ugonjwa wake? Tayari kuna maneno mtandaoni na mitaani,Padre ameongeza sababu ya kuhoji. Kwa maoni yake Marehemu alipaswa aondoke lini akiwa amekamilisha nini? Kuhoji kwa nini sasa kuna leta swali la ilipaswa kuwa lini na kwanini?

Tuko pagumu sana kama Taifa.
 
Back
Top Bottom