Sijui lengo la mtumishi ni nini lakini kwenye suala la kifo hakuna foleni ya umri au hadhi. Sote tutaondoka pale ambapo Mungu aliyetupa pumzi atakaposema imetosha. Ndio maana wapo wanaokufa wakiwa na masaa tu duniani. Kujiuliza kwanini aondoke wakati huu kunaleta maswali ambayo hakuna majibu.
Amezungumzia ugonjwa ambao haukuwa hatarishi kwa mgonjwa bila kuutaja. Watu wanaomsikiliza wanapimaje uhatarishi au kutokuwa hatarishi kwa ugonjwa wake? Tayari kuna maneno mtandaoni na mitaani,Padre ameongeza sababu ya kuhoji. Kwa maoni yake Marehemu alipaswa aondoke lini akiwa amekamilisha nini? Kuhoji kwa nini sasa kuna leta swali la ilipaswa kuwa lini na kwanini?
Tuko pagumu sana kama Taifa.