Padre Kitima: Suala la kuminywa haki za Wamasai wa Ngorongoro si sahihi

Padre Kitima: Suala la kuminywa haki za Wamasai wa Ngorongoro si sahihi

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoriki Tanzania Daktari wa Falsafa na Padre ndugu Kitima amesema si haki na ni udhalilishaji wa wazi wanafanyiwa Wamasai wa NGORONGORO kwa kunyimwa haki zao.

"....leo hii tunapozungumza ndugu zetu Wamasai wa kule NGORONGORO wanatuma ujumbe mbaya wenye twasira hasi Kimataifa. Unapowaeleza ni hiari yao kubaki NGORONGORO halafu ukiwanyima haki zao za msingi huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu! Jiulize kwa walichokifanya leo huko Duniani waelevu wanatufikiriaje!?" Amehoji Kiongozi huyo mtendaji wa TEC.

Chanzo: Jambo TV

Pia soma:Kuelekea 2025 - Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
 
TEC tuliwategemea sana, tukadhani mna nguvu zisithomithilika pengine mkaliokoa taifa, kumbe na nyie ni kama vyama vya upinzani tu....
Kanisa sio chama cha siasa.

Hii kazi ya kuiwajibisha serikali tufanye sisi wananchi sio makanisa wala misikiti kazi zao sio harakati za siasa.

Ni mbaya dini zikitawala siasa za nchi.
 
Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoriki Tanzania Daktari wa Falsafa na Padre ndugu Kitima amesema si haki na udhalilishaji wa wazi wanafanyiwa Wamasai wa NGORONGORO kwa kunyimwa haki zao.

"....leo hii tunapozungumza ndugu zetu Wamasai wa kule NGORONGORO wanatuma ujumbe mbaya wenye twasira hasi Kimataifa. Unapowaeleza ni hiari yao kubaki NGORONGORO halafu ukiwanyima haki zao za msingi huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu! Jiulize kwa walichokifanya leo huko Duniani waelevu wanatufikiriaje!?" Amehoji Kiongozi huyo mtendaji wa TEC.

Chanzo: Jambo TV
 
Kanisa sio chama cha siasa.

Hii kazi ya kuiwajibisha serikali tufanye sisi wananchi sio makanisa wala misikiti kazi zao sio harakati za siasa.

Ni mbaya dini zikitawala siasa za nchi.
Ni kweli lakini unawakumbuka wale maaskofu 20 wa kule kwa Tshikedi? Walizungumza, Kabila hakuchukua round!

Sisi wengi tulidhani nguvu yao iko hivyo hata huku kwetu....kumbuka jeshi ni loyal tayari, sasa kwa upuuzi unaoendelea, nani mwingine wa kuokoa jahazi?
 
TEC washakuwa maaachawa wa mama. Katibu TEC anasema haoni umuhimu wa katiba mpya. Sababu zake eti hata kama katiba mpya itapatikana haitasaidia chochote kama utashi hakuna.

Kaongea utumbo sana huyu katibu wa TEC.
Hivi hajui kuwa katiba bora huwa na mifumo bora ya kujilinda? Katiba bora inaimarisha uhuru wa mihimili 3 na hivyo kufanya kazi ya check and balance ipasavyo. Katiba bora haichezewi hovyo.
 
Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoriki Tanzania Daktari wa Falsafa na Padre ndugu Kitima amesema si haki na ni udhalilishaji wa wazi wanafanyiwa Wamasai wa NGORONGORO kwa kunyimwa haki zao.

"....leo hii tunapozungumza ndugu zetu Wamasai wa kule NGORONGORO wanatuma ujumbe mbaya wenye twasira hasi Kimataifa. Unapowaeleza ni hiari yao kubaki NGORONGORO halafu ukiwanyima haki zao za msingi huo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu! Jiulize kwa walichokifanya leo huko Duniani waelevu wanatufikiriaje!?" Amehoji Kiongozi huyo mtendaji wa TEC.

Chanzo: Jambo TV
Achilia mbali kwamba maaskofu ni mitume wa Mungu ila Askofu mmoja wa catholic ana degree si chini ya tatu, hizi ni PhDs, zikiongea kaa usikilize kwa utulivu.
 
Ni kweli lakini unawakumbuka wale maaskofu 20 wa kule kwa Tshikedi? Walizungumza, Kabila hakuchukua round!
Mimi haya mambo siyataki kabisa nayafahamu madhara yake.

Imani ni kitu kibaya tena Afrika kwa waafrika elimu na matumizi ya akili yapo chini ni hatari.

Wao wabaki makanisani na misikitini kazi ya kuiwajibisha serikali tuachiwe sisi wananchi kama wanataka kuungana nasi wavue kanzu na majoho waje kama wananchi wa kawaida sio viongozi wala taasisi fulani ya kidini.

Dini ikae mbali kabisa na siasa za nchi kuna madhara makubwa ikisogezwa ni rahisi kuleta mpasuko wa hatari.
 
Back
Top Bottom