Jana Padre Kitima alinukuliwa na chombo fulani cha habari akitoa kauli kuhusu kile kinachoendelea Ngorongoro.
Kitima ambaye anafahamika kwa ukada wake ndani ya CHADEMA alisema ni wakati kwa Watanzania kukemea vitendo alivyodai viovu vinavyofanyika nchini.
Cha kustaajabisha Kitima ambaye ni kiongozi wa dini tulitegemea kabla ya kuzungumza kile cha Ngorongoro angeanza kukemea na maovu haya yaliyofanywa na Mapadre wenzake.
1. Padri Elipidius Rwegoshora wa Bukoba kashiriki kumuua Albino, Padri Charles Kitima hajamuona ila anaona Wamasai Ngorongoro.
2. Padri Bunda anaibia masista raia wa hispania kisha kwenda kufungua baa na vituo vya kamari. Padri Charles Kitima haoni ya kukemea katika hayo, anaona Wamasai wa Ngorongoro tu walio-printiwa Mabango nchini Kenya.
3. Padri Stanslaus Sala wa Jimbo la Moshi kalawiti, yeye hajamuona ila anaona nchi imekuwa mbaya kuishi.
Huu upofu wako mtumishi wa kanisa ni wa asili, ukubwani, wa kuamua au wa kulipwa?