Padre Kitima: Tanzania kinachosumbua ni utashi wa watu kuongozwa na sheria

Padre Kitima: Tanzania kinachosumbua ni utashi wa watu kuongozwa na sheria

Mm sikubaliani na padre Kitime, kwasabb msingi wa nchi kuwa na katiba ni kuiondoa dhana ya viongozi kuendesha nchi kwa utashi na matakwa yao.

Katiba bora haitoi mwanya wa kiongozi kuamua kuiheshimu ana kutokuiheshimu kwa utashi wake. Katiba bora huwa Ina wivu sana. Hivyo humuadhibu yeyote anayekwenda kinyume nayo.

Katiba bora hujenga mihimili imara isiyooneana aibu ktk kushughulikiana. Na mihimili hiyo imara haitegemeani na haina muingiliano wowote
Asante mkuu Sexless kwa maoni mazuri

Mimi nami nakubaliana na wewe kwa kutokukubaliana

Unadhani ni kwa nini katiba imekuwa ikivunjwa na hakuna chochote kile cha kufanywa hao watu?
 
Sasa kwa nini katiba imekuwa ikivunjwa na hakuna chochote?
Ni kwasabb katiba ni mbovu. Rais yuko juu ya sheria (na anateua viongozi wengi sana), Na hao wateule wake wanakuwa juu ya sheria pia, maana ili uwawajibishe lazima rais mwenyewe aridhie.

Ndiyo maana viongozi wanavunja katiba lkn inakuwa ngumu kuwawajibisha..
 
Nipo hapa...

Ndio maana mimi ni miongoni mwa WAPINGAJI KATIBA MPYA kwa kuisimamisha misuli ya shingo kwa "mbango" mpaka kichwa kinaniuma....

Si vijiwe vya kahawa....ninaipinga katiba mpya.....

Si mabanda ya wanzuki na komoni....ninaipinga katiba mpya...

KATIBA ILIYOPO NI NZURI NA IENDELEE TU...

Kinachohitajika tu ni UTASHI WA USIMAMIZI WA KATIBA.....

#SiempreJMT[emoji120]
Wee ni mbogamboga usiejitambua bora etwege!!
 
Hata tukawa na katiba bora kabisa , kama hakuna utashi wa kuongozwa na sheria ni Bure!

Kumbe huyu ni mbobezi wa Constitutional Law!

Msikilize
Wachache ndio watamuelewa Kitima, utashi wa kuongozwa na sheria haupo kwa sababu ya mfumo!! Mfumo hauheshimu katiba. Mfano ni hii katiba iliyopo tu wanaivunja na kuikanyagakanyaga!!
 
Inatakiwa hiyo Katiba Mpya ikipatikana iwabane wale wasiotaka kuifuata, nao wajue watabanwa na Katiba husika, kuanzia hapo ndio tutaanza kutembea njia moja inayofanana.

Huwa naona kinachofanya hili jambo lionekane kuwa gumu, ni pale ambapo utakuta viongozi fulani hawawajibiki kwa makosa wanayofanya wakiwa kwenye utawala, kinga ya kutoshtakiwa ndio chanzo cha viongozi kuvunja sheria makusudi.

Ikishaondolewa hiyo kinga kwao, wote tukawa sawa chini ya sheria, hayupo atakayemletea ujuaji mwenzake kwasababu ya nafasi anayoshikilia kisiasa, tutaanza kuheshimiana, baada ya hapo ndio sheria zitaanza kufuatwa bila shuruti.
Huwa namshangaa mtu anapoona eti Katiba mpya bora sio muhimu 😅😅😅

Hata Mwalimu Nyerere alisema hii katiba imempa madaraka makubwa sana Rais wa Nchi kuliko mihimili mingine yooote !!
Kwahiyo kama Padre Kitima anaona Katiba sio sababu ya matatizo tuliyonayo basi hakuna haki ya kulalamikia jambo lolote lililofanyiwa maamuzi na wenye kufanya maamuzi kwa sababu wanafanya maamuzi kwa mujibu wa sheria zinavyowaongoza na kwa mujibu wa Katiba ambayo ndio sheria mama !!
Conflict of interest 😂😂😂. ?
 
Kwa uelewa wako, nia ya kuongozwa na sheria ina maanisha nini?. Huwezi kusema kwamba wananchi hawana nia ya kuongozwa na sheria kwasababu Tanzania kuna vyombo vya usalama ambavyo vinatakiwa kuhakikisha kwamba wananchi wote wanatii sheria hizi.
kwa kawaida sheria ina maana kwa wenye utashi wa kuitii,otherways ni gazeti la wiki iliyopita tu.

maana ya father hapo juu,ni mfano pale tunapopiga kelele za katiba mpya wakati hata hii iliyopo wandewa wanaichambia mara kadhaa.
 
Huwa namshangaa mtu anapoona eti Katiba mpya bora sio muhimu 😅😅😅

Hata Mwalimu Nyerere alisema hii katiba imempa madaraka makubwa sana Rais wa Nchi kuliko mihimili mingine yooote !!
Kwahiyo kama Padre Kitima anaona Katiba sio sababu ya matatizo tuliyonayo basi hakuna haki ya kulalamikia jambo lolote lililofanyiwa maamuzi na wenye kufanya maamuzi kwa sababu wanafanya maamuzi kwa mujibu wa sheria zinavyowaongoza na kwa mujibu wa Katiba ambayo ndio sheria mama !!
Conflict of interest 😂😂😂. ?
bado father ni akili kubwa.

hiyo hiyo iliyompa mamlaka makubwa rais lakini bado kuna muda inaonekana hayamtoshi madaraka hayo.vipi yakipunguzwa!!ni mara ngapi ataivunja hiyo katiba???
 
Mm sikubaliani na padre Kitime, kwasabb msingi wa nchi kuwa na katiba ni kuiondoa dhana ya viongozi kuendesha nchi kwa utashi na matakwa yao.

Katiba bora haitoi mwanya wa kiongozi kuamua kuiheshimu ana kutokuiheshimu kwa utashi wake. Katiba bora huwa Ina wivu sana. Hivyo humuadhibu yeyote anayekwenda kinyume nayo.

Katiba bora hujenga mihimili imara isiyooneana aibu ktk kushughulikiana. Na mihimili hiyo imara haitegemeani na haina muingiliano wowote
Nadhani Fr. Kitima anaongea katika Muktadha wa dini, kuheshimu "AMRI" za Mungu kwa utashi.... KITU AMBACHO HAKIPO KWA MWANADAMU (au kama kipo ni wachache ).
Ukimwondolea rais kuteua govn officials, Rais hatakuwa dictator! ataheshimi katiba

How do you do it kumwondolea ufalme?
1. Kuwe na wagombea huru kwa urais, ubunge etc etc
2. CJ agombee na wenzake (kama ilivyo kenya)
3. IGP agombee
4. Futa wakuu wa mikoa, wilaya (au wachaguliwe na wananchi na kuondolewa na wananchi...wapigiwe kura na wananchi)
5. DED wagombee
6 Gavana wa Benki Kuu , mameneja wa makampuni ua umma ( na vyeo vikuvwa kama hivyo wagombee)
 
bado father ni akili kubwa.

hiyo hiyo iliyompa mamlaka makubwa rais lakini bado kuna muda inaonekana hayamtoshi madaraka hayo.vipi yakipunguzwa!!ni mara ngapi ataivunja hiyo katiba???
Watu wengi hawaitaki au hawaipiganii Katiba mpya bora kwa sababu nimegundua wengine ni wanufaika wa hii katiba kwa namna moja au nyingine 😅😅🙏🙏

Kwahiyo hapo kuna ile kitu inaitwa Conflict of interest 😅🙏🙏
Na mara nyingi wenye Akili kubwa ndio huwa wahusika wakuu !!
Ndio maana huwezi kuwasikia wakidai Katiba mpya !!🙏🙏🙏
 
Watu wengi hawaitaki au hawaipiganii Katiba mpya bora kwa sababu nimegundua wengine ni wanufaika wa hii katiba kwa namna moja au nyingine 😅😅🙏🙏
sijui wewe unapata imani kiasi gani kwamba katiba mpya itaheshimiwa.
Kwahiyo hapo kuna ile kitu inaitwa Conflict of interest 😅🙏🙏
Na mara nyingi wenye Akili kubwa ndio huwa wahusika wakuu !!
Ndio maana huwezi kuwasikia wakidai Katiba mpya !!🙏🙏🙏
binafsi sioni hata haja ya katiba mpya sababu iliyopo inapuuzwa pia.
 
Na
Nadhani Fr. Kitima anaongea katika Muktadha wa dini, kuheshimu "AMRI" za Mungu kwa utashi.... KITU AMBACHO HAKIPO KWA MWANADAMU (au kama kipo ni wachache ).
Ukimwondolea rais kuteua govn officials, Rais hatakuwa dictator! ataheshimi katiba

How do you do it kumwondolea ufalme?
1. Kuwe na wagombea huru kwa urais, ubunge etc etc
2. CJ agombee na wenzake (kama ilivyo kenya)
3. IGP agombee
4. Futa wakuu wa mikoa, wilaya (au wachaguliwe na wananchi na kuondolewa na wananchi...wapigiwe kura na wananchi)
5. DED wagombee
6 Gavana wa Benki Kuu , mameneja wa makampuni ua umma ( na vyeo vikuvwa kama hivyo wagombee)
huo ndio ukweli wenyewe!!
 
Back
Top Bottom