Issue sio kuuwa watu wote bali ni kwamba inasemwa kuwa enzi za Magufuli kulikuwa hakuna amani na uhuru wa kukosoa kwamba watu waliyokosoa walitekwa na kuuliwa, tukawa tunaambiwa hadi zile maiti za kwenye viroba ambazo japo haikuwa ikijulikana waliyouliwa ni akina nani ila ilikuwa inasemwa kuwa ni wakosoaji wa serikali ya Magufuli na kwamba watu waliogopa kukosoa.
Katika mazingira kama hayo ya kwamba hata wasiojulikana tu walishughlikiwa kwa kukosoa sasa tunapoona wanaojulikana wanakosoa tena waziwazi lazima tuulize imekuaje ni kwamba Magufuli aliogopa kumshughlikia huyo Padri au alimuacha tu?