UKITENDA MEMA DUNIANI UTAKUMBUKWA DAIMA. SOMENI WASIFU WA MAREHEMU KAKA NA NDUGU YETU PADRE PAUL IGNAS SHEWIYO KAMA NILIVYOUPOKEA KUTOKA KWA KIONGOZI WA PAROKIA MOJA ALIYOHUDUMU DAR ES SALAAM.
PUMZIKA KWA AMANI KAKA.ULIKUWA MMOJA WA WANASEMINARI WANYOOFU SANA KIPINDI HICHO UKIWA SEMINARI.
***********^^^^^^^^^^*****
Bado natafakari, nayastaajabu matendo Makuu na ya ajabu ya Mwenyezi MUNGU! 🙆🏾♂
Ni kama siamini ninachokisoma au kusikia. Ni kama naota mchana..... lakini la hasha, ni kweli, naona Baba Shewio hatunae tena! 😭
Pole sana Baba Paroko, Baba Paroko Msaidizi, Waumini wote na zaidi kwa Kanisa kwa ujumla! 🙏🏾
Nimemfahamu Baba Shewio tangu huko Moshi muda mrefu sasa, hakika nimemfahamu kama Baba mwenye mapenzi mema sana kwa Kanisa na jamii ya Waumini wote! Tumepata pigo na pengo ambalo MUNGU Baba Mwenyezi pekee ajua siri na mpango wake.
Baba Shewio alikuwa Mcheshi, mwenye furaha na tabasamu toka rohoni! Alijaa upendo wa dhati, alipenda Yatima na wenye shida! Aliwakumbuka walemavu na wenye uhitaji...na hakika, alisikia raha na faraja alipoweza kutenda jambo la huruma kwa wahitaji! 🙏🏾
Leo hatunae, ametangulia. Tuhuzunike lakini tufurahi kwa bahati ya kupata fursa ya kuishi na Baba Shewio. Kila mmoja wetu amuenzi Baba Shewio kwa kuishi "Upendo" na kuyaendeleza yale mambo makuu aliyoyaishi hapa Duniani! 🙏🏾
Baba Shewio, natazama picha zako, nakumbuka maneno yako, nakukumbuka sana! Natokwa machozi, machozi ya simanzi ya kutuacha...lakini pia ya furaha kwa matumaini makubwa kuwa umeenda kwa Baba Mbinguni! 🙏🏾
Buriani Baba Shewio, hakika kuishi kwako ni KRISTO na hata kifo chako naamini ni faida kwako, Starehe kwa Amani Baba Shewio! Nakumbuka jinsi ulivyoendesha Misa ya Marehemu Baba yako Mzazi na jinsi ulivyokuwa shupavu, mwenye furaha na Imani.....na hasa maneno yako ya faraja na Imani. Ulimshika Kristo haswa, pumzika! 🙏🏾
Umekuwa Jemedari mnyenyekevu, Askari mpole wa YESU,.... Rubani mwenye Hekima kwetu Waumini Wasafiri hapa Duniani, Baba aliejaa Upendo kwa Kanisa lote bila ubaguzi na Mchungaji Mwema uliyekuwa kimbilio la wengi, hakika tutakukumbuka sana! 🙏🏾
Kwaheri Baba Shewio, japo umezimika ghafra kama Mshumaa barazani! Safari yako ni somo kwetu, naam, kwetu tuliosalia.... tuwe tayari, tuishi kwa Upendo na kumtumaini Bwana, kwani hatujui siku wa saa!
Tulikupenda Baba Shewio, tunakupenda, na tutakuenzi daima! Ukiweza, tuombee Baba Shewio, tuombee kama ulivyofanya hapa Duniani. Nasi tutakuombea mara kwa mara! Wana Upanga, tutakukumbuka! 🙏🏾
Starehe kwa amani Baba Shewio, pumzika Baba Shewio! Vita umevipigana, mwendo umeumaliza na hakika, Imani umeishika! Mwanga wa Milele ukuangazie, upumzike kwa Amani, Ameeen! 🙏🏾🙏🏾🙏🏾😔😭😔