Padri Katika Njama za Kumuua Mpenzi wake...

Mwamakula

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2010
Posts
1,890
Reaction score
384
Bi Celestina Ananius(35) amenusurika Kuuawa na Padri ambaye kwa Sasa anaishi kwenye Makazi ya Katoliki Mbezi kwa ajiri ya Masomo.Dada huyo anasema amekuwa katika ngono na padri huyo tangia akiwa Fratel,akawa Shemasi na sasa ni padri nasuala hilo ni siri yao na wazazi wa pande mbili hadi wamezaa mtoto anaitwa Agnes(3).
Bi Celestina ambaye anaishi Dodoma alikuja Dar kumufuata Mpenzi wake huyo na kama kawada baada ya kupata huduma walikuwa na safari ya kwenda kibaha ambapo walitofautiana katika mambo yao , na Padri alikasirika na kumukanyaga na gari ya Jimbo la Katoliki kabla ya Kumushambulia kwa Panga.
Taarifa za Polisi Mkoa wa Pwani zinaonyesha kuwa Mwanamke huyo aliokolewa na Wasamalia wema na kukimbizwa Hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu!!!.Hadi sasa Padri hajakamatwa !!!!!!!!!
Hii ni Kali kuliko ya Nabii na Mtume Mwingira pale Karibu Hotel
source: Police Kibaha
 
duuh hawa viongozi ndiyo wanaoharibu taswira ya kanisa katoliki. Inabidi ashughulikiwe sio kuhamishwa jimbo ni aibu kwa kanisa letu...
 
mkuu unapokea mambo na kuyaamini kirahisi sana.

Ingekuwa siyo Padre ungeamini kirahisi, lakini kwa vile Padre kahusika naona inakuwia ngumu kuamini!!!! LOL.
Mapadre wamezidi UZINZI!
 
Mapadre wetu hawa balaa tupu yaani tangu akiwa mseminari, kwa hiyo anaadhimisha vitakatifu huku akiwa mdhambi, any way Mungu atuhurumie kwa kuwa ni wadhambi
 
leo katika kipindi cha patapata wapo redio fm.......kuwa padri wa kanisa katoliki parokia ya hombolo iliyoko dodoma kwa jina la celestine john nyaumbana....anashikiliwa na polisi kwa kosa la kutaka kumuua mpenzi wake kwa jina sista agnes huko maeneo ya kiluvya.......

chanzo kinasemekana kuwa padri huyo alimpa mimba sista agnes...na kuzaa nae mtoto....ila walizaa na dada huyo kwa siri kubwa sana....sasa wakati padri huyu yupo jijini dar kimasomo sista huyu alikuwa akimtafuta padri huyu ili kujua hatma ya maisha yake na mtoto....sasa wakati wapo dar padri huyo kukutana na mpenzi wake huyo alimuomba dada huyo watoke kidogo kwenda kutembea maeneo ya kiluvya...na klufika huko wakati wapo katikati ya poli padri huyo alishuka kwenye gali na kumshambulia sista agness kwa madhumuni ya kumuua na kupoteza ushaidi ila hakufanikiwa kumuua

source: wapo radio kipindi cha patapata
 


Ongeza maelezo namna alivyodakwa na je mtoto yuko salama. Tutaona mengi kutoka kwa hawa mapadri wenye roho ya kungonoka. Mtume Paulo aliwaonya kuwa kama hawawezi kuishi kama yeye, ni bora waoe kuliko kuwaka tamaa(kungonoka)
 
mmmh!hawa mapadri bora waruhusiwe kuoa kieleweke!
 

God Have Mercy On Us Sinners.
 
K ni kiungo hatari sana kwa afya za wanadamu...yaani ndo maana mi mapema nikaacha upadri nikajichanganya na walimwengu..maana viuno vinanivuruga akili sana
 
mmmh!hawa mapadri bora waruhusiwe kuoa kieleweke!
Si suala la kuoa au kutooa.

Kuna mapadre wasiooa na wanaishi maisha mazuri ya kitakatifu na kufanya uchungaji mzuri sana tu.

Vile vile kuna wachungaji waliooa na wanazini ovyo na kubaka. Mifano hii hapa

HII NI VIDEO YA MCHUNGAJI ALIYENASWA AKIZINI NA MWANAMKE TASA AMBAYE ALIDANGANYWA KUWA ATAPATA MTOTO!! - GUMZO LA JIJI

https://www.jamiiforums.com/mahusia...gaji-afumaniwa-na-mke-wa-mwanakondo-live.html

https://www.jamiiforums.com/jamii-p...-afumwa-akimuogesha-mke-watu.html#post3570351

https://groups.google.com/forum/?fromgroups=#!topic/mabadilikotanzania/KMXSSpme6Rk

JICHO LANGU BLOGU: MTWANGA INJILI WA MIAKA 46 ABAKA KIBINTI CHA MIAKA 14

https://www.jamiiforums.com/habari-...-mchungaji-atuhumiwa-kumbaka-mwaanafunzi.html

Tatizo ni kuwa kuna wengine wanaingia Upadre au Uchungaji kama kazi tu ya kuwapatia kipato na hawana imani ya kweli na hofu ya Mungu.

Si suala la kuoa au kutooa.
 
Hawa mapadri aisee ni bora waruhusiwe tu kuoa, haya mafundisho mengine bwana, yaani binaadamu yuko kamili, anakula anakunywa ana uwezo kifedha, halafu unamwabia asioe, kinyume kabisa na maumbile yetu wanaadamu.
tutake tusitake tendo la ndoa ni muhimu mno kama kula au kunywa. kama uko mzima lazima ulitimize. sasa kueka sheria ya kulizuia matokeo yake ndo haya.
 
Narudia tena, tatizo si la Mapadre tu, ni wote wanaoingia kwenye Utumishi wa Mungu kwa malengo ya ajira badala ya wito.

Mapadre wanaoingia kwenye utumishi wa Mungu wakiwa kweli na imani na wamevutwa na wito na kutafuta ukamilifu wapo na wanaishi vema sana, kitakatifu na wanafanya uchungaji vizuri pia.

Kwa wanaochukulia Utumishi wa Mungu Upadre/Uchungaji kama biashara, hata kwa wachungaji wanaooa yanatokea hayo.

Soma visa hivi

HII NI VIDEO YA MCHUNGAJI ALIYENASWA AKIZINI NA MWANAMKE TASA AMBAYE ALIDANGANYWA KUWA ATAPATA MTOTO!! - GUMZO LA JIJI

Mchungaji afumaniwa na Mke wa Mwanakondo LIVE.

mchungaji wa kiume afumwa akimuogesha mke watu

JICHO LANGU BLOGU: MTWANGA INJILI WA MIAKA 46 ABAKA KIBINTI CHA MIAKA 14

Mchungaji atuhumiwa kumbaka mwaanafunzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…