Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Katibu Mkuu wa TEC, Padri Dkt. Kitima akiwa kwenye mahojiano na The Chanzo amesema kuwa ule uwezo wa kuchambua masuala ya kitaifa umeshuka.
' Ule uchambuzi, kuchambua masuala, kupembua wa watu wa kawaida umeshuka. Wewe angalia sasa hivi watu wana miaka saba hatujawaongelea juu ya haki zao za msingi za kujitawala.
Hatujawaongelea uzuri wa kuwa na kitu kinachoitwa Katiba ambayo ni sheria mama ambayo kila mtu anapaswa kuwajibishwa nayo.
Hata ungewaambia watu kuwa, sasa jamani tutakuwa tuna vitabu viwili tu vinavyotawala nchi hii Quran na Biblia, ambavyo vimewekwa na muumba wenu, bado Watanzania wanaweza wakavichoma moto wakaendelea na mambo yao wanayoyataka.
Hata ukiwa na Katiba, utashi na kusudio, dhamiri na makusudio maalum ya kila aliyeko madarakani kusema hili na lile litawale, kama hiyi haipo hatuwezi kwenda.
Kwa hiyo, mimi nakubali sheria mama ni ya msingi lakini mwisho wa siku hebu angalia uhalisia uliopo. Bunge linafikiri kichama, Bunge letu la sasa ukuu wa Bunge haupo.
Umeona spika ametishwa kidogo amejiuzulu. Uchaguzi unafanya wa kumchagua mtu mmoja bungeni, eti mtu amepata kura zote za watu sijui 300 na ngapi
Hata Nyerere alikuwa hapati zote, ambaye tunaamini kweli ni Baba wa Taifa.
Unaona kabisa kwamba ule utashi wa kuwa na utawala wa sheria nchi hii haujadhamiriwa na walioko madarakani.