Padri Kitima: Bunge letu linafikiri kichama. Upeo wa kuchambua masuala ya nchi yetu umeshuka

Bunge hili liliojaa viti vya CCM ni sawa sawa na kulinganisha na timu ambayo inajiandaa kimchezo yani ikiwa mazoezini hujishindanisha pande mbili lakini ni dhahiri hakuna tofauti ukilinganisha na wanapo kutana na timu pinzani uwanjani kusaka pointi ambapo hapo sasa hujipima kweli kweli misuli, maarifa, upeo na uwezo kiakili na kimwili hapo hupata matokeo halali
 
Tangu siasa za ushindani zishike kasi ndani na nje ya chama, magwiji wa ufisadi wa CCM wamekuwa smart zaidi:

1. Wamehakikisha chama lazima kiendelee kushika dola kama suala la kufa na kupona (by hooks and crooks);

2. Rais/mwenyekiti wa chama lazima awe juu ya sheria na asiwe na mipaka katika udhibiti wa matumizi ya rasilimali na fursa zote nchini; uamuzi wake ndio amri;

3. Nafasi zote za utumishi wa umma ziwe finyu, zenye maslahi haba/duni, na kupatikana kwa upendeleo zaidi (nepotism, cronyism, patronage, uchawa, n.k.);

4. Maslahi kibao yarundikwe kwenye nafasi za kisiasa na hasa teuzi za Rais;

5. Mafungu kibao kwa wenye kazi maalum za kimtandao zinazoeleweka na zisizoelweka (uchawa, propaganda, wasiojulikana, etc.).

Akili itoke wapi katika mazingira hayo? Bunge lazima liwe la viazi. Neurosurgeon katika sekta ya umma hata awe mahiri kiasi gani asipojua kuimba mapambio ni kama taka mbele ya mwenezi.

Ndizo athari za totalitarian state yenye uongozi usiojielewa kabisa.
 
Mkuu,
Nakumbuka kaka yangu akiwa UDSM miaka ya 2008-2010 Kama sikosei sina kumbukumbu nzuri maana nilikuwa bado mdogo.

Kulikuwa na maandamano ya wanachuo sana mpaka Polisi walikuwa wanaenda kutuliza ghasia.

Kiukweli niseme miaka ile na miaka hii tuliyomaliza sisi kuna utofauti mkubwa sana yaani mwanafunzi alikuwa na confidence ya kuhoji viongozi na hakubaliani na kila jambo.
Zile piga piga na kamata kamata zimeua kile kizazi na sasa kimebaki kizazi cha kila kitu ni sawa.
 
Sahivi wamebaki chawa pekee hakuna mtu wa kuhoji zaidi ya kusifia pekee
 
Comrade umemaliza kila kitu
 
Sahivi wamebaki chawa pekee hakuna mtu wa kuhoji zaidi ya kusifia pekee
Mkuu hili tatizo mizizi yake ni nini haswa?
Yaani wasomi wa miaka ile wengi wao si wasomi kwenye makaratasi tu la hasha! Hata ukija kwenye kufanya maamuzi unaona huyu kweli ni msomi.

Wengi wetu sikuhizi tumekosa kabisa ile kujiamini na kuhoji.
 
Padre anayetetea mashoga hawezi kuipenda serikali inayopinga ushoga.
Serikali ipi inayopinga ushoga? Kama inapinga ushoga si ifanye kama serikali ya Uganda iliyotunga sheria ya kupinga ushoga kabisa....kutwa viongozi wa serikali hii wanajipeleka kuomba msaada kwenye nchi zinazo promote ushoga... unafikiria kwa kutumia makalio ndugu yangu?
 
Mkuu hili tatizo mizizi yake ni nini haswa?
Yaani wasomi wa miaka ile wengi wao si wasomi kwenye makaratasi tu la hasha! Hata ukija kwenye kufanya maamuzi unaona huyu kweli ni msomi.

Wengi wetu sikuhizi tumekosa kabisa ile kujiamini na kuhoji.
Tatizo ni huu mfumo wa kijinga, mwasisi wa huu ujinga ni Makonda, pesa za Rais na siyo za serikali lakini deni ni la taifa. Ni mambo ya kijinga sn, kila mtu anataka uteuzi alambe asali, kwanini nafasi zote zisitangazwe watu waombe wafanyiwe interview?
 
Hata kuongelea hawaongelei kabisa
 
Ni combination ya sababu Mkuu;

1. mtu amesoma na ameelimika ila kwa NJAA zake anaona akiusema ukweli ataondolewa kwenye mfumo wa ulaji.

2.Elimu yetu ni kama "indirectly" inaandaa watu tegemezi ambao wanaamini katika kupata fadhila na kusadiwa ili WASIMAME.Tuwe wakweli kua hawa waliojaa kwenye makundi ya kusifu na kuabudu kila kitu mostly ni WASOMI.

3. Watawala wamejijengea "ukuta" na kuamini kua kila mwenye mawazo na mitazamo tofauti haitakii mema nchi.

4.Tabia binafsi tu za kupenda short cut kwenye maisha na kudhani kuishi kwa kusifia hata mambo yasiyo na tija itamsaidia mtu kupiga maisha hivyo kuukataa ukweli maana atakakufa njaa.

Huu ni mtazamo wangu.
 
Uko sahihi kabisa boss, baada ya ccm kuishiwa ushawishi ndio tumeanza kuona hivi vituko.
 
It was one's making
 
Hata ukiwa na Katiba, utashi na kusudio, dhamiri na makusudio maalum ya kila aliyeko madarakani kusema hili na lile litawale, kama hiyi haipo hatuwezi kwenda.
Sikubalini na padre Kitima ktk hili. Katiba bora huwa injilinda na Ina wivu sana, humshughulikia kila atakayejaribu kuibagaza.

Ukiona katiba inategemea utashi wa viongozi ili kuiheshimu basi tambua ya kwamba katiba hiyo ni mbovu.
 
Padre anayetetea mashoga hawezi kuipenda serikali inayopinga ushoga.
Usikute na wewe unategemewa yaani, umetumia pesa za babako kusoma ili uelimike!

Nikuulize, padri ametaja jina serikali hapo?

Utakapojua maana ya bunge na Serikali, na si ajabu na maisha yako yakawa yamehitimika duniani
 
Rais/mwenyekiti wa chama lazima awe juu ya sheria na asiwe na mipaka katika udhibiti wa matumizi ya rasilimali na fursa zote nchini; uamuzi wake ndio amri;
Hili Naona ni kweli kweli kabisa
Majuzi anasimama Waziri wa Ardhi Msomi learned brother huko Ndachi Dodoma anasema Mama katoa maagizo
Wavamizi halali wapewe maeneo juu ya hati ila Wavamizi pandikizi washughilulikiwe

Sheria zipoje kama Mama anahitaji maeneo ya watu si ataifishe ijulikane moja!!
Hii nchi Sasa ni hovyo kabisa
 
huyu akae kimya watu watayatoa madhambi yake na itabidi ajiuzulu upadri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…