Padri Kitima: Unafiki na kusifia kila jambo ili kupata vyeo kutaliua Taifa

Mimi Ni mkristo lkn hii trend ya akiingia rais Muislam then RC na madhehebu mengine ya kikristo kujifanya yanamuwashia Moto sio fair.Enzi za JPM walitulia kimya na ujinga wote ule aliokua anafanya.

Pamoja na yote niliyosema lkn ujumbe wa Kitima Ni Valid.
Kitima hajawahi kutulia sema we ndo ulikua hufuatilii.Alimchana JPM mara kibao.Lkn sio yeye tu hata issue ya corona Kanisa Katoliki lilikua kinyume kabisa na JPM.Fuatilia mambo usipost kwa hisia
 
Walimfanya Nini alipowatishia kuondoa exemption Kwny magari ya Taasisi za kidini, alipowahangaisha wakina Bagonza, Niwemugizi?

Na hayo aliyoyafanya Magu leo Samia akiwafanyia RC reaction ya kanisa itakuaje?

Wacha mboyoyo
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima ametahadharisha unafiki wa kisiasa unaoendelea miongoni mwa Watanzania kwa sasa kwa kupenda kusifia kila jambo kuwa utaliua taifa.

Amesema tabia hiyo inaendelea kupata mashiko nchini kutokana na upeo mdogo wa watu kushindwa kujua misingi ya haki za binadamu na badala yake wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele .

Akizungumza leo Dar es Salaam, Septemba 30, 2022 katika kongamano la viongozi wa dini zote linaloangazia haki za binadamu nchini, kiongozi huyo amesema tabia hiyo iliyojengeka isipokomeshwa ni wazi mahusiano mazuri miongoni mwa Watanzania yanaenda kupotea.

"Unafiki unaharibu nchi, unafiki wa kisiasa uliopo miongoni mwa Watanzania kupenda kusifia viongozi ili tu kujipendekeza wapate vyeo unaenda kuliua Taifa na tatizo hili linaendelea kwa sababu watu hawajui misingi ya haki za binadamu," amesema Padri Kitima

Kiongozi huyo wa kiroho amesema hata kujitoa kwenye mahakama ya haki iliyopo Arusha na kuwahamisha wananchi kutoka Loliondo kwenda Handeni mkoani Tanga ni uvunjivu wa haki za binadamu.

"Kwa sababu nchi imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu haki za binadamu," amesema

Amesema wao kama viongozi wa dini baada ya kuona tabia hiyo hususan miaka mitano iliyopita, mwaka 2020 walianza kuandika kitabu Cha elimu ya haki za binadamu kwa lengo la kuanza kutoka elimu watu wote.

"Haki za binadamu haziombwi, zinapiganiwa, dini ni kiungo muhimu na tumeona tufanye hivi na tunatarajia kuwafikia viongozi 16,000 nchi nzima na kushuka kwa Watanzania wote," amesema

Chanzo: Mwananchi
Baba Padri uko sahihi kabisa.
 
Mapadre fanyeni kazi ya Mungu.

Maoni yenu kwa sasa yamechafuka.
Kwani hiyo kazi ya Mungu anawafanyia kina nani? Watu wenyewe si ndiyo sisi hawa hawa machawa, unazeeka vibaya[emoji23]
 
Padri yupo sahihi...lakini kwa nini hakutuyasikia haya kipindi cha JPM,ilifika hatua hadi anapewa mic kanisani ahutubie.....huku wakina Pengo wakimtaka Makonda awe raisi wa awamu ya Sita.
Ni kweli Padri Kitima yupo sahihi,"Unafiki wa kisiasa unaondelea miongoni mwa watanzania,utaliangamiza taifa"
inaonekana wewe ni mgeni na huyu jamaa,katika viongozi wa dini waliokuwa na uwezo wa kuyaongea haya ni huyu.
 
Mimi Ni mkristo lkn hii trend ya akiingia rais Muislam then RC na madhehebu mengine ya kikristo kujifanya yanamuwashia Moto sio fair.Enzi za JPM walitulia kimya na ujinga wote ule aliokua anafanya.

Pamoja na yote niliyosema lkn ujumbe wa Kitima Ni Valid.
Waislam huwa wanachanganya dini na siasa🤣🤣🤣
 
Walimfanya Nini alipowatishia kuondoa exemption Kwny magari ya Taasisi za kidini, alipowahangaisha wakina Bagonza, Niwemugizi?

Na hayo aliyoyafanya Magu leo Samia akiwafanyia RC reaction ya kanisa itakuaje?

Wacha mboyoyo
ETi mboyoyo, 🤣
Ndio nini?
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima ametahadharisha unafiki wa kisiasa unaoendelea miongoni mwa Watanzania kwa sasa kwa kupenda kusifia kila jambo kuwa utaliua taifa.

Amesema tabia hiyo inaendelea kupata mashiko nchini kutokana na upeo mdogo wa watu kushindwa kujua misingi ya haki za binadamu na badala yake wanatanguliza maslahi yao binafsi mbele .

Akizungumza leo Dar es Salaam, Septemba 30, 2022 katika kongamano la viongozi wa dini zote linaloangazia haki za binadamu nchini, kiongozi huyo amesema tabia hiyo iliyojengeka isipokomeshwa ni wazi mahusiano mazuri miongoni mwa Watanzania yanaenda kupotea.

"Unafiki unaharibu nchi, unafiki wa kisiasa uliopo miongoni mwa Watanzania kupenda kusifia viongozi ili tu kujipendekeza wapate vyeo unaenda kuliua Taifa na tatizo hili linaendelea kwa sababu watu hawajui misingi ya haki za binadamu," amesema Padri Kitima

Kiongozi huyo wa kiroho amesema hata kujitoa kwenye mahakama ya haki iliyopo Arusha na kuwahamisha wananchi kutoka Loliondo kwenda Handeni mkoani Tanga ni uvunjivu wa haki za binadamu.

"Kwa sababu nchi imeridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu haki za binadamu," amesema

Amesema wao kama viongozi wa dini baada ya kuona tabia hiyo hususan miaka mitano iliyopita, mwaka 2020 walianza kuandika kitabu Cha elimu ya haki za binadamu kwa lengo la kuanza kutoka elimu watu wote.

"Haki za binadamu haziombwi, zinapiganiwa, dini ni kiungo muhimu na tumeona tufanye hivi na tunatarajia kuwafikia viongozi 16,000 nchi nzima na kushuka kwa Watanzania wote," amesema

Chanzo: Mwananchi
NJAA KALI CHAWA WAMETOTOLEWA KWA WINGI NCHI HII
 
Mimi Ni mkristo lkn hii trend ya akiingia rais Muislam then RC na madhehebu mengine ya kikristo kujifanya yanamuwashia Moto sio fair.Enzi za JPM walitulia kimya na ujinga wote ule aliokua anafanya.

Pamoja na yote niliyosema lkn ujumbe wa Kitima Ni Valid.
Kama huwa unamskiza Pd Kitima vizuri au kama unakumbukumbu vizuri.huwa anaongea ukweli hata enzi za JPM km kuna Jambo alikuwa anaongea.haogopagi mtu
 
Unafiki haupo tu kwa wanasiasa ata viongozi wa dini ndio wamekuwa wanafiki wakubwa.
 
Hoja ya padri Kitima ni sahihi lakini wakati huu hoja yake inakosa nguvu sababu kanisa katoliki, TEC maaskofu na mapadri wamepoteza sifa ya kimaadili kusema haya.

Sasa watu washangaa awamu ya upande huu wanazungumza na kupaza sauti ikifika awamu ya upande ule hawa hawazungumzi tena, wanakua kimya.
Na hii ni unafiki na kujipendekeza kwa viongozi wa dini au tuite nini?
 
Mimi Ni mkristo lkn hii trend ya akiingia rais Muislam then RC na madhehebu mengine ya kikristo kujifanya yanamuwashia Moto sio fair.Enzi za JPM walitulia kimya na ujinga wote ule aliokua anafanya.

Pamoja na yote niliyosema lkn ujumbe wa Kitima Ni Valid.
Unasahau haraka sana. Yani umesahau wakati wa Magufuli, KKKT waliandika waraka mzito sana wa kuikosoa serikali.

Umemsahau huyu huyu Padri Kitima akiikosoa serikali kuhusu Covid19?

Mbona makanisa yote mawili makubwa(RC na KKKT) yalikemea sana serikali enzi ya JPM, au ulikuwa umelala?
 
Back
Top Bottom