Padri Kitima: Unafiki na kusifia kila jambo ili kupata vyeo kutaliua Taifa

Tuwache siasa za udini pembeni tuangalie uhalisia.

Naomba tumsikilize huyu mtumishi wa Mungu tuna cha kujifunza juu ya ustawi wa maisha yetu kama watanzania.
Your browser is not able to display this video.
 
Naona masheh wameamua Rasmi kupambana na warumi!!!

Vuguvugu lilianza pale masheh walipoamua kuwaaachia masheh waliotuhumiwa kwa ugaidi!!

Juzi mmoja kasema wazi Kuwa mapadri zaidi ya hamsini wameuawa Lakini VYOMBO vya habari havitangazi!

Leo kuna kesi kadhaa za ulawiti!!


Samiah mama YANGU nakuonya !!!Acha kupambana na Hawa WATU!we Tulia coz waliyemuamini akapewa kutawala aliharibu Sana!wanamaumivu walipoteza utawala pale mtu wao alipo itwa na MUNGU!Wana uchungu Sana!!!


Wakiamua huwezi washinda can masheh BADO hawajatengeneza Taasisi imara ya kutawala Dunia kama wao!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe katiba mpya"
 
Chawa wataanza kumparua Padre sasa hivi bila kupima uzito wa ujumbe wake.
Alikuwa wap enzi za mwendazake akat masifio yalifika Hadi juu ya kitu Cha enzi
Et mh Mungu pumbavu mwambie kitima atulie
 
Huu ugonjwa wa uchawa wa viongozi aliotuletea magu unaliteketeza taifa.

Kabla yake ilikua serikali ya ccm, alipoingia ikawa ya magu sio ccm tena, sasa hivi imehamia mama samia sio ccm tena

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Mwambie maoni yake ni mazuri Ila aanzie ndani kwake kwanza maana Mapadri wamekuwa wanalawiti watoto na wengine wanauwawa kiutata sana.
Nasema uongo ndugu zanguuuu
 
Labda umemfahamu leo padre
 
Rudi kwenye mada usichanganye mafaili kukwepa ukweli!!!
 
Rais Samia, kama anataka uongozi wake uwe na tija kubwa, ni lazima awaondoe wanafiki wote ndani ya Serikali yake.

Ndani ya Serikali wamejaa watu wanafiki. Watu watoa rushwa ya sifa. Sifa wanazozitoa kwa Rais kw kila kitu, hata zisipostahili, ni rushwa ya sifa kwa Rais.

Kiongozi yeyote ana haki ya kusifiwa anapofanya jambo jema la pekee, lakini kumsifia Rais kwa kila kitu, tena kwa baadhi ya mambo ambayo ni ya kawaida kabisa au hata kwa yale ambayo yamefanyika vibaya, ni unafiki, ujinga, uwendawazimu, na rushwa kwa kiongozi anayesifiwa, na njia ya kumpofusha mtawala.

Hongera sana Baba Kitima, kwa kuunena ukweli.
 
nafikiri umeanza kumjua jana
 
Ifike mahali sasa viongozi wawe wanatuma maombi ya kazi, interview ifanywe na wananchi hadharani na wapangiwe kazi na kusimamiwa na hata kufukuzwa na wananchi, hii teuanateuana inatuumiza sana
 
Yeye na Kanisa lake pia ni Wanafiki. Wakati wa Mwendazake ambaye ndiye mwanzilishi wa hii tabia hawakudiliki kusema kitu. Sana sana walimsifia.

Kwenye hili siliungi mkono Kanisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…