PostGE2025 Padri Kitima: Utawala ni dhamana unayopewa na wananchi na lazima uwasikilize wananchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

Akizungumza katika Misa Takatifu ya kuwaombea marehemu na waathirika wa matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Padri Charles Kitima amewakumbusha viongozi na wananchi kuwa utawala wa kisiasa ni dhamana inayotoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kuwasikiliza wananchi na kuheshimu mfumo wa vyama vingi pamoja na michakato halali ya kukabidhiana madaraka kupitia uchaguzi huru na wa haki.

Padri Kitima ameangazia uovu wa wizi wa kura na vitendo vya kuchakachua matokeo, akionya kuwa vitendo hivyo huzaa dhambi na madhara makubwa yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi na kwamba ni lazima kung'oa mzizi wa dhambi hiyo ya kiburi na kurejesha misingi ya heshima, upendo, na utawala wa sheria.
 
My friends ladies and gentlemen,

viongozi wa taifa letu, kupitia serikali sikivu ya CCM wanafanya hayo kwa maneno na vitendo tangu uhuru wa taifa letu, na kwahivyo hakuna jipya kwenye humilia hiyo ya muheshimiwa sana baba padre Dr Charles Kitima.

Ni muhimu sana kama viongozi, kukemea uovu wa aina zote ikiwa ni pamoja dhuluma za kingono miongoni mwa viongozi wa dini dhidi ya vijana wadogo na huo ndio uongozi wa kweli kiroho na kimwili na itapendeza zaidi 🐒
 
My friends ladies and gentlemen,

viongozi wa taifa letu, kupitia serikali sikivu ya CCM wanafanya hayo kwa maneno na vitendo tangu uhuru wa taifa letu, na kwahivyo hakuna jipya kwenye humilia hiyo ya muheshimiwa sana baba padre Dr Charles Kitima.

Ni muhimu kukemea uovu wote ikiwa ni pamoja dhuluma za kingono miongoni mwa viongozi wa dini na huo ndio uongozi wa kweli kiroho na kimwili na itapendeza zaidi 🐒
Gentleman, umeona nondo za FATHER KITIMA?

Anatukemea sisi majizi ya kura bila woga.

Mungu aninusuru, mwaka jana niliiba kura na kukimbia na masanduku vichakani :1Head:
 
"Kuiba kura ni dhambi au si dhambi.? Msipoacha dhambi ya kuiba kura mtauana kweli kweli."

Asante Fr.Kitima
 
Gentleman, umeona nondo za FATHER KITIMA?

Anatukemea sisi majizi ya kura bila woga.

Mungu aninusuru, mwaka jana niliiba kura na kukimbia na masanduku vichakani :1Head:
Nondo gani sasa hapo kwa mfano?

muheshimiwa sana baba padre Dr. Charles Kitima hanaga jipya kabisa zaidi ya kurudia rudia masuala ya yale yale ya kisiasa, sambamba na chama cha demokrasia na maendeleo.

ndio maana hua nasisitiza humu jukwaani kwamba muheshimiwa sana baba padre Dr Charles Kitima ni katibu mkuu kivuli wa chadema na ndio maana huzungumza mambo yale yale, kwa tone na body language ile ile inayotumiawa na chama cha demokrasia na maendeleo na kujaribu kuliingiza kanisa katoliki lote chadema, hiyo haitawezekana.

Anapenda siasa, madaraka na vyeo kuliko hata wito wake kwa kanisa 🐒
 
Hii nchi hapa tulipo lazima damu zimwagike tena ndio watawala wasikie sauti za wananchi.

Kidemocrasia tu imeshashindikana. Samia hawezi ruhusu CCM imufie mkononi, atailinda kwa nguvu zote. Atakae fuata baada yake nae vilevile. CCM hata kama wanaharibu hawasikii kabisa.

Na ndio maana watu wanatekwa wanapotezwa, hakuna mwana ccm hata mmoja wa kukemea hayo mambo. Hadi najiuliza CCM wanaipenda kweli hii nchi ama wameshakuwa na mioyo migumu kiasi cha kutaka kuongoza mawe badala ya binadamu?
 
Nondo gani sasa hapo kwa mfano?

muheshimiwa sana baba padre Dr. Charles Kitima hanaga jipya kabisa zaidi ya kurudia rudia masuala ya yale yale ya kisiasa, sambamba na chama cha demokrasia na maendeleo.

ndio maana hua nasisitiza humu jukwaani kwamba muheshimiwa sana baba padre Dr Charles Kitima ni katibu mkuu kivuli wa chadema na ndio maana huzungumza mambo yale yale, kwa tone na body language ile ile inayotumiawa na chama cha demokrasia na maendeleo na kujaribu kuliingiza kanisa katoliki lote chadema, hiyo haitawezekana.

Anapenda siasa, madaraka na vyeo kuliko hata wito wake kwa kanisa 🐒

Hakika kama wewe mwenyewe hujitambui kuwa ni mwendawazimu, basi tatizo lako litakuwa ni kubwa na baya zaidi ya uwendawazimu!!

Ungekuwa na akili japo kidogo, ungetambua kuwa:

Tendo ovu haijalishi limesemwa na nani, iwe limesemwa na CHADEMA, Padre, mchungaji, askofu, mwanaCCM au shekhe, inabakia kuwa ni uovu. Kukemea uovu inatakiwa kufanywa wakati wote, bila ya kujali uovu huo umekemewa mara ngapi. Hata tunapoenda ibadani, siyo kwamba kila siku waumini wanaenda kuambiwa mambo mapya, bali wanaenda kukumbusha yale yale ambayo wameyasikia mara nyingi. Sheria ya Mungu ni ile ile siku zote.

Kwa akili ya punguani Tlaatlaah, padre au shekhe akikemea wizi au uzinzi mara nyingi, analalamika kuwa hayo ni maneno yamekuwa yanasemwa siku zote.

Wizi wa kura ni dhambi, maadamu bado upo, watumishi wa Mungu, ni wajibu wao kuendelea kukemea siku zote. Na hata wizi huo ikitokea imetoweka, bado watumishi wa Mungu wana haki ya kuendelea kuonya, ili watu wasirudi tena kwenye uovu.

MAOMBI YETU:
BABA WA MBINGUNI, tunaomba uwajalie hekima watawala waliojaa mioyo ya uovu kiasi cha kuwaua binadamu wenzao ili wizi wao wa kura usihojiwe, watambue kuwa WEWE MUNGU wa haki upo, na matendo yao ni kinyume cha mapenzi yako. Tunaomba kama hawatataka kujutia uovu wao na kuwa na dhamira ya kujitenga na uovu, mkono WAKO wenye mamlaka ukawafikie wote walio na kiburi cha kuyatwaa mamlaka kwa gharama ya damu za watu.

Wenye akili wote, hasa wale wanaotumika na watawala waovu, uwakumbushe hekima yako,

"Yakufaa nini kuyapata yote ya Dunia, halafu ukaupoteza uzima wa milele?'

Baba Mungu uwajalie hekima watu wako ambao kutokana na tamaa zao na wakati mwingine vitisho toka kwa watawala, kiasi cha kukubali kutumika na watawala waovu kuwaua wanadamu wenzao, Uwajalie ujasiri watu hao, kutokukubali kuingizwa kwenye jehanamu ya milele kutokana na amri na maelekezo wanayopewa na watawala waovu. Mioyo yao isikilize amri yako kuliko ya watawala waovu wa Dunia, wakikumbuka maagizo yako;
"Inapasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu", na lile jingine, "amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu, akamsahau BWANA MUNGU".
 
Gentleman,
elezea porojo zako kwa heshima tu jukwaani, bila kujipiga kifua, mihemko wala makasiriko na itapendeza zaidi 🐒
 
Aliyeondoka wabunge wote pinzani akabakisha wa chama kimoja ,hamkumuandama ..Mjinga wenu mnaona eti mwanamke ni dhaifu.

Nyie mmefanya maamuzi ya vurugu na wenzenu wamekabiliana nayo ,kwa nn mnaleta lawama na huruma ,kama mna nia ya dhati andamaneni tena mchome mali za watu ...Sio taarabu tu kila siku kisa mmekosa bandari.

Mlivyokuwa wajinga ,hamuoni hata takwimu za juzi kwamba bandari imepanda sana nyie mnapuuza ,sifieni kwenye ukweli sio kuongea chuki tu kila siku.
 
viongozi wa taifa letu, kupitia serikali sikivu ya CCM wanafanya hayo kwa maneno na vitendo tangu uhuru wa taifa letu, na kwahivyo hakuna jipya kwenye humilia hiyo

Hapo umekiuka mwongozo wako ulioutoa usiku kwenye jukwaa hili kuhusu defective political theory of change. Jisahihishe.
 
Nondo gani sasa hapo kwa mfano?

muheshimiwa sana baba padre Dr. Charles Kitima hanaga jipya kabisa zaidi ya kurudia rudia masuala ya yale yale ya kisiasa, sambamba na chama cha demokrasia na maendeleo.

ndio maana hua nasisitiza humu jukwaani kwamba muheshimiwa sana baba padre Dr Charles Kitima ni katibu mkuu kivuli wa chadema na ndio maana huzungumza mambo yale yale, kwa tone na body language ile ile inayotumiawa na chama cha demokrasia na maendeleo na kujaribu kuliingiza kanisa katoliki lote chadema, hiyo haitawezekana.

Anapenda siasa, madaraka na vyeo kuliko hata wito wake kwa kanisa 🐒
Nonsense
 
Back
Top Bottom