PostGE2025 Padri Kitima: Utawala ni dhamana unayopewa na wananchi na lazima uwasikilize wananchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Tuliwabeza Rwanda, Kenya kwamba wanaukabila. Tukajinasibisha kuwa Tanzania imefuta ukabila, udini na ukanda. Hatukuelewa kwamba ukabila, na udini hakuna kitu zaidi ya itikadi moja ambayo ndio inacement muunganiko wa watu sawa na itikadi ya chama cha siasa. Itikadi yoyote inaamini katika kuwaongoza wengine. Ulaya wameondokana na itikadi hizo kwa kuzifanya serikali zao kuwa na nguvu za kiutawala kuliko itikadi au kundi lolote ndani ya nchi.
Tanzania nguvu tumeziacha kwenye chama. Chama kina itikadi yake na kinajinasibu kama kikundi fulani. Uadui uliopo kati ya ccm na chadema hauna tofauti na uadui wa wahutu na watusi. Uadui ambao mmoja yuko tayari kuua mpinzani ili aendelee kutawala. Kenya tuliokuwa tunawacheka kwamba wanaukabila kwa sasa taratibu wanaiachie serikali kuwa na nguvu kuliko kundi lolote lile. Zambia na Malawi nguvu za kiutawala zimepelekwa serikalini hivyo hofu ya kundi fulani kutawala imetoweka, wananchi wamebaki na nguvu zao za kumweka wanaye mtaka madarakani. Tanzania nguvu ziko kwenye chama na serikali imekuwa zana ya kutumika na kundi la watawala. Uhasama wa CHADEMA na CCM hauwezi kuondoka kwa maridhiano au kuwanyamazisha chadema ikiwa nguvu ya kuongoza nchi itabaki ccm badala serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…