Padri Kitima: Wagombea walikuwa wengi kwa sababu walitengenezwa kuondoa ushindani

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, amebainisha kuwa mchakato wa uchaguzi na mfumo wa kisiasa umekuwa ukivurugwa mara kwa mara tangu mwaka 2019 hadi kufikia mwaka 2025.

Akizungumza leo Septemba 15, 2026 katika mjadala kuhsu Demokrasia na Katiba Mpya Tanzania, ameeleza kuwa hali hiyo ndiyo iliyosababisha kuwepo kwa wimbi kubwa la wagombea wasio na tija badala ya kuwa na ushindani wa dhati wa kisiasa, amesisitiza kuwa kuanzia mwaka 2019 na 2020, misingi ya ushindani ilianza kuharibiwa na kuongezeka zaidi katika uchaguzi wa 2025, hatua iliyoondoa msisimko na maana halisi ya uchaguzi wa kiraia.

Padri Kitima amebainisha kuwa vurugu hizo hazikuanzia kwenye uchaguzi mkuu pekee, bali zilianza ndani ya vyama vyenyewe vya siasa kupitia michakato ya ndani iliyovurugwa. Hali hiyo ilipelekea baadhi ya vyama kukataa kushiriki na vingine kuishia kusindikiza mchakato tu, jambo lililoharibu misingi ya demokrasia kabla hata ya wananchi kwenda kupiga kura.

Aidha, Padri Kitima amejibu hoja kuhusu kuwepo kwa uchaguzi kwa kukiri kuwa japo vituo vilifunguliwa na wananchi wakapiga kura, swali la msingi linasalia kwenye idadi ya walioshiriki na jinsi ushindani ulivyovurugwa.

Padre Kitima bana, dah!
hajazungumzia kabisa changamoto mizengwe ya kwenye uchaguzi wa jumuiya, kanda, dekania, vyama vya kitume na baraza la walei jimbo kwenye kanisa moja, takatifu, katoliki la mitume??

Inashangaza sana, inasikitisha sana nyani kutoona kundule ila anaona boriti kwa wengine bila kutoa kibanzi jichoni pake.
Unafiki ni kipaji 🐒
 
Kwanini wewe usizungumzie
 
Kwani chaguzi za vyama vya kitume kulitokea mauaji?
 
Saa100 ana DNA za Idd Amini ,aliyewahi kuwa Rais mbabe wa Uganda
 
Ana hoja ila wafia timu hawatamuelewa hasa ukizingatia hoja imetolewa na mgalatia.
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, amebainisha kuwa mchakato wa uchaguzi na mfumo wa kisiasa umekuwa ukivurugwa mara kwa mara tangu mwaka 2019 hadi kufikia mwaka 2025.

Akizungumza leo Septemba 15, 2026 katika mjadala kuhsu Demokrasia na Katiba Mpya Tanzania, ameeleza kuwa hali hiyo ndiyo iliyosababisha kuwepo kwa wimbi kubwa la wagombea wasio na tija badala ya kuwa na ushindani wa dhati wa kisiasa, amesisitiza kuwa kuanzia mwaka 2019 na 2020, misingi ya ushindani ilianza kuharibiwa na kuongezeka zaidi katika uchaguzi wa 2025, hatua iliyoondoa msisimko na maana halisi ya uchaguzi wa kiraia.

Padri Kitima amebainisha kuwa vurugu hizo hazikuanzia kwenye uchaguzi mkuu pekee, bali zilianza ndani ya vyama vyenyewe vya siasa kupitia michakato ya ndani iliyovurugwa. Hali hiyo ilipelekea baadhi ya vyama kukataa kushiriki na vingine kuishia kusindikiza mchakato tu, jambo lililoharibu misingi ya demokrasia kabla hata ya wananchi kwenda kupiga kura.

Aidha, Padri Kitima amejibu hoja kuhusu kuwepo kwa uchaguzi kwa kukiri kuwa japo vituo vilifunguliwa na wananchi wakapiga kura, swali la msingi linasalia kwenye idadi ya walioshiriki na jinsi ushindani ulivyovurugwa.
Father Kitima naye kaanza kuongea kwa woga. Dah nchi ngumu hii. Anaogopa kunyoosha maneno kabisa. Anashindwa kusema hakukuwa na uchaguzi na anaogopa kutaja kuwa CHADEMA ndio waliojiondoa kana kwamba hajui ni chama gani kilijiondoa.
 
Wewe una ujasiri wa kuzungumza kama yeye au unabwabwaja tu?
 
Inasikitisha sana kupoteza fedha zetu za KODI kwa FUTUHI za UCHAFUZI.
 
Back
Top Bottom