Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesema dhana ya maridhiano nchini inapaswa kuanza kwa kukiri na kukubali ukweli kuhusu matatizo yaliyopo. Akifafanua kuhusu maana ya maridhiano, amesema neno hilo linapaswa kueleweka kwa upana, akitumia mfano wa neno la Kiingereza “reconciliation”, ambalo kwa mtazamo wa Wakristo na Waislamu linahusisha kwanza hatua ya kukiri makosa kabla ya kufikia hatua ya kupatana.
Padre Kitima amesema ili kufikia maridhiano ya kweli, ni muhimu kwa taifa kukubali kuwepo kwa matatizo yanayohitaji kutatuliwa, akitaja mkwamo wa kisiasa ambao, kwa maelezo yake, umewaathiri wananchi.
Amesema tatizo haliwezi kutatuliwa ikiwa ukweli kuhusu hali iliyopo hautakubaliwa, akisisitiza kuwa wananchi ndio wamekuwa waathirika wa changamoto hizo, badala ya kuangalia maslahi ya makundi au watu wanaonufaika na hali iliyopo.