Niseme nini juu ya kifo cha Fr. Mbiku. Hakika jina lako si dogo katika Taifa la Mungu.
Itoshe kusema, Mungu wetu ujuaye siku zetu za hapa Duniani, tulipozaliwa uliweka karama zako ndani yetu. Ni neema pia kuzifahamu karama hizi na kuzifanyia kazi kadiri ya mpango wako. Tunakushukuru Mungu, kwa zawadi ya Fr. Mbiku maana kwa kupitia kwake ulilijenga Kanisa lako na kuueneza ujumbe wako kwa wanadamu wote.
Tunaomba sasa umpokee na kumpumzisha mtumishi wako katika ufalme wako. Uyatazame mema yake ili yawe utakaso wa pale alipopungukiwa.