Padri Rwegoshora kesi ya mauaji ya Asimwe imebainika hana tatizo la Akili, Mahakama kuruhusu Kesi kuendelea

Padri Rwegoshora kesi ya mauaji ya Asimwe imebainika hana tatizo la Akili, Mahakama kuruhusu Kesi kuendelea

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mtuhumiwa namba moja wa kesi ya mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Asimwe Novat aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu, Padri Elipidius Alfred Rwegoshora, ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa tisa aliyepelekwa Isanga mkoani Dodoma, ili achunguzwe akili yake kufutia ombi la mawakili wake, imethibitika hana tatizo la ugonjwa wowote wa afya ya akili.

1739797466145.png
Taarifa hiyo imesomwa Mahakamani na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mheshimiwa Gabriel Malata, amesema taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa afya ya akili ya mtuhumiwa huyo ambaye leo ameletwa mahakamani pamoja na watuhumiwa wengine nane kuwa imesainiwa na Daktari Bingwa wa Hospitali ya Milembe, Enock Changarawe.

Soma: Kesi ya 'mauaji ya Asimwe' yasogezwa mbele Padri akapimwe Akili kwanza

Amesema kufuatia matokeo ya taarifa uchunguzi kuwa Mahakama haina kikwazo cha kuanza kusikiliza kesi hiyo inayovuta hisia za watu wengi walioko kwenye maeneo ya mkoa Kagera.

Baada ya Mheshimiwa Jaji Malata kusomwa taarifa hiyo upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bi. Ajuaye Bilishanga, aliomba taarifa ya matokeo ya uchunguzi ipokelewe kama moja ya vielelezo vya ushahidi katika kesi hiyo.

Ombi hilo limepingwa na wakili wa mshitakiwa huyo Mathias Rweyemamu, aliyeomba kielelezo hicho kisipokelewe na kutumika kama kielelezo cha ushahidi kuanzia hatua za mwanzo za usikilizwaji wa kesi hiyo badala yake kitumike kama kielelezo cha ushahidi wa ziada.

Wakili wa Serikali Mkuu Bi. Bilishanga amesema kielelezo hicho kinatakiwa kupokelewa kwa kuwa ombi la kumpeleka Isanga mtuhumiwa Padre Elipidius Rwegoshora lilitolewa na upande wa mawakili wa utetezi hivyo akaomba mahakama katika kutoa maamuzi ya pingamizi la mawakili hao izingatie hilo huku akinukuru vifungu mbalimbali vya sheria.

Mheshimiwa Jaji Malata katika kutoa maamuzi ya maombi hayo madogo amesema kielelezi cha taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa akili ya mtuhumiwa namba moja kuwa lazima kipokelewe kama ushahidi ili taratibu za usikilizwaji wa kesi ziweze kuendelea hivyo akaeleza kuwa kitakuwa kielelezo namba moja.

Chanzo: ITV
 
Mapàdri wanapitia mchujo mkali huko seminary kabla ya kupewa upadre. Asijifanye chizi huyo nyonga kabisa.
 
Kwa hiyo baada ya kula mchongo wa mauaji ndio akakosa akili?
 
Mapàdri wanapitia mchujo mkali huko seminary kabla ya kupewa upadre. Asijifanye chizi huyo nyonga kabisa.
Mapadre nao ni watu. Lazima tu watakuwa na matatizo yanayo wapata watu!
Ila kwenye vipimo vya afya ya akili ilibidi tuambiwe walitumia parameters zipi!!
Make kwa uelewa wangu wa mental health issues ile tu kuwaza na zaidi kushiriki mchakato wa kumuua mtoto wa miaka 2.5 ni inference muhimu.
 
Back
Top Bottom