Padri Titus Amigu: Kwanini tunasheherekea Sikukuu ya Krismasi?

Padri Titus Amigu: Kwanini tunasheherekea Sikukuu ya Krismasi?

Jackwillpower

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2017
Posts
2,467
Reaction score
3,687
Heri ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya

KITABU: ZIJUE BARABARA SIKUKUU ZA NOELI NA PASAKA

Na. Padri Titus Amigu.
Chapa - Benedict publication Ndanda - Peramiho -
Juni 2000.

KRISMASI: Pg. 56.

..... Basi, ili kuwa na umoja waamini wapate kusherekea kuzaliwa kwa Yesu, Kanisa likajiwekea tarehe 25 Decemba. Hii haina maana kuwa Desemba ndio mwezi rasmi alipozaliwa Krsto, ila imewekwa hapo kwa sababu za kihistoria.

Yafaa tupitie historia hiyo kifupi. Katika siku za mwisho za dola ya kipagani ya kirumi, ibada za kuabudu Jua zilikuwa zikifanyika sana. Mjini Roma dini ya Mithras, mungu - jua wa kiajemi, ilistawi sana. Kaisari Aurelian akajengesha hekalu la jua lisiloshindika, mnamo mwaka 274. Sikukuu kubwa ya mungu - jua, ilifanyika kila tarehe 25 Desemba, siku ambayo tabia ya kupungua pungua kwa mwanga wa jua ilikoma, na hivyo kuanza kuongezeka tena, yaani, ilikuwa kama siku ya kuzaliwa upya jua.

KITABU: BUSTANI YA KATEKISTA

Ukurasa - 73.

Swali: JE YESU ALIZALIWA TAREHE 25 DESEMBA?

Jibu: Kwa kweli, hakuna anayejua tarehe ya kuzaliwa Kwa Yesu. Tarehe 25 Desemba ilikuwa sikukuu kubwa ya kwa wapagani, walikuwa wakifanya IBADA zao kwa MUNGU JUA.

Kwenye karne ya IV mwaka 336 baada ya Kristo, viongozi wa Kanisa walionelea, siku hiyo, washerehekee kuzaliwa kwa Yesu Mwanga, Nuru ya ulimwengu. LENGO KUBWA lilikuwa kuwahusisha pia wapagani katika kunshangilia Yesu badala ya miungu ya uongo......
FB_IMG_1735070969128.jpg

FB_IMG_1735071040878.jpg

Vitabu hivi vipo maktaba au bookshop za RC vinauzwa ili kuwasaidia wenye nia ya kutaka kujua.

NA HII SIKU IMEANDIKWA KATIKA BIBLIA KABLA YA KRISTO, ILISHEREKEWA NA WAPAGANI WA BABEL ZAMA HIZO.

Yeremia 52:31-34
Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika....
mwezi wa kumi na mbili siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani.

Akasema naye maneno mazuri, akaweka kiti chake juu ya viti vya wafalme waliokuwa pamoja naye huko Babeli.Naye akabadili mavazi yake ya gerezani, akala chakula mbele yake daima, siku zote za maisha yake.Na kwa posho yake, alipewa posho ya daima na mfalme wa Babeli; kila siku alipewa posho hata siku ya kufa kwake, siku zote za maisha yake.

Licha ya yote, Biblia haijatoa kibali icho cha kukristisha upagani wala kibali cha kusherekea siku ya kuzaliwa ya Bwana Yesu. Wanaofanya hivo hawajui watendalo.

Biblia imeonya shiriki kati ya ukristo na upagani.

14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17 Kwa hiyo,Tokeni kati yao,Mkatengwe nao, asema Bwana,Msiguse kitu kilicho kichafu,Nami nitawakaribisha.
18 Nitakuwa Baba kwenu,Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,asema Bwana Mwenyezi. (2Wakorintho 6:14-18)

Ebu jaribu kuhoji haya kibiblia:-

Fadher christmas(santaclaus katokea wapi ktk ukristo?
Boxing day ni gani?
Christmass trees imetokea wapi?
Mayai na sungura ni vipi?
FB_IMG_1735104426319.jpg

Najua kwa ushahidi huu bado utabisha lkn huo ndo ukweli, wewe endelea kujinyonga na tai ya dini shingoni ila mwenye macho ataona.

Bwana akubariki kwa kusoma.
 
Ukristo ulishakuwa corrupted kitambo sana

Shetani aliahidi atapanda juu pande za kaskazi

Makanisa yote yameshaingiliwa , Illuminati wameshajipenyeza na wanaongoza ibada na wameshaweka alama zao
 
Ukristo ulishakuwa corrupted kitambo sana

Shetani aliahidi atapanda juu pande za kaskazi

Makanisa yote yameshaingiliwa , Illuminati wameshajipenyeza na wanaongoza ibada na wameshaweka alama zao
Roman Catholic imejaa upagani mwingi
 
Mwenye masikio na asikie
Mwenye macho na aone
 
Sio Roman tu ni ukiristo wote.
Hata uislamu pia

Zile Nyota na mwezi Unajua zimetoka wapi hizo alama?

Sikukuu ya maulidi Unajua imetoka wapi

Ibada ya jiwe jeusi pale maka Unajua ni ya wapagani?
 
Hata uislamu pia

Zile Nyota na mwezi Unajua zimetoka wapi hizo alama?

Sikukuu ya maulidi Unajua imetoka wapi

Ibada ya jiwe jeusi pale maka Unajua ni ya wapagani?
Sio alama za uislamu na hazitumiwi katika ibada , msikiti mingi mkubwa haina.
 
Ukishindwa Kuhubiri habari za Kristo, lazima uangukie kwenye Habari za kufikirika kama hizi.

Kwani Roman Catholic wenyewe wanaadhimisha Christmas kwa sababu gani?

Nimetoka kushiriki Misa Asubuhi hii, Yule Padri kaongea sana ila sikusikia mahala alipowananga Wasiosherehekea Christmas...

Ila Wasiosherekea wamekimbilia JF kutusema, Aiseee.
 
Ukishindwa Kuhubiri habari za Kristo, lazima uangukie kwenye Habari za kufikirika kama hizi.

Kwani Roman Catholic wenyewe wanaadhimisha Christmas kwa sababu gani?

Nimetoka kushiriki Misa Asubuhi hii, Yule Padri kaongea sana ila sikusikia mahala alipowananga Wasiosherehekea Christmas...

Ila Wasiosherekea wamekimbilia JF kutusema, Aiseee.
Kwahiyo Hawa wakatoliki ni waongo ?
FB_IMG_1735071040878.jpg
 
Back
Top Bottom