House4Sale Pagala la kisasa, Bei imepungua (pugu)

Naomba ramani yake nimeipenda,nami nina site yangu inasize sawa na icho kiwanja
 
mkuu ni huyu huyu,namba na kila kitu vyake tulifika site nikamuuliza hizi ndo mita 25 kwa 40?akadai ooh nili edit vipimo kumbe ni 17m kwa 25m nikwambia kwanini uedit tangazo kwani uliandika bila kupima?haya sasa ata hizo mita 17 kwa 25 hazipo yaani ni mita 10 kwa 17hv, halafu sio KIGOGO fresh ni DAMPO,then ni kama 2km toka road,sasa nashindwa kuelewa kwanini wanadanganya au wanafikiri mtu atalipa bila kwenda kupaona?au ndo anataka ela ya udalali?ETI ALINIDAI ELA YA KUJA SITE,NIKAMUULIZA MBONA KWENYE TANGAZO LAKO UKUSEMA KUHUSU ILO ANASEMA OOH MIMI NIMEACHA SHUGHULI ZANGU.akuambulia ata sh.100
 
Kiwanja kina meters 27*18
Nilienda na mteja weekend iliyopita na alipima mwenyewe na Fundi aliyekuja nae.
Kuhusu eneo lote: eneo linaitwa kigogo fresh na kituo ndio kinaitwa dampo.
acha uongo,yeyote atakayeenda site na mkapata hizo mita mimi nampa laki 2 niko tayari kwenda kuandikishiana kokote kule.
 
Kaka mimi nimeenda na huyu mpaka site,nilimpigia kwa namba hiyo hapo tukakutana,yeye Alisema kigogo Fresh,nilivyofika akanidirect kituo cha mbele panaitwa DAMPO tukakutana tukaenda site,ramani ya nyumba kweli ipo hivyo,umeme upo ila kwanza nguzo hiyo ya umeme iko kama mita 2 toka kwenye nyumba hivyo maana yake tayari kiwanja kimefinywa,pili upana ni mita 10 kwa 17 hv sasa nikamuuliza mita 25 ziko wapi akajing·ata tu,kuhusu eneo ni hilo hilo na mtu ni huyu huyu anachofanya hivi ni kujaribu kuukwepa ukweli,anasahau ukweli auna tabia ya kujificha,KAMA MWANA JF AKAENDA HIYO SITE AKAKUTA DIMENSION HIZO ANAZOZISEMA BASI KABLA AJAENDA TUANDIKISHIANE MIMI NITATOA LAKI MBILI.nafanya hivi ili kulinda heshima yangu ya kusema kweli na kuonesha namna gani huyu Dalali mbabaishaji,mbaya zaidi eti mwishon alitaka nimpe ela za kuona site,ajui kwamba mimi nilienda kuona sababu ya vipimo vilivyotajwa sasa nafikq nakuta tofaut.
 
Tang tumeenda,ni kama mwez hv umepita na sikupenda kusema haya ila ninavyoona anazidi kulirudia rudia hili tangazo lenye uwongo ndani yake nikapatwa na hasira na kuamua kuusema ukweli,kwan naamin siwez kupata dhambi kwa kusema ukweli,na haya nayoyasema MUNGU WANGU NI SHAHIDI.
 
acha uongo,yeyote atakayeenda site na mkapata hizo mita mimi nampa laki 2 niko tayari kwenda kuandikishiana kokote kule.
Pole sana mkuu!
Ulienda na jamaa yangu wa kutoka TABATA nadhan
Kiwanja/pagala kipo kwenye process zakulipiwa.
Aliyekua anahitaji alipelekwa na kuhakiki ukubwa wa kiwanja.
Nilipata mrejesho baada ya Jana kumpigia simu.
Mlienda wawili kama sikosei kwa Maelezo yake ni kwamba baada ya kufika mlikuwa mnakadiria kiwanja na si kwa vipimo I.e tape measure au roughly kwa hatua (miguu)
Aliyekwenda jumapili alitafuta na Fundi akaenda na muhusika na kuoneshwa mipaka yote.
Pole sana pengine haikua rizki yako
All in all kiwanja/PAGALA kinalipiwa mda wowote
 
mkuu ukienda site utapata mrejesho na naamini ata hiyo hutotoa.
Pole sana, naona umepatwa na jazba
Mungu akufanyie wepesi na akuondolee lilo ndani ya nafsi.
Kiwanja kinalipiwa 12m.
 
Watu wazima tumekuelewa, ila kuwa muaminifu hii itakusaidia uaminike wakati mwingine ukileta tangazo la biashara
 
We jamaa kumbe ni mpigaji MACHONDELA ahsante kwa kutujuza boss
 
Pole sana, naona umepatwa na jazba
Mungu akufanyie wepesi na akuondolee lilo ndani ya nafsi.
Kiwanja kinalipiwa 12m.
Kiufupi, kiwanja hakijanunuliwa ila umeamua kuchutama kwa style hiyo, sema nimekuwekea notification ya Dalali mbabaishaji ili siku nisije kuingia mkenge.....
Uaminifu na Ukweli ni nguzo ya mafanikio... Umejiharibia sana. Ukitaka kurudishia imani yako weka vithibitisho vyote kama hiyo biashara imefanyika kama unavyosema.
 
Ukweli utakuweka huru usiogope kusema kweli siku zote utawaokoa wengine. Madalali ukienda kichwa kichwa utalia
 
Ukweli utakuweka huru usiogope kusema kweli siku zote utawaokoa wengine. Madalali ukienda kichwa kichwa utalia
 
Aisee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…