Paka kunifatafata ni jambo la kawaida?

Unatia mabanzi yakizushi huku unamsemesha nakumuonesha kosa alilolifanya kama kadokoa finyango ama kakata gogo kwenye unga
Maana paka muda mwingine wanaujinga mwngi[emoji16]
Hapana bwana unatakiwa umfundishe angali mdogo, kwenye kujisaidia muwekee chombo kikubwa jaza mchanga muoneshe hapo ndio sehemu yake ya kujisaidia, kwenye chakula hakikisha humpi nyama au samaki wabichi, pika au kaanga ndio umpe ukimzoesha vitu vibichi ndio anakua mwizi, pia hakikisha vyombo vyake vina chakula na maji muda wowote akijisikia kula akute msosi,

Paka wangu hua namfanya mlinzi kama nikianika Samaki au Dagaa Kunguru wasile na anasimamia hiyo sekta kikamilifu hadokoi sababu anajua sio vyake.
 
Nyama nakula hasa Kuku ni my fav [emoji39][emoji1787]
Mume wangu ndio Veggie
Hahaha kumbe hii, kitu hata ukiwa mla nyama fresh tu. Mm nilijuaga ma veggie pekee ndo wanayo, mimi nilshauriwa niache kula nyama. Ila nilikaa mwaka tu, uzalendo ukanishinda nikawa nakula kwa hamu.
Vp khs mumeo anayo hiyo nguvu ya kuvutia wanyama Kama yy ni veggie?
 
Apande juu ya dresseing table yangu?aniachie manyoya yake?ATAJUA HAJUI
 
Naweza kuacha nyama ya Ng'ombe au Mbuzi ila sio Kuku na Samaki jamani hapo wataniswamehe,

Yeye ameanza uVegan ana miaka mi5 sasa anapenda pia Wanyama ana huruma sana imagine aweza kumuacha Mbu amng'ate hadi atosheke aondoke hataki kumfukuza ati anajitafutia chakula [emoji119] hapo ndio tunapogombana sasa,

Ameenda mbali zaidi hata vitu vya ngozi hatumii mfano viatu, mikanda, n.k ile pure leather kwake ni BIG NO

Yeye ni Dog Person na mie ni Cat Person
 
Apande juu ya dresseing table yangu?aniachie manyoya yake?ATAJUA HAJUI
Mbavu zangu, wallah umejua kunichekesha leo una sound kama ndugu yangu flani hivi yeye na Wanyama mbali mbali hasa Paka
 
Hiyo ya kuacha mbu amng'ate, kuna jamaa alikua na tabia hio, asee nlikua nacheka mno, anakuonesha kabisa mpk mbu anashiba anakwenda zake. Ila huko ni kupitiliza sasa. Huko ni kurisk afya lol 😂

Mwambie asiwe na mentality hio, itamkost baadae kuna vitu lazma uvichukulie kawaida maisha yasonge, atadata asipoangalia. Kuna kipindi nilibonga na mzungu flan yeye alikua anawaachia nzi, mende, na buibui na alikuwa ana wapatia chakula kabisa, just imagine eti kisa nao ni viumbe lol 😂, huko ni kupitiliza. Kwaiyo angekua nyoka au scorpion pia angemwacha?

Mimi pia ni Dog Person, na mpango wa kuagiza bulldogs.
 
Nimepoteza paka wanne ndani ya week 1, wameumwa hatujui nini mpk Leo...kutapika, kukosa appetite ht maji walikuwa hawawezi kunywa. Watatu wadogo wana km 2 months tu, na mmoja mkubwa kiasi alizaliwa mwaka jana. Kabaki mama yao tu na hivi km mwezi nilimfungisha uzazi. Yaani naandika hapa machozi yananitoka
 

Attachments

  • IMG-20240419-WA0063.jpg
    47.6 KB · Views: 1
Huyu ndio kafia hospital, tulijua atapona lkn haikuwa rizk 😭😭😭
 

Attachments

  • d870d1f0e7ed4bf7a563cba9e2eeeb2c.mp4
    2 MB
Mbavu zangu, wallah umejua kunichekesha leo una sound kama ndugu yangu flani hivi yeye na Wanyama mbali mbali hasa Paka
Dah, 🤣🤣🤣 Yaani Nikija kwako nikute paka juu ya kochi sijui kitanda unanikata stimu zooote.....
 
Utakua unanukia harufu ya thamaki.
 
Daah! Pole sana hawajawekewa sumu kweli au kula chemical yoyote? au ni Virus iliwavaa!?maana kama ni ugonjwa wa kawaida haiwezekani wafe kwa mkupuo hivyo

Siwezi kuyabeba maumivu yako Angel pole sana tena sana
 
Labda na ww ni Paka ila hujui
 
Dah, [emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yaani Nikija kwako nikute paka juu ya kochi sijui kitanda unanikata stimu zooote.....
Ana kochi lake tumeweka kitambaa kwa ajili ya manyoya na yeye kupata joto, mtu akikaa kwenye kochi lake atamsukuma na kulia kama ni mtoto na hakuna wakubwa around atamkwarua, yeye anaweza kuja kukaa sehemu zenu ila sio nyie mkakae kwake ni ugomvi [emoji23][emoji119]

Ukija kwangu kweli utakereeka na huyu Paka maana yeye ndio kama lastborn
 
Usinikumbushe siku tumemuona Tandu mie nshapanda dirishani napiga makelele kaja kamtoa na fagio sasa nitoke nimuone alivyombaruza ati nimemuacha aende huwezi jua pengine ana familia, nilichoooooka,

Si unaona hata hawa Rastafarians wana roho ya upendo uliopitiliza, nadhani sababu ya uVegan

Wait, Bulldog! hao sio wale Mbwa kila wakikua wanatengeneza ukichaa na anaweza kuattack nyumba nzima
 
Eeeeeehhhh 🙆🙆Nimekomaa Mimi! Tukibahatika kuwa marafiki urafiki wetu utaishia mtaani kwako hapana
 
Na umri huo unapanda dirishani? Tandu hatishi kivile, ila nimecheka eti huenda anafamilia. Vipi kama angedhuru mtu siku hiyo? Hv huwaga wanakua poisonous kweli hao? Maana sina experience kuona mtu kang'atwa na tandu.

Yah rastafarian wapo very emphatic na spiritual, kitu kilicho nishinda zaid ni kutunza manywele ila lifestyle yao na admire Sana. Kingine kilichonishinda ni ganja.

Bulldogs wanatisha kweli, na mwanzo kati ya specie nilizkuwa naziogopa ni hao, but with time am learning wapo very humble kwa care takers wao. Ni security guards wazuri sana. Hilo swala la ukichaa ni uzushi tu.
 

Sasa si bora Tandu, kuna huyu mdudu anaitwa Washa Washa naweza kukuamkia hata mara 100 ili mradi tu umtoe kwenye macho yangu, Tandu ananitisha kwanza miguu yake ilivyo mingi, uwezo wake wa kung'ata mbele na nyuma, hujakutana na litandu likubwa limekomaa hadi likitembea lina kishindo (nimetia chumvi kidogo [emoji1787]) wanasema ana sumu kali na anaweza kuua mtu,

Kwa Rastafarians sio lazima kufuga nywele kikubwa ni imani na kufata sheria zao hata Ganja sio wote wanatumia japo wanaamini ni mmea wa peponi, wana lifestyle nzuri sana ila siipendi kivile kwenye dunia yetu hii hutakiwi kua mnyonge sana utafanywa daraja na kila mtu, huruma iwepo na ukali uwepo,

Haya kila la kheir na BullDog, mimi hapana wananitisha kwa kweli.
 
Cats love height
Tafuta documentary inaitwa Inside the Mind Of a Cat ya 2022 utajifunza mambo mengi kuhusu paka. Kuna namna wanawasiliana na sisi iwe kwa ishara au kwa sauti lakini sisi tunapuuza tu kwavile hatujui ukicheki hiyo Documentary utajifunza vingi sana kuhusu paka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…