Paka kunifatafata ni jambo la kawaida?

Paka kunifatafata ni jambo la kawaida?

Wewe unadhani kwanini paka wawe wanafia kwako tu?

Paka wanaishi muda mrefu sana sasa nashangaa hajawahi kuishi na paka hata miaka mitanoe.
 
Wewe unadhani kwanini paka wawe wanafia kwako tu?

Paka wanaishi muda mrefu sana sasa nashangaa hajawahi kuishi na paka hata miaka mitanoe.

Hao waliokufa walikua wamefika umri mkubwa ukimtoa yule aliyewekewa sumu,

Paka wangu niliyemfuga mimi aliishi miaka 8, alikua dume, mama yake aliishi miaka 5.
 
Una malengo Gani na kuku mkuu?kama wanauwezo wa kujua ndio maana wakiniona nduki!kuku nikimuona tu nawaza kidali[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Nimecheka sana,
Basi kumbe kweli hao viumbe wana macho ya rohoni wanajua kabisa huyu ana lengo la kutufanya kitoweo
 
There's something about you, labda upo na high spiritual energy inayo attract hao viumbe, mimi pia kwa wanyama sio paka tu, hata kuku huwa wanapenda kuwa karibu nami. Najua wengi watacheka na kubisha ila kuna nishati isiyo onekana kwa macho ya nyama ila hao viumbe wanaweza kuisense haraka na kujua mawazo na malengo uliyonayo kumuhusu. So hata usishangae mummy! It's your energy.

Cha kufanya wewe endelea kuwa karibu nao, na kuoffer chakula kama kawaida.
Mimi nakuelewa na umenielezea kabisa, kupitia uzi huu ndio nilikuja kujitambua mimi ni nani kwenye ulimwengu wa kiroho kupitia wanyama hasa Paka.
 
Habari zenu waungwana wa humu ndani,

Nina jambo lanitatiza sana, kila nikiishi pahali lazima nifatwe na Paka, yaani atokee Paka aweke kambi kwangu, nikianzia kwetu kwa wazazi alikuja kipaka kidogo nikawa nampa chakula baadae kikaanza kuingia ndani, haikua rahisi kwa wazazi kumpokea lakini baadae wakampokea, basi tuliishi nae hadi alipofariki, baadae kakaja kengine kadogo nikakachukua pia, alikulia pale, akazaa, akafariki akaacha mtoto akakua pale mimi niliondoka baadae akaja kufariki,

Nilipohamia, ile nyumba nilikuta wapangaji wawili na mimi nikawa watatu, baada ya wiki kadhaa tangu nihamie wakaja paka watatu, wakaanza kuweka kambi eneo langu, wenzangu waliwafukuza lakini haikufua dafu, walishangaa kabla hawakuwahi kufatwa na hao Paka, nikaamua tu niwe nawapa chakula, mpaka siku moja asubuhi Paka mmoja alifariki mbele ya macho yangu nahisi aliwekewa sumu, nikahama hilo eneo kwa sababu zangu sio kwa ajili ya Paka,

Nilipohamia napo akaja kipaka kidogo kikaanza mazoea na mimi, Mbwa walikua wanamsumbua nikawa namsaidia wasimguse na kumpa chakula pia, sikukaa sana eneo hilo nikahama kutoka wilaya moja kwenda nyingine,

Nyumba niliyohamia, mwenye nyumba aliishi eneo hilo pia,alikua anafuga Paka, baada ya muda kidogo yule Paka akaanza kuja kwangu, akawa kwao haendi kabisaa anashinda na kulala kwenye baraza yangu, mwenye nyumba akahuzunika kama vile nimemteka Paka wake lakini haikuwezekana kumtoa , alipata Mimba akajifungua akaacha watoto kwao akawa anashinda kwangu tu, hadi nilipohama eneo hilo,

Nilipohamia napo nikakuta mpangaji mmoja ana Paka wake mzuri Maa shaa Allah, heeeh akaanza kuja kwangu, nikimpa chakula anakula lakini cha kwao hali, sikukaa sana hapo nikahama.

Hapa nilipohamia sasa hivi mmh, mwezi mmoja umepita kwa amani, sasa nikashangaa siku moja asubuhi naamshwa na sauti za Paka, nafungua mlango asalaleee nakuta vipaka vitatu vimejitandaza barazani kwangu havina habari, nikatoka wawili wakakimbia mmoja akabaki, sasa imekua utaratibu wao wapita nyumba zoote wanakuja kwangu kuweka kambi hawa nimesema siwapi chakula tuone kama wataishi,

Lakini nimejiuliza sana, kwanini Paka wananipenda na kunifata? Kuna nini nyuma ya pazia? Na hii sio tu kwa nyumba nilizoishi hata nyumba yoyote yenye Paka nikifika tu lazima anizoee au hata njiani nikikutana na Paka hawezi nikimbia atasimama na ku meow,

Nini hii jamani?

View attachment 1510235
Shindwa pepo, Holy Ghost Fire, 🔥
 
Nimecheka sana,
Basi kumbe kweli hao viumbe wana macho ya rohoni wanajua kabisa huyu ana lengo la kutufanya kitoweo
Ndio Wana macho ya rohoni,Kuna mmbwa nilimuona nyumba Fulani Kwa watu,huyo mmbwa anabwekea hewa yaani kama Kuna kitu anakibwekea mi sioni Mtu aaaghhr ndio alizidi kunichanganya😅😅
 
Una malengo Gani na kuku mkuu?kama wanauwezo wa kujua ndio maana wakiniona nduki!kuku nikimuona tu nawaza kidali😁😁😁😁
🤣🤣🤣 basi una nuksi! Kiumbe yeyote anauwezo wa ku sense hatari kabla haijamkumba.
 
Bibi yangu mmoja alikua na mipaka miwili.
Mmoja mama mtu hakuwa na shida tutakaa tutapiga story yaani ile mnakumbatiana analala.
E bwana alikua na toto tundu lake.
Ukitaka kula gegedo linafungua mlango linajilaza kati.
Nikiwa naangalia tv linakuja linazima,mara linata msosi mara ulipeleke chooni.
Tukawa tunafukuzana na kimbizana kila muda.
X alisema paka huyo alipata cancer wakaenda kumtema.
Ila mama mtu yupo mpoole.
 
Mnyama anayenitazama machoni muda wote bila kupepesa macho ziwezi kukaa naye karibu muda mrefu, itabidi aende tu sina imani naye.
Mkuu hivyo anavyokutizama usoni kuna kitu anakisoma kwako tabia hii as kwa paka tuu hata mbwa pia anayo 😁
 
We
Kwa Hizo comment zenu za roho nzuri,nimekubali Mimi ni certified roho mbaya.....Sio tu kuwapenda sipendi hata kuwaona hao wadudu ....wanyama waroho utasema Nini sijui wanakuangalia machoni ukiinua kipaja Hadi unavyotafuna Hadi unavyomeza ndio Nini sasa,!
Ndio mroho pia mchoyo

Ukitaka paka asikusumbue unapotaka kula hakikisha na yeye unamuweka pembeni kwa chombo chake ,sio we unakula unakuja kumpa makombo sio sawa
 
Back
Top Bottom