Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe unadhani kwanini paka wawe wanafia kwako tu?
Paka wanaishi muda mrefu sana sasa nashangaa hajawahi kuishi na paka hata miaka mitanoe.
Bila shaka unakimbizwa na Bata dume, nasikia hua wana wivu sana na wake zao [emoji23]Mimi Nina unafiki na Bata, aki niona lazima ani kimbize.
Sasa huwa napigana nae [emoji23][emoji23]
Nimecheka sana,Una malengo Gani na kuku mkuu?kama wanauwezo wa kujua ndio maana wakiniona nduki!kuku nikimuona tu nawaza kidali[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Mimi nakuelewa na umenielezea kabisa, kupitia uzi huu ndio nilikuja kujitambua mimi ni nani kwenye ulimwengu wa kiroho kupitia wanyama hasa Paka.There's something about you, labda upo na high spiritual energy inayo attract hao viumbe, mimi pia kwa wanyama sio paka tu, hata kuku huwa wanapenda kuwa karibu nami. Najua wengi watacheka na kubisha ila kuna nishati isiyo onekana kwa macho ya nyama ila hao viumbe wanaweza kuisense haraka na kujua mawazo na malengo uliyonayo kumuhusu. So hata usishangae mummy! It's your energy.
Cha kufanya wewe endelea kuwa karibu nao, na kuoffer chakula kama kawaida.
Shindwa pepo, Holy Ghost Fire, 🔥Habari zenu waungwana wa humu ndani,
Nina jambo lanitatiza sana, kila nikiishi pahali lazima nifatwe na Paka, yaani atokee Paka aweke kambi kwangu, nikianzia kwetu kwa wazazi alikuja kipaka kidogo nikawa nampa chakula baadae kikaanza kuingia ndani, haikua rahisi kwa wazazi kumpokea lakini baadae wakampokea, basi tuliishi nae hadi alipofariki, baadae kakaja kengine kadogo nikakachukua pia, alikulia pale, akazaa, akafariki akaacha mtoto akakua pale mimi niliondoka baadae akaja kufariki,
Nilipohamia, ile nyumba nilikuta wapangaji wawili na mimi nikawa watatu, baada ya wiki kadhaa tangu nihamie wakaja paka watatu, wakaanza kuweka kambi eneo langu, wenzangu waliwafukuza lakini haikufua dafu, walishangaa kabla hawakuwahi kufatwa na hao Paka, nikaamua tu niwe nawapa chakula, mpaka siku moja asubuhi Paka mmoja alifariki mbele ya macho yangu nahisi aliwekewa sumu, nikahama hilo eneo kwa sababu zangu sio kwa ajili ya Paka,
Nilipohamia napo akaja kipaka kidogo kikaanza mazoea na mimi, Mbwa walikua wanamsumbua nikawa namsaidia wasimguse na kumpa chakula pia, sikukaa sana eneo hilo nikahama kutoka wilaya moja kwenda nyingine,
Nyumba niliyohamia, mwenye nyumba aliishi eneo hilo pia,alikua anafuga Paka, baada ya muda kidogo yule Paka akaanza kuja kwangu, akawa kwao haendi kabisaa anashinda na kulala kwenye baraza yangu, mwenye nyumba akahuzunika kama vile nimemteka Paka wake lakini haikuwezekana kumtoa , alipata Mimba akajifungua akaacha watoto kwao akawa anashinda kwangu tu, hadi nilipohama eneo hilo,
Nilipohamia napo nikakuta mpangaji mmoja ana Paka wake mzuri Maa shaa Allah, heeeh akaanza kuja kwangu, nikimpa chakula anakula lakini cha kwao hali, sikukaa sana hapo nikahama.
Hapa nilipohamia sasa hivi mmh, mwezi mmoja umepita kwa amani, sasa nikashangaa siku moja asubuhi naamshwa na sauti za Paka, nafungua mlango asalaleee nakuta vipaka vitatu vimejitandaza barazani kwangu havina habari, nikatoka wawili wakakimbia mmoja akabaki, sasa imekua utaratibu wao wapita nyumba zoote wanakuja kwangu kuweka kambi hawa nimesema siwapi chakula tuone kama wataishi,
Lakini nimejiuliza sana, kwanini Paka wananipenda na kunifata? Kuna nini nyuma ya pazia? Na hii sio tu kwa nyumba nilizoishi hata nyumba yoyote yenye Paka nikifika tu lazima anizoee au hata njiani nikikutana na Paka hawezi nikimbia atasimama na ku meow,
Nini hii jamani?
View attachment 1510235
Ndio Wana macho ya rohoni,Kuna mmbwa nilimuona nyumba Fulani Kwa watu,huyo mmbwa anabwekea hewa yaani kama Kuna kitu anakibwekea mi sioni Mtu aaaghhr ndio alizidi kunichanganya😅😅Nimecheka sana,
Basi kumbe kweli hao viumbe wana macho ya rohoni wanajua kabisa huyu ana lengo la kutufanya kitoweo
😅🙆True cats love fish. Especially salt fish
🤣🤣🤣Huo sio urafiki ni uaduiMimi Nina unafiki na Bata, aki niona lazima ani kimbize.
Sasa huwa napigana nae 😂😂
Yule mjinga ana jua kuni dhalilisha, unaeza kuta napita kwa wema tu.Bila shaka unakimbizwa na Bata dume, nasikia hua wana wivu sana na wake zao [emoji23]
Mwanangu wa faida huyo, Niki taka kusababisha vita naku chonganisha nae😂🤣🤣🤣🤣🤣Huo sio urafiki ni uadui
🤣🤣🤣 basi una nuksi! Kiumbe yeyote anauwezo wa ku sense hatari kabla haijamkumba.Una malengo Gani na kuku mkuu?kama wanauwezo wa kujua ndio maana wakiniona nduki!kuku nikimuona tu nawaza kidali😁😁😁😁
Sawa, je unakula nyama? Au ww ni vegetarian!?Mimi nakuelewa na umenielezea kabisa, kupitia uzi huu ndio nilikuja kujitambua mimi ni nani kwenye ulimwengu wa kiroho kupitia wanyama hasa Paka.
Mkuu hivyo anavyokutizama usoni kuna kitu anakisoma kwako tabia hii as kwa paka tuu hata mbwa pia anayo 😁Mnyama anayenitazama machoni muda wote bila kupepesa macho ziwezi kukaa naye karibu muda mrefu, itabidi aende tu sina imani naye.
Unasema?[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] khaaaaaah yaaaan weee sijui unawza nn? Tena paka ni hatareeeeh kweny mapenzi, maan style zote za kibinadamu wanajua na kupract, so burudaaaaaan tyuuuh.
Pia kumbuka Paka wote mikono utumia MashotoHakika mkuu, ila mi nawapenda maana they are so cute...
Ukiwa free mnacheza wee, na ukimtizama usoni unaona kabisa anafurahia.😂
Akiwa amepumzika zake uanze kumsumbua utaona anamind, anakuwa anakutishia na vimikono vyake..😂
Ndio mroho pia mchoyoKwa Hizo comment zenu za roho nzuri,nimekubali Mimi ni certified roho mbaya.....Sio tu kuwapenda sipendi hata kuwaona hao wadudu ....wanyama waroho utasema Nini sijui wanakuangalia machoni ukiinua kipaja Hadi unavyotafuna Hadi unavyomeza ndio Nini sasa,!