Paka kunifatafata ni jambo la kawaida?

Paka kunifatafata ni jambo la kawaida?

Paka wana dizain moja ya kumjua mtu mwema. Wanasema ukiona paka anamuogopa mtu ujue huyo mtu ni hatari,anaweza akawa mchawi au vyovyote. Kwa hiyo paka kukufuata sio kesi ni hali ya hali yako ya wema tu
Shukrani kwa kunifumbua macho, kwa hakika nakubaliana na wewe.
 
Habari zenu waungwana wa humu ndani,

Nina jambo lanitatiza sana, kila nikiishi pahali lazima nifatwe na Paka, yaani atokee Paka aweke kambi kwangu, nikianzia kwetu kwa wazazi alikuja kipaka kidogo nikawa nampa chakula baadae kikaanza kuingia ndani, haikua rahisi kwa wazazi kumpokea lakini baadae wakampokea, basi tuliishi nae hadi alipofariki, baadae kakaja kengine kadogo nikakachukua pia, alikulia pale, akazaa, akafariki akaacha mtoto akakua pale mimi niliondoka baadae akaja kufariki,

Nilipohamia, ile nyumba nilikuta wapangaji wawili na mimi nikawa watatu, baada ya wiki kadhaa tangu nihamie wakaja paka watatu, wakaanza kuweka kambi eneo langu, wenzangu waliwafukuza lakini haikufua dafu, walishangaa kabla hawakuwahi kufatwa na hao Paka, nikaamua tu niwe nawapa chakula, mpaka siku moja asubuhi Paka mmoja alifariki mbele ya macho yangu nahisi aliwekewa sumu, nikahama hilo eneo kwa sababu zangu sio kwa ajili ya Paka,

Nilipohamia napo akaja kipaka kidogo kikaanza mazoea na mimi, Mbwa walikua wanamsumbua nikawa namsaidia wasimguse na kumpa chakula pia, sikukaa sana eneo hilo nikahama kutoka wilaya moja kwenda nyingine,

Nyumba niliyohamia, mwenye nyumba aliishi eneo hilo pia,alikua anafuga Paka, baada ya muda kidogo yule Paka akaanza kuja kwangu, akawa kwao haendi kabisaa anashinda na kulala kwenye baraza yangu, mwenye nyumba akahuzunika kama vile nimemteka Paka wake lakini haikuwezekana kumtoa , alipata Mimba akajifungua akaacha watoto kwao akawa anashinda kwangu tu, hadi nilipohama eneo hilo,

Nilipohamia napo nikakuta mpangaji mmoja ana Paka wake mzuri Maa shaa Allah, heeeh akaanza kuja kwangu, nikimpa chakula anakula lakini cha kwao hali, sikukaa sana hapo nikahama.

Hapa nilipohamia sasa hivi mmh, mwezi mmoja umepita kwa amani, sasa nikashangaa siku moja asubuhi naamshwa na sauti za Paka, nafungua mlango asalaleee nakuta vipaka vitatu vimejitandaza barazani kwangu havina habari, nikatoka wawili wakakimbia mmoja akabaki, sasa imekua utaratibu wao wapita nyumba zoote wanakuja kwangu kuweka kambi hawa nimesema siwapi chakula tuone kama wataishi,

Lakini nimejiuliza sana, kwanini Paka wananipenda na kunifata? Kuna nini nyuma ya pazia? Na hii sio tu kwa nyumba nilizoishi hata nyumba yoyote yenye Paka nikifika tu lazima anizoee au hata njiani nikikutana na Paka hawezi nikimbia atasimama na ku meow,

Nini hii jamani?

View attachment 1510235
Aisee
 
Wewe upo kama mimi kabisa hata nikienda Bar ambayo ina paka tunaweza kuwa wengi ila bado akaja upande wangu na Lazima tu nimpe msosi, home kuna paka huyo ananipenda sana hata niwe nje ya home kwa miezi nikirudi hanisahau na lazima aje alale chumba ninacholala
 
Dream Queen bado Paka wanakupenda?[emoji1][emoji1][emoji1]
Juzii tu hapa nilienda kutembea kwa watu nashangaa Paka ananifata hadi miguuni wenyeji wanasema hao Paka hawana makazi walizaliwa wanazagaa zagaa na hawajawahi kusogelea nyumba yao zaidi ya kukatiza tena kwa mbio ndefu,
Basi nilivyopewa historia hiyo nikamnyanyua hakubisha, nikamuweka mapajani kumuangalia vizuri jamani kana mimbaaaa, yaan kaPaka kadogo wamekajaza Mimba kumbe mifedhuli sio binaadam tu hadi wanyama! [emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo paka kama ni wa akiume basi tambua ni boyfriend wako uliyemdamp zamani na wingi wa paka husika basi ujue ni wingi wa wanaume uliokuwa umewatosa...kuna paka mmoja nimeuona tazama yake ni kama ya mshkaji wangu mmoja aliyetoswa na demu wake ambaye hadi leo hajaamua kutangaza nia nyingine.
Imebidi nicheke kama chiz..
 
Yaan kwanilivyo mpenda paka nisingewaza hata, maana paka humfuata mtu mwenye upendo na karoho flan kazuri, mm nilikuwa nafuga paka nyumban tena wawili wakizaa hapo ni balaa tupu na walikuwa na lishe safi niliwagawa huko mtaa wa tatu lakn walirudi
 
Lol, hao Paka wanatafuta nyumba ya kuishi, wamekuletea huyo Panya kusudi uwakaribishe wao wanaona wamekuletea zawadi sababu kwao ni chakula chao pendwa,

Ukijua tabia za Paka raha sana, tena hata unayemfuga nyumbani kuna siku anaweza kuja na mzoga wa ndege huko akakuwekea kwenye sahani yako ya chakula, yeye anajiona shujaa amekuwindia,
Napenda sana Paka.
Tena wamemuheshimu kweli yani paka panya kwao ni kama chair fire kuleta kitu kipo mang'alu untouched ni jambo linalohitaji uvumilivu kweli

Mm nnachowapendea paka hawapangiwi maisha ...
 
Back
Top Bottom