Pekejeng
JF-Expert Member
- Jul 5, 2016
- 808
- 2,155
Pole kuna kipindi kidogo nitoe chozi, Miaka hiyo nyumbani tulikuwa tunafuga paka, Yule paka alikuja kushika mimba na kuzaa kwenye stoo flani hivi ya nyumbani, Bi mkubwa alimaindi kuzalia kwenye stoo yake akanipa kazi ya kuvitoa vile vitoto na kuviamisha kwenye banda flani hivi la pembeni, Mda huo mama paka alilkuwa ametoka mimi nikaviamishia kwenye hilo banda ambalo bi mkubwa alinielekeza kuviweka.Huyu ndio kafia hospital, tulijua atapona lkn haikuwa rizk ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜
Yule mama paka kurudi anaona vitoto vyake stoo havipo akaanza kulia na vile vipaka kule kwenye banda vinalia ila cha ajabu badala ya kwenda kule kuvifata yeye anan'gan'gana kuzunguka tu maeneo ya stoo kuvitafuta ikabidi nitoke na kumbeba kumpeleka kwenye banda ambalo ndo vitoto vyake vilipo cha ajabu ukimuweka anatoka mbio havitaki utasema sio vitoto vyake, Nikawa nashangaa nikasema ngoja nimuache kwa vile nimeshamuonyesha vilipo vitoto vyake basi atakuja kuvifata mwenyewe akitaka kumbe hamna ilipita siku ya kwanza, ya pili, wala havisogelei kabisa aisee kadri siku zinavyosogea na vitoto ndo vinazidi kupiga kelele sababu ya njaa mara viaende huku mara kule na vile vilikuwa hata macho havijaanza kufumbua utavionea huruma