Pre GE2025 Pakifanyika Reforms kwenye Katiba kupata Tume huru ya Uchaguzi, Watanzania wanaweza kuiamini na kuipigia kura CCM, tuondoe hofu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
unafikiri kwanini wanakwama? kama inafaida kwao?
 
Tayari bunge lilishapitisha kuwa tume iliyopo iitwe tume huru ya uchaguzi. Sasa ni tume gani tena mnataka?
 
CCM Ina njia nyingi za kushinda uchaguzi hata ikiwepo hiyo Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya,

Bado Wana machinery za kushinda vita ya Uchaguzi.

CCM inaweza kubadilika na kupokea mabadiliko haya na kuendelea kusalia mamlakani Kwa HAKI.

..CCM inapokea BILLIONI 3.2 kila mwezi kama ruzuku toka kwa msajili wa vyama.

..uwezo huo wa kifedha unapaswa kukifanya chama hicho kijiamini kwamba kinaweza kushinda uchaguzi hata kama utasimamiwa na Tume Huru.
 
Chaguzi zote toka 2010 hazitoai matokea yanayowafanya wakubali tume huru. Ingekuwa kweli wanapata kura wanazotangazwa nazo, wangekubali hiyo tume huru.
 
Ukweli mchungu ni kuwa katika mazingira ya uchaguzi huru CCM ya sasa haiwezi kuishinda hata ACT Wazalendo.
 
Ndio Hasa msingi wa HOJA,

Pesa wanazo,

Ofisi zipo Nchi nzima ,zile walizorithi Toka mfumo wa chama kimoja,

Vitega Uchumi wanavyo,

Wasichokuwa nacho ni kujiamini tu kuwa wanaweza kushinda bila Hila za kuiba kura Kwa kupitia Tume huru ya Uchaguzi.
 
Tayari bunge lilishapitisha kuwa tume iliyopo iitwe tume huru ya uchaguzi. Sasa ni tume gani tena mnataka?
Iitwe sio, Yaani Tume Ile Ile ipewe Jina jipya!,

Uliishia la ngapi ndugu!!
 
Chaguzi zote toka 2010 hazitoai matokea yanayowafanya wakubali tume huru. Ingekuwa kweli wanapata kura wanazotangazwa nazo, wangekubali hiyo tume huru.
Kwa mtaji walionao,

Wanaweza kushinda hata pakiwepo Tume huru ya Uchaguzi,

HOFU na kukumbatia RUSHWA ndio Hasa tatizo,
 
Ukweli mchungu ni kuwa katika mazingira ya uchaguzi huru CCM ya sasa haiwezi kuishinda hata ACT Wazalendo.
Kijijini kwetu hicho chama hakuna anayekijua,

Sasa uichagueje ACT isiyojulikana ,isiyo na uwezo kuisimamisha mgombea, isiyo na ofisi?

CCM waache HOFU, wakubali ujio wa Tume huru ya Uchaguzi, wanashinda asubuhi na mapema.
 
CCM siyo kama inahofu ya kushindwa kwa Hivi sasa hakuna chama Chochote ambacho kina mtandao kama CCM. Pia ambacho kimejipanga vizuri kila Idara, Tatizo la CCM kutotaka reform ni hizi
1.Wanataka kuzoa viti vyote kwenye chaguzi zote
2.Wanataka kulazimisha kupitisha watu ambao sehemu nyingine hawakubaliki
3.Chama kimekuwa kama Abiria wa Mbagala hata kama wapo watatu lazima wafanye vurugu kuingia kwenye Basi.
Kwa hiyo kwa misingi hiyo mitatu Abadani CCM haitakuwa tayari kwa Reform yoyote iwe ya katiba au yatume huru. Kwasababu swala la Haki kwao Halipo. Viongozi hivi sasa wanaandaa watoto wao na jamaa zao kushika madaraka hata kama hawawezi unadhani kuna mtu atakubali reform yoyoote. Watanzania wasipo Shtuka watakuja kukuta kila kitu kwenye nchi kimeshikwa na wageni kwani wao ndio wanafanikisha hizo ajenda za CCM. Wabunge wetu wote wamekuwa si wazalendo, Hata huyo Mpini wa jembe anayepiga kelele ni kwa sababu tu amewekwa nje ya ulaji lakini angepatiwa kanafasi kakula wala usinge msikia, Lakini afadhali hata yeye kidogo.
 
HOJA nzito hizi,

Kumbe wakiacha Ujinga wa kukumbatia RUSHWA wakatenda HAKI, wakarugusu mchakato wa HAKI ndani ya chama Chao kupata wagombea wanaokubalika,

Bado CCM inaweza kushinda vita ya Uchaguzi hata pakiwepo Tume huru ya Uchaguzi.
 
Kwa mtaji walionao,

Wanaweza kushinda hata pakiwepo Tume huru ya Uchaguzi,

HOFU na kukumbatia RUSHWA ndio Hasa tatizo,
Huo mtaji upo kipropaganda zaidi, na kukiwa na uchaguzi huru hawawezi kupata 2/3 bungeni ambayo itawawezesha kupitisha chochote watakavyo. Na ndani ya chaguzi 2 hawatafikisha hata hiyo 2/3.
 
2010 na 2015 Mbowe na Lissu walipita na kushinda uchaguzi kupitia tume na katiba ipi?
 
Wasira amesema wananchi hawataki hayo mabadiliko wanataka chakula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…