Pre GE2025 Pakifanyika Reforms kwenye Katiba kupata Tume huru ya Uchaguzi, Watanzania wanaweza kuiamini na kuipigia kura CCM, tuondoe hofu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna ukakasi hapa, kwa nini CCM hawataki hii reform? Kuanzia Tume ya Jaji Nyalali, Kisanga hata hii ya Jaji Warioba - report zipo wazi kabisa kwa nini CCM hawataki? Kuna biashara gani kati ya Tanganyika na CCM.

Lissu tuongoze katika mpambano hawa jamaa yaonekana bila shuruti hawaendi.

Masuala ya kupangishana foleni jua kali kupiga kura zisizo na maana sasa imefika mwisho.
 
Ni fear of unknown!

Kwa uwekezaji, raslimali pesa na viongozi, miundombinu,

Hawawezi shindwa uchaguzi kirahisi.

CCM ikubali Tume huru ya Uchaguzi Ili ishinde tena Kwa kishindo.
 
Katiba Mpya ndio inaleta Ugali? Tuendelee hivi hivi
 
Sina tatizo na kushindwa kihalali boss. Tatizo ni kuwa watu hawako tayari kujitokeza kugombea kwa kuhatarisha maisha yao, ama kuhujumiwa shughuli zao za kuwaingizia vipato. Kwahiyo huo uduni unachangiwa na hujuma zaidi.
 
Pamoja na kupata Tume huru ya Uchaguzi, upinzani ukishindwa kupata wagombea imara,ikishindwa kujenga ofisi Hadi mashinani nk,nk, wasahau kukishinda CCM.
Mabadiliko ni taratibu. Unajua vitisho pia vinawarudisha nyuma raia. Lakini kukiwa na uwanja huru na elimu ya uraia ikatolewa wananchi wanabadilika. Sheria ikiruhusu hadi wagombea binafsi mbona wagombea watajitokeza kama kukiwa hakuna kutishana
 
2020 hata bila kuvuruga uchaguzi CCM ingeshinda ila Magufuli nia yake ilikuwa kufuta upinzani Tanzania na kuirudisha nchi kwenye mfumo wa chama kimoja na hayo yalikuwa maandalizi ya yeye kuwa Rias wa milele chini ya mfumo wa Chama kimoja. Yule kiumbe alikuwa na ushetani mwingi sana.
 
Alikuwa sawa,

Kama chama kilichoaminiwa na watz kuwa Cha upinzani,

Kumbe ni wafanyabiashara kupitia siasa.

Hapo hakuna ushetani,

The man alinyooka kama rula,

Abarikiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…