Pre GE2025 Pakifanyika Reforms kwenye Katiba kupata Tume huru ya Uchaguzi, Watanzania wanaweza kuiamini na kuipigia kura CCM, tuondoe hofu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watachaguliwa na nani au watachaguliwaje? Dogo mbona swali jepesi hili?
Tume huru maana yake viongozi wa juu wanasailiwa na kupitishwa na jopo. Hiyo tume huru kwa mfano inakuwa na viongozi kutoka makundi mbalimbali mfano viongozi wa dini nk.

Ikifika zoezi la uchaguzi, hiyo tume huru inafanya mchakato yenyewe kuwapata wasimamizi wa uchaguzi kutoka mtaank ambao si waajiriwa wa serikali (yaani kazi ya muda). Sasa hawa wasimamizi kutoka mtaani wanaweza kuwa na faida kwa sababu hakuna wa kuwatishia kwamba nitakufukuzisha kazi kama haumtangazi fulani kama ilivyo kwa Wakurugenzi na walimu kutishiwa!

Kibongo bongo tume huru inaweza kusaidia kupatikana madiwani na wabunge wengi wa upinzani mana matokeo yake yanajumlishwa ngazi ya kata na jimbo, hivyo zile amri za kumtangaza fulani hazitakuwepo kwa sababu msimamizi siyo mwajiriwa wa serikali hivyo hatakuwa na cha kupoteza, itabaki ujanja ujanja mdogo wa kuibiana tu kura ndani ya vituo.

Kimbembe kitabaki ngazi ya urais hapo ndio kunakuweza kupindishwa matokeo hata kwa makusudi ili kuzua la kuzua na kuingia katika meza ya mazungumzo.

Pata picha, nini kitatokea ikiwa tume huru ya uchaguzi inatangaza ajira za muda za wasimamizi halafu waombaji ni graduates ambao hawana ajira wapo mtaani na hakuna wa kuwaamrisha kama ilivyo kwa walimu.
 
Mpka sasa ccm haijiamini ktk chaguzi zoote ndio maana unaona mapicha picha mengi sanaaaa,

Hakuna kiongozi wa chama cha upinzani ambacho kipo hai zai ya miaka 15 hajapitia misuko suko ya kipolic ikiwepo kupigwa kuzuiwa kufanya mikutano kuwekwa mahabusu kwa makoso yasio julikana nk, hii inaonyesha kwamba wao hawapo bora kama wangekuwa wanajiamni wasingefanya haya,

Uchaguzi kuanzia selikali za mitaa ni vigisu kubwa sana sasa kama wangekuwa na sera nzuli utawala bora wasifanya haya kuna mengi yapo nyuma ya pazia ukiwa ndani ya chama chochote ndio utayajua haya
 
Hellow Tanzania.

Nani anaingiza HOFU ndani ya chama Cha MAPINDUZI kuwa, pakifanyika Reforms kwenye Katiba tukapata Tume huru ya Uchaguzi, kwamba CCM itaanguka na kushindwa vita ya Uchaguzi mkuu?

CCM Ina mtajj mkubwa wa wanachama Nchi nzima, na wamefanikiwa kumtangaza Mwenyekiti wa chama kwenye mabango na picha kwenye bodaboda zilizotapakaa Nchi nzima,

CCM Ina ofisi Nchi nzima Hadi mashinani huko,

CCM Ina vitegauchumi na inapokea ruzuku ya kutosha Kila mwezi, Bilioni zaidi ya 3. Mtaji wa viongozi waliopikwa ,wasomi inayo.nk nk

Mabalozi wa nyumba kumi kumi Nchi nzima ni CCM, sasa HOFU ya kushindwa vita ya Uchaguzi inatoka wapi?

Mzee Kikwete aliruhusu Mchakato wa Katiba mpya kuanza Ili kuwahakikishia WAPINZANI kuwa CCM inaweza kushinda uchaguzi Kwa namna yoyote.

Ushauri: CCM itoke mbele na kukubali Reforms kwenye Katiba Ili Tume huru ya Uchaguzi ipatikane Ili CCM ishinde Kwa kishindo na WAPINZANI wakiongozwa na TUNDU Lissu, wakose pa kuficha sura zao Kwa Aibu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Lucas aje aone sababu Gani Ccm haitaki tume huru ya uchaguzi, na inaamini kwamba imetumia njia zisizo halali kuingia madarakani na hivyo unaona inatumia gharama kubwa kushawishi kukubalika, wanatumia Kila jambo linalokutanisha watu kumtaja Mama Yao na hata sehemu zisizostahili kulazimisha umma kumkubali! Fedha zinazopotelea humu matumizi yake ni hayo sasa pamoja na Kununua magoli.
 
Attachments

  • 1739690982557_1.jpg
    1739690982557_1.jpg
    249.6 KB · Views: 1
Huo mtaji upo kipropaganda zaidi, na kukiwa na uchaguzi huru hawawezi kupata 2/3 bungeni ambayo itawawezesha kupitisha chochote watakavyo. Na ndani ya chaguzi 2 hawatafikisha hata hiyo 2/3.
Tuseme Kweli,

TUNDU Lissu amekiri uchaguzi wa mitaa uliopita kuwa, CHADEMA haikuwa imewaandaa wagombea wenye uwezo Kupambana katika vita ya Uchaguzi,

So, mbali na hujumanna wizi, capacity ya wagombea wa CHADEMA mara nyingi ni duni.

Vivyo hata baada ya kupatikana Tume huru ya Uchaguzi, CHADEMA ikiendelea kuweka wagombea duni, itaendelea kushindwa na CCM.
 
Hakuna wa kushinda Urais wa Nchi Hii nje ya Mgombea wa CCM. Ni CCM pekee yenye hati miliki ya kushikilia na kukalia kiti cha Urais.
Hiyo hatia milki ya CCM kushikilia na kukalia KITI Cha Urais anaitoa bibi Yako?
 
Tume huru maana yake viongozi wa juu wanasailiwa na kupitishwa na jopo. Hiyo tume huru kwa mfano inakuwa na viongozi kutoka makundi mbalimbali mfano viongozi wa dini nk.

Ikifika zoezi la uchaguzi, hiyo tume huru inafanya mchakato yenyewe kuwapata wasimamizi wa uchaguzi kutoka mtaank ambao si waajiriwa wa serikali (yaani kazi ya muda). Sasa hawa wasimamizi kutoka mtaani wanaweza kuwa na faida kwa sababu hakuna wa kuwatishia kwamba nitakufukuzisha kazi kama haumtangazi fulani kama ilivyo kwa Wakurugenzi na walimu kutishiwa!

Kibongo bongo tume huru inaweza kusaidia kupatikana madiwani na wabunge wengi wa upinzani mana matokeo yake yanajumlishwa ngazi ya kata na jimbo, hivyo zile amri za kumtangaza fulani hazitakuwepo kwa sababu msimamizi siyo mwajiriwa wa serikali hivyo hatakuwa na cha kupoteza, itabaki ujanja ujanja mdogo wa kuibiana tu kura ndani ya vituo.

Kimbembe kitabaki ngazi ya urais hapo ndio kunakuweza kupindishwa matokeo hata kwa makusudi ili kuzua la kuzua na kuingia katika meza ya mazungumzo.

Pata picha, nini kitatokea ikiwa tume huru ya uchaguzi inatangaza ajira za muda za wasimamizi halafu waombaji ni graduates ambao hawana ajira wapo mtaani na hakuna wa kuwaamrisha kama ilivyo kwa walimu.
Pamoja na kupata Tume huru ya Uchaguzi, upinzani ukishindwa kupata wagombea imara,ikishindwa kujenga ofisi Hadi mashinani nk,nk, wasahau kukishinda CCM.
 
Naona umepaniki tayari kama ilivyo kawaida kwa asiye na akili.
Nimemuuliza hiyo hatia milki anatoa bibi Yako Hadi useme usemavyo?

Mamlaka ya kuongoza Nchi hutoka Kwa wananchi, sasa wapiga kura wakiikataa CCM Kwa sababu mbalimbali, hatia milki hiyo haitakuwepo.
 
Hapo wanacheka tu na kuambiana " Mnauona mtego huu? 😄 🤣
Yaani vyoo vya misaada, madawati hakuna mashuleni, dawa hospital hakuna mpaka kiongozi anawachamba wajawazito lakini hajui alizaliwa kwenye hali gani?
Jamani kukubali hili linatakata ufanywe zezeta labda
 
Mtego upo kwenye kuachana na RUSHWA na wizi wa kura na kuifisadi Nchi,

Lakini HOFU ya kushindwa uchaguzi Kwa ujio wa Tume huru ya Uchaguzi ni HOFU ya kutengeneza tu,
 
Hellow Tanzania.

Nani anaingiza HOFU ndani ya chama Cha MAPINDUZI kuwa, pakifanyika Reforms kwenye Katiba tukapata Tume huru ya Uchaguzi, kwamba CCM itaanguka na kushindwa vita ya Uchaguzi mkuu?

CCM Ina mtajj mkubwa wa wanachama Nchi nzima, na wamefanikiwa kumtangaza Mwenyekiti wa chama kwenye mabango na picha kwenye bodaboda zilizotapakaa Nchi nzima,

CCM Ina ofisi Nchi nzima Hadi mashinani huko,

CCM Ina vitegauchumi na inapokea ruzuku ya kutosha Kila mwezi, Bilioni zaidi ya 3. Mtaji wa viongozi waliopikwa ,wasomi inayo.nk nk

Mabalozi wa nyumba kumi kumi Nchi nzima ni CCM, sasa HOFU ya kushindwa vita ya Uchaguzi inatoka wapi?

Mzee Kikwete aliruhusu Mchakato wa Katiba mpya kuanza Ili kuwahakikishia WAPINZANI kuwa CCM inaweza kushinda uchaguzi Kwa namna yoyote.

Ushauri: CCM itoke mbele na kukubali Reforms kwenye Katiba Ili Tume huru ya Uchaguzi ipatikane Ili CCM ishinde Kwa kishindo na WAPINZANI wakiongozwa na TUNDU Lissu, wakose pa kuficha sura zao Kwa Aibu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Mkuu upo serious au hii ni sarcasm?
 
Mkuu upo serious au hii ni sarcasm?
Nipo serious,

CCM wakiteua wagombea Kwa HAKI wenye nguvu aina ya Mpina, wakatumia ushawishi wao na mtaji walionao na raslimali walizonazo, wakitumia mtandao wao wa kuweka mikakati ya ushindi, wanaweza kushinda uchaguzi hata iwepo Tume huru ya Uchaguzi.
 
Mwanadamu ana akili Sana . Jambo hili kama lingekuwa jepesi na hakuna athari nakwambia ccm wangekuwa wamekwishalikubali . Lakini tume huru ya uchaguzi na uchaguzi ukafanyika bila mizengwe ,ccm inaenda kuwa chama Cha upinzani . Siku kikiwa Chama Cha upinzani kitakuwa chama Bora Sana Tanzania. Aidha nasikitika tu kusema kwa asili ya watanzania wa ccm wengi watahamia katika chama kitakachokuwa madarakani
 
Viongozi wote wakubwa Lema, Mbowe, Slaa nk nk wametokea huko huko CCM baada ya kukataliwa na mfumo ovu wa RUSHWA,

Sasa CCM isingewatema ikatenda HAKI, upinzani ungekuwa wapi Leo?

Ije Tume huru ya Uchaguzi na CCM iendelee kushinda Kwa HAKI.
 
Hellow Tanzania.

Nani anaingiza HOFU ndani ya chama Cha MAPINDUZI kuwa, pakifanyika Reforms kwenye Katiba tukapata Tume huru ya Uchaguzi, kwamba CCM itaanguka na kushindwa vita ya Uchaguzi mkuu?

CCM Ina mtajj mkubwa wa wanachama Nchi nzima, na wamefanikiwa kumtangaza Mwenyekiti wa chama kwenye mabango na picha kwenye bodaboda zilizotapakaa Nchi nzima,

CCM Ina ofisi Nchi nzima Hadi mashinani huko,

CCM Ina vitegauchumi na inapokea ruzuku ya kutosha Kila mwezi, Bilioni zaidi ya 3. Mtaji wa viongozi waliopikwa ,wasomi inayo.nk nk

Mabalozi wa nyumba kumi kumi Nchi nzima ni CCM, sasa HOFU ya kushindwa vita ya Uchaguzi inatoka wapi?

Mzee Kikwete aliruhusu Mchakato wa Katiba mpya kuanza Ili kuwahakikishia WAPINZANI kuwa CCM inaweza kushinda uchaguzi Kwa namna yoyote.

Ushauri: CCM itoke mbele na kukubali Reforms kwenye Katiba Ili Tume huru ya Uchaguzi ipatikane Ili CCM ishinde Kwa kishindo na WAPINZANI wakiongozwa na TUNDU Lissu, wakose pa kuficha sura zao Kwa Aibu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
CCM hawawezi kukubali reform Kwa kuwa itawamaliza
 
Mtego upo kwenye kuachana na RUSHWA na wizi wa kura na kuifisadi Nchi,

Lakini HOFU ya kushindwa uchaguzi Kwa ujio wa Tume huru ya Uchaguzi ni HOFU ya kutengeneza tu,
Ni kweli kabisa na hapo ndio hawataki kuiacha rushwa na wizi maana umekuwa kama mila na jadi kwa wengi
Kama tukiweza kuzuia Rushwa hata robo basi tuakuwa tumepiga hatua
Lakini ipo siku hata wizi huo utagonga mwamba
 
Back
Top Bottom