Pakistan: Sadiq Masih, Mkristo mwenye umri wa miaka 40 aliyekuwa akifanya kazi katika tanuri la matofali, aliuawa baada ya kupata kiu na kunywa maji kutoka kwenye chombo cha kupoozea maji (Water cooler) ambacho wafanyaazi wenzake wa kiislam hawataki wenye dini nyingine kutumia.
Mfanyakazi mwenzake mmoja wa kiislam alimzuia kunywa maji akidai kuwa Wakristo hawakuruhusiwa kutumia maji hayo. Hata hivyo, kutokana na kiu kali baada ya kuchoma matofali, Sadiq Masih alikunywa maji hayo.
Baadaye, mfanyakazi mwingine alimshika kutoka nyuma na kumkata koo, na kusababisha kifo chake.
Sadiq Masih ameacha mke na watoto wanne.
Hata hivyo, hadi sasa haijafahamika iwapo aliechinja amechukuliwa hatua. Kumekuwa na matukio mengi ya dini nyingine wanaponyanyaswa au kuuawa, wahusika hawachukuliwi hatua au kupewa adhabu ndogo.
View attachment 3645191
Tukio hili limeibua mjadala kuhusu ubaguzi wa kidini, haki za binadamu, na usalama wa makundi ya wachache nchini Pakistan.
Source: Morning star news