Pakistan wana bidhaa nzuri na bora, lakini tumekariri Dubai, Uturuki, China na Thailand

Mimi huwa nawaza jinsi tunavyoweza kuwatumia Wapakistani kujenga viwanda vyetu vidogo. Huwa naona wana viwanda ambavyo havifiki thamani hata ya TZS 200M ila wana skills kubwa na uzoefu. Sema wanafanya kazi mazingira magumu sana
Tanzania ina tatizo la skilled labors
 
Viwanda vidogo vidogo unaweza anzisha hata wewe tatizo ni kushindana na wachina.

Utatengeneza ili uuze kwa 50,000 ila mchina atauza kwa 45,000 ubora mbovu ila Mtz ataona bora hiyo
Nilishwahi kuweka uzi w akuwapongeza serikali kwa kupiga kodi 500% kwa bidhaa za fenicha toka China, kwa sasa Workshop na viwanda vya vitanda, masofa nk. vya mbao na vya chuma vimetapakaa kila kona ya Tz, vijana wengi mno mno mno wamepata ajira kwenye sekta hiyo moja tu, imagine wangefanya hivyo kwa sekta zingine
 
VP kuhusu Bei zao na logistics nyingine
 
Kweli ila bado wenye uwezo wananunua vya nje sababu kubwa ikiwa ni ubora wa utengenezaji.

Bidhaa za siku hizi hazihitaji pure wood bali MDF, Plywood.
 
Kweli ila bado wenye uwezo wananunua vya nje sababu kubwa ikiwa ni ubora wa utengenezaji.

Bidhaa za siku hizi hazihitaji pure wood bali MDF, Plywood.
Ni sawa, ila ni wachache sana, kwa sasa sofa hizo wanazoagiza nje gharama yake inafika hadi milioni nane kwa sofa set moja, wakati mwanzo ilikuwa milioni 3, kwahiyo imesaidia sana kwa ajira za ndani
 
Kuna miaka fulani nilikuwa Tehran
Enzi za ubaharia,aise jamaa wana vitu
Vizuri sana nao

Ova

Ndio wairan nao wana balaa kubwa sana , halafu ubora wa vitu unakua mkubwa hadi unajiuliza kwa nini hawa hawakuendelea na biashara ya afrika kama miaka ya utumwa, walipompa gap mzungu hawakuwahi kurudi tena kuleta bidhaa
 
Ni sawa, ila ni wachache sana, kwa sasa sofa hizo wanazoagiza nje gharama yake inafika hadi milioni nane kwa sofa set moja, wakati mwanzo ilikuwa milioni 3, kwahiyo imesaidia sana kwa ajira za ndani
Ila watu wananunua sababu ya ubora.

Vya Tanzania vingi hutumia mbao mbovu ukikaa vibaya zinavunjika
 
Kama umeshindwa kujua tofauti ya aLovera na aRovera utajua bidhaa nzuri kweli?
 
Nadhani wameshindwa kujitangaza zaidi kupata wateja
 
Kama sikosei hata kwenye maonyesho ya 77 huwa wanaleta bidhaa zao!
 
Pakistan pia wana import toka china.Ila pia wana bidhaa nzuri hasa za nguo nguo ila bei imechangamka kidogo.Halafu security kule inakera kidogo.pia viwanda vidogovidogo vinatoa vitu interesting hasa vile vya artwork kama mapambo.

Sijajua kwa karachi,ila Islamabad pako na tension hiv.

Cement ni cheap pia.usisahau pakistani pia ni miongoni mwa nchi zenye maskini wengi sana
 
Akili ya Mwafrika, kazi kusifia vitu vya wenzake yeye mwenyewe hajiulizi ni lini atakuwa kama hao anaowasifia ??!!, tunayo safari ndefu sana ya kujitambua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…