Pale Bungeni simuoni Mbunge wa kuichambua ripoti ya CAG baada ya kukosekana Zitto Kabwe na wabunge wa CHADEMA

Tukiweka itikadi pembeni, kiukweli pale bungeni simuoni mtu mwenye uwezo wa kuichambua ripoti ya CAG kama walivyokuwa Zitto Kabwe, J J Mnyika, James Mbatia na Tundu Lissu.

Kuwa mwanasiasa mzuri ni jambo moja lakini kuwa mwanasiasa " mahiri" ni jambo lingine kabisa.

Hao niliowataja unapofika wakati wa uchambuzi wa maswala ya kitaalamu iwe uchumi, sheria au fedha huwa na udadisi wa kitaaluma siyo kishabiki.

Ripoti ya CAG iliyowasilishwa kwa mh Rais Samia leo inahitaji hoja nyingi za kibobezi/ kidadisi lakini sidhani kama akina Babu Tale na Nusrat Henje wana viwango hivyo.

Itoshe tu kusema wabunge wengi wa sasa wana uwezo mdogo na ujasiri hafifu wa kujenga hoja.
Wabunge wenu akina Babu Tale🤣🤣🤣plus vilaza akina Msukuma
 
Alaf Mbona Babu Tale anakua mfano kwenye mambo mengi ya msingi yahusuyo bunge?😂😂😂 Kama jimboni kwake wapo watu wa design yake mlitakaje?😂😂😂

Anyway This time anaweza toa hoja moja amazing na hamtaamin masikioni mwenu😂😂😂
Kuna Mbunge CCM aliyechaguliwa na wananchi?? Sidhani. Kama wapo hawazidi 50%
 
Hizi dharau ni kubwa sana na kulikosea heshima Bunge zima kuwa hakuna watu wenye weledi wa kuchambua mambo. ila sikushangai maana mmerithishwa na Mbelgiji mmoja ambaye anajiona katika nchii hii yeye ndo mtaalamu wa Sheria zote
 
Kumbuka mleta mada ni kijani mwenzenu
 
Hahahaaaa...... Kuna mambo ya kushabikia na kuna mambo ya kusimamia kweli.

Mtu kama Rajab Adadi hana kashfa yoyote tena kaongoza kura za maoni akakatwa na kuwekwa yule mwanaFA kwa sababu tu alipiga show ya Corona!

Sasa wanaletewa ukaguzi wa SGR na bwawa la Nyerere utasikia taarabu zao, bora hata angekuwemo tumbili mwenyewe badala ya mama tumbili!
Hivi mama tumbili yupo miongoni mwa covid 19?
 
Bajeti inakwenda kutekeleza ilani sasa ulitaka watukane au? Hizi stress za maisha na kukosa nafasi za uongozi katika chama na serikali zinatupeleka kubaya.
 
Tukiweka itikadi pembeni, kiukweli pale bungeni simuoni mtu mwenye uwezo wa kuichambua ripoti ya CAG kama walivyokuwa Zitto Kabwe, J J Mnyika, James Mbatia na Tundu Lissu.

Kuwa mwanasiasa mzuri ni jambo moja lakini kuwa mwanasiasa " mahiri" ni jambo lingine kabisa.

Hao niliowataja unapofika wakati wa uchambuzi wa maswala ya kitaalamu iwe uchumi, sheria au fedha huwa na udadisi wa kitaaluma siyo kishabiki.

Ripoti ya CAG iliyowasilishwa kwa mh Rais Samia leo inahitaji hoja nyingi za kibobezi/ kidadisi lakini sidhani kama akina Babu Tale na Nusrat Henje wana viwango hivyo.

Itoshe tu kusema wabunge wengi wa sasa wana uwezo mdogo na ujasiri hafifu wa kujenga hoja.
ACHA DHARAU MKUU
 
Back
Top Bottom