Pale dunia inapofumbwa kwa yale yanotokea nchini Sudan

Waafrica kilakitu tunasungizia marekani na ulaya.
Ifike kipindi waafrica tuachane na hizi propaganda za kijinga, Kwa kinachoendelea Sudan sioni sababu ya kusingizia nchi za magharibi
 
Mi sijasema uelimishi, mimi nimekutaka u- summerize ulichokikopi uko gugo na kuiweka hapa.
Kunukuu na kuweka hapa bila "acknowledgement" ya chanzo ni "plagiarism".

Mimi huwa nafanya "acknowledgement" ya vyanzo vyangu.

Ndo maana nimeweka chanzo cha uchambuzi wangu.
 
Waafrica kilakitu tunasungizia marekani na ulaya.
Ifike kipindi waafrica tuachane na hizi propaganda za kijinga, Kwa kinachoendelea Sudan sioni sababu ya kusingizia nchi za magharibi
Inachukiza sana. tumewageuza wamarekani kuwa kama miungu vile!! Wao ndiyo wanaamua nani apigane na nani asipigane tena kwa wakati wanaotaka wao.
Hizi nyuzi zinalenga kuebdeleza inferior complex kwa mtu mweusi na kuendelea kuamini kuna taifa ama mtu ndiye anaamua hatima yetu wakati hatima yetu hipo mikononi mwetu sisi wenyewe.

Shida ya Africa kwa ujumla zipo wazi kabisa lakini kuna mtu anajikita kupotosha kwa maksudi kabisa in profitless way.

Wakati wa wale wahuni Amboni na Mukuranga kuna watu (magreat thinker wa Jf) wakawa wanaasema wanafadhiliwa na marekani.. et kwasababu kuna mikataba Tanzania imesain na China hivyo Marekani imeamua kutengeneza waasi Tanzania kupitia Dini.
Watu wanaosemwa kufadhiliwa na US, Maskini wa Mungu!!!! wengine Yebo Yebo zimeisha, kanzu chafu na chakavu na walikuwa wanatembea na viroba vya unga na dagaa silaha zao nyingi ni Mapanga na shoka ila wasomi waa Jf wakawa wanasisitza humu kuwa hao jamaa ni kazi ya Marekani na ukiwapinga unaambiwa ujui chochote kuhusu Geopolitical.
 
Tende watamuachia nan huku dunian
 

Hata Muingereza na Marekani hawapendi kuona demokrasia inashamiri Afrika.

yaliyotokea Zanzibar 1964 ni mfano tu wa jinsi Uk ilivyoshiriki kuiondosha serikali iliyochaguliwa kidemokrasia na wananchi pia yaliyotokea Ghana wakati wa Nkrumah namna gani CIA ilivyomwondosha madarakani .
 
Yapo maneno mengi ambayo hutumika panapokuwa na migogoro inohusika wakubwa wa dunia maneno kama- "Geopolitics", "Hegemony", "Imperialism", Unipolar, Multipolar, Warmongering, Military Aggression, Proxy War, Nuclear Armageddon, Imperialist Powers, Strategic Autonomy, Vassalisation, Great Reset, New World Order, Deep States, Remilitarization,

Haya ni baadhi tu ya maneno ambayo katika diplomasia ya kimataifa ni lazima uyatumie.

Ila elewa Sudani ni moja ya nchi za Afrika ambazo zimegeuzwa kuwa uwanja wa vita vya miamba ya dunia kugombania rasilimali.

Kwa mfano, "Hegemony" ni kuongeza wigo wa eneo la kujidai kwa kutumia njia na mbinu za kijeshi kuingia katika ardhi ya nchi ingine.

Soma vitabu viwili vinoelezea "geopilitics" walivoandika wazee Henry Kissinger na Zbigniew Brzezinski vya Diplomacy na kitabu kingine cha "The Grand Chessboard"- "American Primacy and its Geostrategic Imperatives".

Hawa wazee wameeleza ni kwanini hata baada ya kuanguka kwa USSR sera ya Marekani ya kuhakikisha kujipanua au Expansionism yahakikisha Russia haiwi tishio kwake.
 
HiI vita ya uchumi haijawahi muacha mwafrica salama. ..Somalia-gas,mafuta...DR Congo.-madini,Chad, Niger,Sudan,libya-hill zone linautajiri mkubwa sn wa madini,mafuta and gas ambayo wamagharibi wanayahitaji sn...mnavurugwa wao wanabeba Mali. ..Libya wamefibeba wapendavyo,Somalia ndio shamba Lao kabisa...Congo jamaa wanabeba kwenda ubelgiji. ..hata vita ya Ukraine ni malighafi zilizopo mlendio wanazozitaka
 
Hakuna watu walokosa akili, vichwa vitupu kama Afrika hasa wenye itikadi za kiislamu.

Shida yoyote ambayo ipo, hawana jibu lingine zaidi ya US. Kila kitu kwao ni US, ni wapuuzi sana.

Yaliyopo Congo na yaliyotokea kwa Patric Lumumba hivi wale ni waislamu ?? Soma history ya CIA na Africa ndio utaelewa , labda una chuki zako za kibinafsi kuhusu waislamu.
 
Mpaka sasa nchi za Misri, Saudi Arabia, Iran, Syria, Ukraine, Hispania, Italia, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Marekani na zingine, zimetuma ndege za kijeshi na wanajeshi maalum kufanya shughuli za uokoaji wa raia wake. Djibouti ndo pamekuwa kituo cha kufikia wageni mbalimbali kabla kusafirishwa kwenda nchi zingine.


SASA UKRAIN INAWAPELEKA WAPI RAIA WAO!? [emoji23] [emoji23]
 
" "

SANA UKRAINE INAWAPELEKA WAPI RAIA WAO [emoji23] [emoji23]
 
Waafrica kilakitu tunasungizia marekani na ulaya.
Ifike kipindi waafrica tuachane na hizi propaganda za kijinga, Kwa kinachoendelea Sudan sioni sababu ya kusingizia nchi za magharibi
Kama Afrika imetawaliwa na mataifa ya magharibi basi bara hili haliwezi kujikomboa kamwe.

Litazushiwa zogo na kila dhahama kutoka nje.

Sababu moja kubwa ni kwamba tuna hazina kubwa ya rasilimali na hao wa nje hawana.

Waliiba wakati wa ukoloni na imeisha wamepagawa.

Waafrika bado hatujajitambua tu maskini, na leo hii haohao wa nje hawatutaki huko kwao ukienda huko kama mkimbizi watakupeleka Rwanda.

Na hata hii operesheni inoendelea ya uokozi ni kwa wale raia wenye pasi za kusafiria za nchi husika kama Marekani, Uingereza, Ujerumani Italy ndo wanoruhusiwa kupanda ndege na kama una viza ya kawaida kama ya kudumu basi hiyo imekula kwako.

Waafrika tuamke usingizi mzito na mtamu lakini wenye madhara makubwa huko mbele.
 
Ukraine imeokoa raia wake ambao wengi ni wataalam wa masuala ya anga na marubani pamoja na mafundi na imewapeleka Misri.
 
Reactions: B51
Mkuu Richard umeandika bandiko refu mno na kuweka mambo mengi sana kiasi cha kuhatarisha kueleweka kwa dhumuni (objective) ya mada na michango unayoitarajia toka kwa wasomaji. Usishangae kuona kila mchangiaji akisema chake bila kueleweka kama anakuunga mkono au anakupinga.

Mimi nimeona umeitaja Darfur kama sehemu ya South Sudan. Sijui kwa maana ipi hasa. Navyojua hii ni sehemu ya Sudan (Western Sudan) inayokaliwa na watu weusi ambao predominantly ni Waislamu. Na ndiko migodi ya dhahabu inayodhibitiwa na Hemedti na Urusi (Wagner forces) iliko. South Sudan inatamba zaidi na visima vya mafuta.
 

 
Reactions: B51
Nililenga kutaja Juba, ila nikaongeza Darfur kama sehemu iloathirika na vita vya wasudani weusi na majeshi ya Khartoum.

Ila ni kweli Darfur ipo magharibi kama jimbo linojitegemea na ndiko anakotokea Jenerali Dagalo.

Lengo la mada yangu ni kuonyesha kwamba pamoja na kwamba Sudan pamekuwepo vita kwa miaka mingi, vita hivyo vimechangiwa na mataifa ya nje ambayo yana kambi tofauti, kambi ya Dagalo, kambi ya Burhan na kambi ya Hamdok.

Na kihistoria nikasema Sudan lilikuwa ni koloni la Uingereza na upande wa Khartoum ndo ulopendelewa kwa kila kitu, huku upande wa kusini ambao ndo wenye rasilimali ukiwa hauna chochote ila ndo wenye rasilimali.

Lakini leo hii, dunia imefumbwa kwa kuambiwa na kuaminishwa kwamba vita vya safari hii baina ya jeshi na RSF ionekane imetengenezwa au kuanzishwa na wasudani wenyewe lakini ukweli halisi ni kuwepo kwa mashinikizo kutoka nje.

Kumbuka safari hii hakuna raia mitaani wanopigana bali ni wanajeshi na wanamgambo, raisi wote wamejifungia ndani.
 
Ndugu yangu jihadhari na hizi hoja nyepesi nyepesi. Matatizo ya Waafrika chanzo kikuu ni sisi wenyewe.

Mfano. Tumeipigania Sudani ya Kusini ijitenge ikafanikiwa. Mara viongozi wakawahi kuanza kutengeneza madili/mikataba ya kifisadi na mafia wa kimataifa ili wajichotee mafuta na rasilimali za nchi na kuwafungulia akaunti Uswisi. Mara wakaanzisha vita ya wenyewe kwa wenyewe silaha zikitoka huko huko nje kwa mafisadi washirika! What is this?

Afrika ya Kusini ilikuwa hivyo hivyo baada ya Mandela kustaafu.

Unaweza kuamini kuwa maRais wa kiafrika walioko madarakani na waliostaafu wanakuwa na utajiri unaowazidi kwa mbali maRais wa taifa kubwa kama Marekani na wale wa Ulaya. Halafu bila aibu wanaweka hela zao huko huko Marekani na Ulaya?

Sisi ni watoto kwamba tuwe tunarubuniwa na kulazimishwa kila wakati baada ya zaidi ya miaka 60 ya uhuru? Hatukui wala kukomaa? Hatuelimiki? Hatujijengei ujasiri? Basi hatuna haja ya kuwepo duniani!
 
Umaskini wachangia sana ndo maana mtu akipat amadaraka yeye awaza kuiba tu kwanza kabla ya mambo mengine.

Sisi waafrika ni "vulnerable" na ni rahisi sana kurubuniwa kama haujitambui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…