Pale mke anapofungwa miaka 30 jela na hurusiwi kuongeza mke, hii hali inatatuliwa vipi?

Pale mke anapofungwa miaka 30 jela na hurusiwi kuongeza mke, hii hali inatatuliwa vipi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
1651479110978.png

Katika sheria za dini za kikiristo ni kwamba hurusiwi kuongeza mke na kifo pekee ndicho cha kuwatenganisha, kinyume na hapo ni nje ya sheria za ukristo.

Sasa inapotokea mfano mke wako anafungwa jela miak 30 ama hata kifungo cha maisha na bado hamna hata mtoto, ndoa bado ilikuwa mbichi, hapo hii hali inatatuliwa vipi?

Haiwezekani Mungu aweke sheria ya kukubana sehemu flani na asiweke mlango wa kutokea, hizi sheria za kuoa ni za viongozi wa makanisa na sio maandiko,

MUHIMU: Wanaokwenda jela sio wote wenye hatia, wengine wamebambikiwa
 
Unakuwa na mchepuko wa kudumu unaweza kumuita rafiki wa kudumu.
Hio ni dhambi, mahusiano pekee baina ya mwanamke na Mwanaume ambayo Mwenyezi Mungu huyabariki ni yale ya kwenye ndoa tu, nje ya hapo hayo mahusiano hayana chembe yoyote ya baraka zake Mungu
 
Hio ni dhambi, mahusiano pekee baina ya mwanamke na Mwanaume ambayo Mwenyezi Mungu huyabariki ni yale ya kwenye ndoa tu, nje ya hapo hayo mahusiano hayana chembe yoyote ya baraka zake Mungu
Yesu alipoletewa yule kahaba aliyehukumiwa kutupiwa mawe alisema asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe. Wote waliondoka. Kuna dhambi unatenda kutokana na mazingira unayoishi au uliyonayo..

Waislam wanaruhusiwa kula nyama ya pork kama hakuna chakula kingine.
 
Uislam umeruhusu Talaka katika mazingira yasiyoeleweka

hata Mwanaume akitokomea bila ya Taarifa Mwanamke ana haki ya kujivua na kuendelea na mambo yake

Mkataba wowote ulioingia kwa hiyari lazima uwe na uhiyari wa kuendelea nao na ndio sababu kwenye Uislam wakati ule ule unapofungishwa ndoa na Sheikh lazima ukumbushwe kuna kuachana na ikibidi achanani japo haimpendezi Mungu ila kairuhusu
 
Hakuna cha vatican wala cha marekani, sheria za ukristo ni kwamba huwezi kuongeza mke na kitu pekee cha kuwatenganisha ni kifo
Vitu vingine muwe mnawauliza hata majirani zenu huko mnakokaa sio lazima kuvileta jukwaani.

Ndoa sio lazima itenganishwe na kifo, hata ikigundulika mwanaume hadindishi ukitoa taarifa ikithibitika kweli ndoa inavunjika ( ya kikatoliki)
 
Uislam umeruhusu Talaka katika mazingira yasiyoeleweka

hata Mwanaume akitokomea bila ya Taarifa Mwanamke ana haki ya kujivua na kuendelea na mambo yake

Mkataba wowote ulioingia kwa hiyari lazima uwe na uhiyari wa kuendelea nao na ndio sababu kwenye Uislam wakati ule ule unapofungishwa ndoa na Sheikh lazima ukumbushwe Luna kuachana na ikibidi achanani japo haimpendezi Mungu ila kairuhusu
Kwenye uislam washaruhusiwa kuoa wake hadi wanne.

Kazi ipo kwa wakristo ambako maandiko yameruhusu ila viongozi wa makanisa ndio hutunga sheria zao za ovyo.

Mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanaume mbele ya Mungu, Fullstop!!
 
Hizo dini huwa mnazisoma mawazo mmeweka wapi?

Nani alikwambia kuoa mke mwingine ni kosa..

Manabii..ibrahimu, yakobo, sulemani n.k
Mababu zetu wa kiafrika walioa wake wengi.. na maisha yalikuwa powa.

Achaneni na mafundisho ya kutishana wakuu..huwezi kushindan na mwanamke hapa duniani.. oa kama uchumi nguvu na uchumi unao
 
Yesu alipoletewa yule kahaba aliyehukumiwa kutupiwa mawe alisema asiye na dhambi awe wa kwanza kumrushia jiwe. Wote waliondoka. Kuna dhambi unatenda kutokana na mazingira unayoishi au ukiyonayo.

Waislam wanaruhusiwa kula nyama ya pork kama hakuna chakula kingine.
Ni rahisi sana kuwajua watu mnaochezaga tu nyimbo za gospel ila neno ni sifuri 😂😂

Huna point kabisa hapo, Kwahiyo wewe unachotaka kusema ni kwamba dhambi zihalalishwe ?
 
  • Thanks
Reactions: THT
Uislam umeruhusu Talaka katika mazingira yasiyoeleweka

hata Mwanaume akitokomea bila ya Taarifa Mwanamke ana haki ya kujivua na kuendelea na mambo yake

Mkataba wowote ulioingia kwa hiyari lazima uwe na uhiyari wa kuendelea nao na ndio sababu kwenye Uislam wakati ule ule unapofungishwa ndoa na Sheikh lazima ukumbushwe Luna kuachana na ikibidi achanani japo haimpendezi Mungu ila kairuhusu
Kitu hakimpendezi Mungu. Binadamu, kwa kupitia ushehe, anakiruhusu. Kwa hiyo shehe ni zaidi ya Mungu! Tufuate anayoruhusu shehe hata kama tunajua kitu hicho hakimpendezi Mungu!
 
Haina mjadala unaoa tu mwngne, wakati mwngne tujue kuwa hiz din n sheria na sheria zmewekwa ili zvunjwe teh teh teh!
Bora kuoa mwngne kuliko kuanza kudanga huku na kule, oa akitoka jela uje kuomba ushaur tena.
 
ni sheria tu ndio hatuzijui na hatuzisomi
kila magereza inatakiwa kuwa na chumba maalumu kwa ajili ya mke na mume wanapoitaji faragha ikiwa mmoja wao kafungwa.
na pia kuwa jela haina maana hautakiwi kuzaa. akiwa jela atapata huduma zote km mzazi na binadam.
tembeleni jela za wanawake mkaone wakiwa waja wazito na watoto
 
Legally kuna presumption of death
Kama mtu kafungwa zaidi ya miaka 5 mume au mke anaweza oa au olewa na mtu mwingine
Kwa hiyo tuna presum amesha kufa
 
Vitu vingine muwe mnawauliza hata majirani zenu huko mnakokaa sio lazima kuvileta jukwaani.

Ndoa sio lazima itenganishwe na kifo, hata ikigundulika mwanaume hadindishi ukitoa taarifa ikithibitika kweli ndoa inavunjika ( ya kikatoliki)
Si kweli unayoyasemea kwa Ukatoliki. Vigezo vitatu vinahitajika kwa ndoa kutambuliwa katika Kanisa Katoliki:
1. Ndoa iwe kati ya mwanamme na mwanamke.
2. Ndoa ifungwe (iwe 'solemnised') na mtu mwenye madaraka ya kufungisha ndoa.
3. Ndoa iwe 'consummated' yaani tendo la ndoa lifanyike kati ya maarusi.

Vigezo viwili vya kwanza vinaweza kutokea, lakini cha tatu kikakosekana. Hapo hakuna ndoa. Kwa mfano Padri ashuhudie arusi kanisani na kuwapa kabisa maarusi cheti cha ndoa. Usiku huo mme anaomba waahirishe unyumba kwa kuwa amechoka mno na pilka pilka za arusi. Kesho yake anaumwa tumbo. Siku inayofuata kuna sababu nyingine, mpaka mwezi unakatika bila unyumba kufanyika kati ya maarusi hawa. Baadaye inakuja kuthibitishwa kwamba mwanaume ni hanithi: hawezi kufanya tendo la ndoa. Kikanisa, kitakachofanyika ni 'annulment' ambayo ni kusema kwamba, japo Padri alifungisha 'ndoa' hiyo, ukweli ni kwamba hakukuwa na ndoa kwa kuwa kigezo cha tatu hakikutimizwa. Kwa hiyo, 'ndoa' hiyo itafutwa kwa 'annulment', yaani kwa kutamka kwamba hakukufungwa ndoa kati ya wahusika. Hapa hakuna talaka kwa kuwa hakuna ndoa iliyofungwa ili sasa ikomeshwe kwa talaka.

Mfano mwingine ambapo 'annulment' hufanyika ni pale mtu na dada yake waoane kanisani bila kujua kwamba wao ni ndugu wa damu. Wanaweza wakaishi katika 'ndoa' yao kwa miaka mingi wakazaa na watoto. Pindi ikijulikana kwamba wao ni ndugu wa damu, 'ndoa' hiyo itasitishwa kwa 'annulment' ambayo ni kusema kwamba ndoa ilikuwa batili japo ilifungishwa na Padri. It was nul and void. Hakuna talaka hapa kwa kuwa hakukuwa na ndoa.
 
Imeandikwa wapi kwamba manabii na mitume walifungisha watu ndoa

Ndoa ni makubaliano ya watu wawili mke na mme

Kuaoa au kuacha kuoa ni maamuzi yako wewe mwenyewe kwa sababu suala la ndoa ni suala linalohusu mwili wa mtu Wala sio suala la kiroho
 
Vitu vingine muwe mnawauliza hata majirani zenu huko mnakokaa sio lazima kuvileta jukwaani.

Ndoa sio lazima itenganishwe na kifo, hata ikigundulika mwanaume hadindishi ukitoa taarifa ikithibitika kweli ndoa inavunjika ( ya kikatoliki)
Inamaana ile mpk kifo,
Kinakua Ni kiapo batili au[emoji848]
 
Back
Top Bottom