Pale samaki alipotuhumiwa kuzamisha meli ya uvuvi haramu

Pale samaki alipotuhumiwa kuzamisha meli ya uvuvi haramu

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Ukisikia kuna kupungukiwa akili, ndiyo huku.

Ukikaa mbele ya luninga yako, halafu ukasikia kuwa mazalio ya samaki yanaharibiwa na wavuvi maharamia wa majini. Halafu baadaye ukamsikia mvuvi haramia akitamka kuwa wameanzisha mapambano dhidi ya samaki kwa sababu amezamisha meli ya kisasa ya uvuvi, utasema nini?

Hakika utasema, huyu haramia mvuvi, licha ya siku zote kufahamika ni haramia, ina maana sasa amekuwa mwendawazimu na kichaa?

Eti Mbowe ni gaidi, ama kweli Duniani vioja haviishi.

Miaka ya nyuma nikiwa Sekondari, Mkuu wa Shule alienda Arusha kwaajili ya selection ya wanafunzi wa kwenda kidato cha tano, aliporudi akasema, majitu yasiyo na nidhamu, yenye akili ndogo yanawezaje kulinda usalama? Mkuu huyo wa shule, anasema kuwa kwenye karatasi ihusuyo mwanafunzi mmoja toka shule moja, mkuu wa shule alindika:

"Mwanafunzi huyu uwezo wake darasani ni wa chini sana, ni mkorofi, mara mbili amewahi kukamatwa kwa wizi wa vifaa vya wanafunzi wenzake, pia mara nyingi amewahi kutoroka shule usiku na kwenda kunywa pombe za kienyeji kijiji cha jirani, aliwahi kutuhumiwa kushiriki tendo la ubakaji lakini ushahidi ulikosekana, aliwahi pia kukamatwa na chumvi aliyoiba kwenye jiko la shule ambayo alikuwa akibadilisha na pombe za kienyeji, nadhani kazi pekee ambayo inaweza kumfaa ni kuwa POLISI!"

Yule mkuu wa shule akashangaa ni kwanini mtu mwovu, kazi itakayomfaa iwe ni ya ulinzi wa usalama!
 
Bahati mbaya mtu muovu huwezi kumtambua kwa sura maaana uovu wa mtu uko moyoni mwake, huwezi kumtambua kwa muonekano wake au matendo au mazungumzo, ni wajanja sana na wanajua kuhadaa ili asitambulike undani wake.
ktk maeneo yetu tunaishi na majambazi, wauza unga n.k lkn ni vigumu sana kuwatambua kwani huwa tunaenda nao kwenye majumba ya ibada na hujionesha wachamungu kweli kweli, sasa ngoja siku akibainika kila mtu huduwaaa na kuacha kinywa wazi......
huanza kusema hata huyu!! kumbe alikuwa jambazi?! kumbe alikuwa muuza madawa ya kulevya wakati alikuwa anatoa sadaka?!
ndio maana leo pia tuna shangaa inawezekanaje Mbowe kuwa gaidi!! inawezekana kwa sababu nafsi ya mtu ni kichaka huwezi kujua alicho nacho moyoni, mm na ww hatujui zaidi ya ushabiki tu.
tuache vyombo vyetu vifanya kazi zake.
 
Tuhuma zipo kwa yeyote yule, Mbowe Ni mwanadamu lazima achunguzwe ili kubaini Kama kweli Ni gaidi au siyo!

Relax dude!!!
 
Back
Top Bottom