Pale tunapotakiwa tukasirike tunacheka, na pale tunapotakiwa kucheka eti tunakasirika! Nchi ya ajabu sana hii!

Pale tunapotakiwa tukasirike tunacheka, na pale tunapotakiwa kucheka eti tunakasirika! Nchi ya ajabu sana hii!

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Nilitarajia kuona kila mtanzania amekasirika na kuonyesha hisia zake hasaa kwenye mambo yafuatayo;

Ufisadi
Kwanini kuwachekelea waliopewa mamlaka kusimamia haki za wananchi pamoja na kulinda kuhakikisha hakuna shilingi ya Mtanzania inakwapuliwa na mafisadi?

Anatokea mtu mmoja tu kusema hili lisijadiliwe tena hapa, kwa mamlaka yake, anasema kwa muda atakoona yeye ndio lijadiliwe! Bado tunakenua meno kuchekelea?

Mtu anafamika kabisa kwamba, yeye ni mwizi na fisadi na hana ufanisi wowote, anapewa kuongoza idara ama wizara, tunachekelea tu eti safi sana mteuzi umepiga penyewe!

Ajira zinatoka, kunaibuka jambo kwamba, kiongozi fulani kuweka watu wake pale, katumia mamlaka yake kuchomeka ndugu zake, eti tunakenua meno kuchekelea tuu

Kwa sasa Watanganyika mna kero kubwa ya muungano! Shida inaanzia pale! Wa upande wa pili karibu kila kitu huko Tanganyika ni vyao, ila vyao huko kwao ni vyao pia!

Wa kule wanaweza kuajiriwa Tanganyika, wa Tanganyika nao waajiriwe Tanganyika tu, kule, hapana. Wa kule, wanunue mashamba, viwanja n.k, ila wa Tanganyika, thubutu yao!

Hayo ndio mambo ya kuonyesha sura za watu kwamba, kumbe zimejaa mistari mistari mingi usoni, na sio ya kuchekelea tuu! Hayo, yanapaswa yatulete pamoja kama Taifa moja kuyaweka sawa na hatimaye kusonga mbele.

Ninauhakika haya yakiachwa, wale ambao wameyashikilia kwa magumu wataondoka, watakao baki ndio watakuja kupata tabu sana namna waende.

Tusinune wala kukasirika mahali tunapaswa kufurahi na tusicheke na kufurahi mahali tunapaswa kukunja ndita na kukasirika
 
Makundi tofauti ya kimtazamo juu ya utawala wa awamu ya 5 kuhusu mambo mbalimbali yote yako sawa maana kila mmoja ana maoni yake shida inakuja pale kundi fulani linapo taka maoni Yao yawe maoni jumla kutokana na mitizamo Yao hili haliwezi kuja kutokea hata siku moja.

Watanzania tumegawanyika katika ushabiki wa kivyama kiasi kwamba agenda muhimu zinazi husu maslahi makubwa ya umma tunajadili kupitia itikadi zetu na mwisho tunapoteza dira suala la wizi wa Mali ya umma kupitia repoti ya CAG ilitakiwa kuwa agenda ya taifa na sio kundi fulani maana walipa Kodi wanamzigo mkubwa sana.

Moja ya makosa ambayo tunafanya kila uchwao ni kuweka tumaini kwenye Bunge kibogoyo kufanya maamuzi magumu kwenye agenda muhimu kwa katiba yetu hii ni nadra sana kutokea kwa Jambo hilo hivyo hakuna tumaini pale maana hata uhalali wa uwepo wao ni mjadala mkubwa

Keep za muungano zilitolewa maoni mazuri tu kupitia tume ya Jaji Warioba hivyo ni muda wa umma kupaza Sauti rasimu ya Jaji Warioba ambayo ndio yenye maoni ya umma kuheshimiwa na mwisho tupate katiba mpya
 
Back
Top Bottom