May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Kila tarehe moja mwezi wa nne kama leo huwa inatajwa kama ni siku ya Wajinga Duniani, ingawa si siku inayotajwa rasmi na Mamlaka za Nchi lakini Wananchi wake wamekuwa wanaziadhimisha kivyaovyao.
Nimekuwa nikishuhudia na kugundua ya kuwa karibia asilimia 99 ya Watanzania huwa Wanawadanganya Wenzao na kisha kukaa pembeni kushangilia kwamba wamefanikiwa 'kuwajingisha' Wenzao hao.
Hii si sawa maana kumdanganya Mtu kuwa Mzazi wake amelazwa Hospitali naye akaacha shughuli zake akakimbilia Hospitali sioni ni kwa vipi wewe umefanikiwa 'kumjingisha' sanasana hapo umemdanganya na umefanya jambo la hatari sana linaloweza kuishia kwa kuleta madhara.
Hii si sawa hata kidogo, na inaonesha dhahiri kwamba ni vigumu sana kwa Wajinga kutofautisha haya mambo mawili.
UJINGA ni pale unapomwambia Mtu jambo lisilowezekana naye bila kutumia akili anaamini kirahisi tu, kwa mfano unamwambia Mtu au Watu kuwa kuna shamba limemea tambi na kwamba naye anaweza kwenda huko kuvuna, naye akainuka na kwenda.
Au kama unamwambia Mtu kuwa kuna mpango wa kupunguza urefu wa Mlima Kilimamanjaro na sehemu ya kifusi kuhamishiwa Mlima Meru na kuufanya Mlima Meru kuwa mrefu zaidi.
Au unamwambia Mtu aende Posta jijini Dar Es Salaam akamuone Mtu ambaye (kama alivyo) ana uwezo wa kuruka kutoka ghorofa ya kumi na mbili na kutua kwenye lami bila kudhurika, naye kama zuzu anaamini kuwa inawezekana.
Kiukweli ujinga hufanyika mara nyingi sana tu hapa Bongo wala hatuhitaji kusubiri tarehe moja mwezi wa nne, tumeshasikia mara kadhaa Watu wakikusanyika eti kuna Mtu kageuka Chatu, au kuna Mti umegoma kukatwa au ukikatwa unarudi pale pale n.k.
Ni hatari sana kwa Wajinga kuachwa kufanya ujinga maana wataishia kuumizana tu.