Palikuwa na uamuzi na miito ya kutokushiriki chaguzi bila katiba mpya. Ya nini kulia lia sasa?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Ni kawaida manabii kutokukubalika kwao. Lipi linalotokea kwenye kuelekea chaguzi za 2024/25 kuwa ni jipya leo?

Kwamba walienguliwa wagombea, kukavurugwa kampeni, wakakamatwa wapinzani, nk?

Kwamba yote hayo ni marudio ya 2019/20?

Kwani hoja na makelele ya nguvu yalipotamalaki, hatukuahidiana kukumbushana ikifika leo?

Waombwe waheshimiwa wanaolia lia sasa kukaa kwa kutulia.

Kwamba hiyo ni sehemu muhimu kwenye kuchagua kucheza pata potea!
 
Utawasikia wakinengua na kuimba CHADEMA IMEPOTEZA umaarufuuu!
Yaañi chama kipoteze umarufu halafu polisi wakamate viongozi wake kila mara?
Kwann wasikamate wa ADC au CCJ au TlP au NCCR?
 
Naunga mkono Israel 😂😂

Hata ICC inawaunga mkono hao.

Ndiyo maana makamanda tuliopeana miadi wamekubali yaishe:

IMG_20211016_132442_593.jpg

Wamekaa kwa kutulia!

imhotep, Moisemusajiografii, Mzee Kigogo, Yoav Gallant au nasema uongo?
 
Chadema ilikosea sana kuamini maridhiano
Chadema wakaiweka pembeni ajenda ya kudai katiba mpya na kukomaa na maridhiano. This is the biggest blunder to regret.
 
Utawasikia wakinengua na kuimba CHADEMA IMEPOTEZA umaarufuuu!
Yaañi chama kipoteze umarufu halafu polisi wakamate viongozi wake kila mara?
Kwann wasikamate wa ADC au CCJ au TlP au NCCR?

Kuridhia kufanya chaguzi bila katiba mpya ni "pain in the arse."

"Kwamba hiyo ni sehemu muhimu kwenye kucheza pata potea!"
 
Chadema wakaiweka pembeni ajenda ya kudai katiba mpya na kukomaa na maridhiano. This is the biggest blunder to regret.

Kuteleza si kuanguka.

Kupajua lilipotokea anguko, ni fursa.

Ukombozi si lelemama!
 
Ni kawaida manabii kutokukubalika kwao. Lipi linalotokea kwenye kuelekea chaguzi za 2025/25 kuwa ni jipya leo?

Kwamba walienguliwa wagombea, kukavurugwa kampeni, wakakamatwa wapinzani, nk?

Kwamba yote hayo ni marudio ya 2019/20?

Kwani hoja na makelele ya nguvu yalipotamalaki, hatukuahidiana kukumbushana ikifika leo?

Waombwe waheshimiwa wanaolia lia sasa kukaa kwa kutulia.

Kwamba hiyo ni sehemu muhimu kwenye kuchagua kucheza pata potea!
Gentleman,
kelele za hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi zilikua kelele za chura tu 🐒
 
Kwamba hiyo ni sehemu muhimu kwenye kuchagua kucheza pata potea!
Chama A kipo madarakani
Chama B kipo upinzani
Ikigundulika Wananchi wanamtaka mgombea wa Chama B basi Chama A kinatumia mabavu kumtangaza mgombea wao na sanduku la kura halizingatiwi tena, wenyewe wanasema wao Viongozi wa Chama A ndio wenye haki na Wananchi pamoja na Chama B hawana haki km hawatoridhika na kutangazwa kwa mgombea wa Chama A ambae ameshindwa kura kwenye uchaguzi km mshindi waende wakashtaki mbinguni, hio ndio principle na process za Chama A hakiangalii haki za Wananchi kwa maana Wananchi hawana haki wao Viongozi wa Chama A tu ndio wenye haki ya kuamua kipi kiwe nini na kipi kiweje

Mwisho wa kunukuu.
 
Swali la msingi:

"Kulikoni chama B kujitosa kwenye uchaguzi huo na kulia lia yakiwakuta?"

Mwisho wa kujiuliza.
 
Lissu kamuambia Mbowe kwamba kukamatwa kwake kule Mbeya kuwe fundisho la kutokukimbilia maridhiano na watawala. Maana Mbowe alikuwa anaambiwa ila hasikii anadai ana Imani na Samiah.
 
Hapo hakuna cha kufanya sababu ni suala la Muda tu yanajirudia yaleyale hakuna Tume Huru ni Tume ya Chama A kwa hio mfano mdogo tu unaoeleweka Mimi tumbuli wa Chama A wewe kima wa Chama B tumeingia kwenye uchaguzi msimamizi wa uchaguzi anatokea upande wa tumbili Chama A wakati wananchi wanamtaka kiongozi atoke Chama B yaan kima kwanini yule msimamizi wa tumbili wa Chama A ambae amewekwa na tumbili wa Chama A asiwatangaze tumbili wenzie wa Chama A kua ndio washindi hata km wameshindwa? Lengo la kuwekwa msimamizi wa Chama A cha tumbili ni kuwapitisha tumbili wote wa Chama A na kuwapa ushindi wawe wameshinda kweli au wameshindwa vibaya kwenye sanduku la kura. Umenielewa vizuri
 
Hapo hakuna cha kufanya sababu ni suala la Muda tu yanajirudia yaleyale hakuna Tume Huru ni Tume ya Chama A kwa hio mfano mdogo tu unaoeleweka Mimi tumbuli wa Chama A wewe kima wa Chama B tumeingia kwenye uchaguzi msimamizi wa uchaguzi anatokea upande wa tumbili Chama A wakati wananchi wanamtaka kiongozi atoke Chama B yaan kima kwanini yule msimamizi wa tumbili wa Chama A ambae amewekwa na tumbili wa Chama A asiwatangaze tumbili wenzie wa Chama A kua ndio washindi hata km wameshindwa? Umenielewa vizuri

Kwamba hakuna cha kufanya, ni kauli ya faraja sana kwa chama A.

Cha kufanya kipo na ndiyo maana Mdude wangali naye.

Si kuwa chama A hakisikii au kuwa ni viziwi.

Chama A ipo lugha kinayoielewa vyema na hiyo ni lazima isikike.

Bila katiba mpya chaguzi zozote ni kusubiria yale Yale kujirudia.
 
Lissu kamuambia Mbowe kwamba kukamatwa kwake kule Mbeya kuwe fundisho la kutokukimbilia maridhiano na watawala. Maana Mbowe alikuwa anaambiwa ila hasikii anadai ana Imani na Samiah.

Sheitwani hana undugu.

Learning it the hard way.
 
Kwamba hakuna cha kufanya, ni kauli ya faraja sana kwa chama A.

Cha kufanya kipo na ndiyo maana Mdude wangali naye.

Si kuwa chama A hakisikii au kuwa ni viziwi.

Chama A ipo lugha kinayoielewa vyema na hiyo ni lazima isikike.

Bila katiba mpya chaguzi zozote ni kusubiria yale Yale kujirudia.
Ndio mkuu, sasa Chama A hilo suala la katiba hakitaki kabisa kusikia ndio maana yule Mzee fulani ambae na yeye ni mwanachama halisi wa Chama A walimkata makofi tena waliomkata makofi ni watoto wake wa kuwazaa kabisa ni pale tu aliposimama kidete kwenye kutaka katiba iliyopo iondolewe iletwe ya Wananchi kwa maana hio hilo sahau kuhusu katiba mpya yaan kwa Chama A ukigusa katiba tu ni sawa umegusa msumali wa moto kwenye kidonda hawataki kabisa kusikia unatajataja katiba na katiba inayopendekezwa hawaitaki wao wanataka katiba yao ile ile ya tangu na tangu iendelee kuwepo na kuhakikisha tumbili wote wanaendelea kua madarakani hakuna kima wa Chama B anaeingia kwenye uongozi hio ndio sera ya Chama A
 
Chama B kuridhia matakwa ya chama A na baadaye kulalamika, ndipo ulipo msingi wa hoja.

Ukiridhiana na chama A kwa misingi yoyote, kulikoni kulia lia yakikukuta yanayojulikana?
 
Back
Top Bottom