Pamba Jiji wanadai kuzimiwa taa wakati wakifanya mazoezi ya mwisho uwanja wa Benjamin Mkapa

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Klabu ya Pamba Jiji yenye makazi yake Jijini Mwanza wanadai kuzimiwa taa wakati wa mazoezi yao ya Mwisho kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga Sc hapo kesho.

"Hii ndiyo hali tuliyokutana nayo uwanja wa taifa, taa zimezimwa tumefanya mazoezi gizani".
 
Timu ya Pamba Jiji FC ya Mwanza wakiwa wanafanya mazoezi uwanja wa Taifa Saa 1 usiku kwenye giza kwakuwa taa hazikuwashwa. Pamba wanacheza na Yanga SC kesho uwanjani hapo mida ya Saa 1 usiku, kwahiyo Pamba walikuwa hapo kutekeleza kanuni ya kufanya mazoezi uwanja wa mechi walau siku 1 kabla ya mechi muda uleule wa mechi, walichokumbana nacho na kupost kwenye Instagram yao ndo hicho.

Kwani mimi nawaonea huruma? Wao si huwa wanajipendekeza kwa kuihujumu Simba? Si mnalikumbuka lile li Mkuu la Mkoa wa Mwanza lenye kichwa kama trekta ya Massey Ferguson lilichoifanyia Simba pale CCM Kirumba?
 
Haihusiani na Pamba jiji. Simba walikuwa wanacheza na Yanga na sio Pamba
 
Mimi nawashauri badala ya kulalamika, wangetoa taarifa kwa wahusika wa uwanja. Na kama hakuna ushirikiano, wapeleke mashtaka yao ngazi inayohusika.

NB; Nina uhakika Yanga haitahusishwa kwa namna yoyote ile. Maana hawana huo muda, na pia sababu ya kufanya hivyo.
 
Taa kuzima uwanja huo sio jambo la kushtua maana ilishawahi kutokea wakati mechi inaendelea.

Waache janjajanja wasubiri kichapo kesho.
 
Mimi nawashauri badala ya kulalamika, wangetoa taarifa kwa wahusika wa uwanja. Na kama hakuna ushirikiano, wapeleke mashtaka yao ngazi inayohusika.

NB; Nina uhakika Yanga haitahusishwa kwa namna yoyote ile. Maana hawana huo muda, na pia sababu ya kufanya hivyo.
Yaleyale ya tarehe 8, wale jamaa wakakimbia
 
Mimi nawashauri badala ya kulalamika, wangetoa taarifa kwa wahusika wa uwanja. Na kama hakuna ushirikiano, wapeleke mashtaka yao ngazi inayohusika.

NB; Nina uhakika Yanga haitahusishwa kwa namna yoyote ile. Maana hawana huo muda, na pia sababu ya kufanya hivyo.
Msemaji!!
 
Na Leo si wanacheza mpira saa Moja jioni basi waseme wazime taa ili mpira uchezwe gizani maana wao Wana uzoefu walifanya mazoezi Jana gizani🙂
 
Back
Top Bottom