LGE2024 Pambalu: Vijana wamesoma mpaka vyuo vikuu lakini ajira zao ni bodaboda na betting

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA taifa John Pambalu akiwa mkoani mwanza wakati wa kufanya kampeni kuwanadi wagombea wa chama chake kuelekea uchaguzi serikali za mitaa amesema vijana wamesoma mpaka vyuo vikuu lakini hawana ajira, ajira za zo ni mbili akiwataja bodaboda na wanaofanya michezo ya kubahatisha 'betting'

Soma pia: Vijana wahitimu wa Vyuo Vikuu wanataka nani awapambanie?
Your browser is not able to display this video.

Chanzo: Arusha zone news
 
Nadhani issue sio kutueleza Problem (we all know it) Issue ni kutoa Suluhisho (which is not rocket science) tena bila hizo bodaboda it could have been worse...

By the way kwa Sera za Chadema fully Private Ownership (katika karne hii ya teknolojia, capitalistic system ya trickle down haipo tena sababu nguvu kazi haiitajiwi tena)



It gonna get worse..., before if it might even get better (kwa njia tunayopitia sasa it won't) unless we change our strategies...

 
Yeye ana ajira gani ya maana zaidi ya utovu wa nidhamu alonao 🐒
 
Miaka 30 ijayo ndio itatuonesha madhara. Rasilimalu za uzalishaji bado zipo nyingi sana tatizo vijana tumebaki na ujinga wa kuajiriwa na uvivu wa kuizunguka hii nchi.

Wengi wa vijana wasomi wapo maeneo ya jiji na manispaa hawataki kabisa kufika vijijini na visingizio vyetu ni vyakijinga sana.

Ni kawaida kukuta kijana msomi ila hajawahi kuuzunguka ukanda wowote wa hii nchi kwenda kuangalia fursa na namna atavyoitumia elimu yake na bado tunataka kupambana soko la Afrika Mashariki na Kusini.

Vijana tuamke, tuzunguke hii nchi yetu. Haiwezekani vijana wageni kutoka hapo Kenya wakaijua Tanzania kuliko sisi vijana wenyeji.
 
Hao vijana wa kenya wanamitaji-hizo ziara za kutafuta fursa zinahitaji fedha

Na hao vijana wa kenya ni wachache wengi wao wanabangaiza hawana kazi ndo maana Rais wao anawatafutia kazi nje ya nchi kama qatar
 
Hao vijana wa kenya wanamitaji-hizo ziara za kutafuta fursa zinahitaji fedha

Na hao vijana wa kenya ni wachache wengi wao wanabangaiza hawana kazi ndo maana Rais wao anawatafutia kazi nje ya nchi kama qatar
Haihitaji fedha nyingi kama inavyoweza kudhaniwa. Nitakupa mfano, mimi niliizunguka kanda ya kaskazini pamoja na ukanda wa kati kwa fedha wastani wa Tshs. 400,000/-

Kama graduate atashindwa kukysanya fedha kwa mwaka akapata Tshs. 600,000/- anatakiwa ajitafakari sana, alienda shule kufanya nini.

Tuambiane ukweli, tuache kupeana visababu ili kujipooza. Graduate asiyeweza kukusanya Tsh. 600,000/- kwa mwaka huyo ni mzigo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
 
Watu hawawezi kuwa na mtazamo wa maisha kama wewe na maisha sio marahisi hivyo
Kuna-watu wengi wanaingiza zaidi ya laki 6 lakin hawawezi kusave sababu wanamajukumu mengi wengine wana wazazi wagonjwa wanatakiwa wawaangalie na mengineyo
 
Watu hawawezi kuwa na mtazamo wa maisha kama wewe na maisha sio marahisi hivyo
Kuna-watu wengi wanaingiza zaidi ya laki 6 lakin hawawezi kusave sababu wanamajukumu mengi wengine wana wazazi wagonjwa wanatakiwa wawaangalie na mengineyo
Mkuu tusijipooze kwa visingizio vya jumla. Ni graduate wangapi wana hayo majukumu mazito? Graduate walioanzisha familia baada ya chuo sidhani hata kama wanafika 10% na kama mtu alianza familia akiwa hana uhakika wa uchumi wake nao ni upumbavu mwingine (tusiuongelee)

Amini nakuambia graduate asiyeweza kutunza wastani wa Tsh. 1500/- kwa siku ni kaamua yeye mwenyewe na upumbavu wake. Tusikae kutetea ujinga lazima vijana tupeane hasira ya mafanikio.

Kuna jamaa hapa jukwaani wiki iliyopita aliweka uzi amefanya ziara kutoka kanda ya ziwa ameenda kuangalia fursa maeneo ya Morogoro alieleza mengi sana kwenye huo uzi na namna nmaeneo yalivyo na uwezo wa kuzalisha mali.

Na akaeleza anashangaa kuona vijana hawapo active hayo maeneo.

Graduate anatakiwa kupambana yeye binafsi sawa na walivyopambana mababu tukaupata uhuru 1961 wale wazee walikubali kupoteza sehemu ya maisha yao sababu yetu sisi na sisi leo tumekuwa wavivu na waoga wa kufanya mambo.

Hii ni aibu kubwa.
 
1
Serikali haitengenezi mazingira yeyote alafu unawalaumu graduate
Naweza sema wewe ndo mjinga na mpumbavu
Kwani yeye kawalaumu graduates? Msome tena. CCM ni washenzi, wao ndiyo wanaolaumiwa kwa kushindwa kuyatengengeneza mazingira ya ajira kwa wahitimu.
 
Serikali haitengenezi mazingira yeyote alafu unawalaumu graduate
Naweza sema wewe ndo mjinga na mpumbavu
Unataka mazingira gani zaidi ya hii amani iliyopo na huu uhuru wakuzurura sehemu yoyote ndani ya Taifa hili?. Yapo maeneo ardhi ekari 1 unauziwa na halmashauri ya kijiji kwa Tshs. 50,000/- hadi hata chini ya hapo na hayo maeneo yapo tu wazi mapori.

Vijana wakiambiwa wanaanza kuleta visingizio mara uchawi mara ni mbali na ujinga mwingi. Wanaenda kununua vigogo maelfu ya hekari huko na vijana wapo wapo tu.
 
Vijana wa kibongo wengi ambao wamehitimu vyuo vikuu ni sawa na standard 7 failures kwani wengi wao hawajitambui akili na usishangae kama hata wao wenyewe wasijuwe ni nini wanataka kufanya maishani mwao. Utawakuta wapo tu kwenye majumba ya betting nje wakiomba hela za kubet ama kuendesha bodaboda, seriously, mtu umeenda shule uendeshe bodaboda kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…