Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Mkurugenzi wa oganaizesheni na uchaguzi wa CHADEMA, John Pambalu anatuhumiwa kwa makosa ya ugaidi, taarifa zimeeleza.
Soma pia:
- Wakili Kisabo: Jeshi la Polisi litoe taarifa rasmi kuhusu alipo kada wa Chadema, John Pambalu
- CHADEMA: John Pambalu akamatwa na kupelekwa Central Police Arusha
Pambalu alikamatwa Oktoba 14, 2026 jijini Arusha na kusafirishwa kuja jijini Dar es Salaam, ambapo Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano, Breda Rupia aliandika katika ukurasa wake wa X kuwa ameshafikishwa kituo kikuu ha polisi cha Kanda ya Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo Oktoba 16, Wakili Hekima Mwasipu aliyekuwa kituoni hapo amesema, “anatuhumiwa kwa ugaidi,”
Hata hivyo, Mwasipu amesema bado anaendelea kuandika maelezo yake kituoni hapo.
Kuondoka kwa Pambalu
Licha ya kutokuwepo kwa taarifa rasmi ya Pambalu kuondoka nchini na kuelekea nchini Kenya, lakini taarifa zinabainisha kuwa aliondoka muda mfupi baada ya yeye na wenzake kukamatwa na polisi walipohudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 24, 2025.
Baada ya kukamatwa, Pambalu na makada wengine wanaodaiwa kufikia 21 walidai kushambuliwa vikali na kwenda kutupwa wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam alikana polisi kuwakamata Pambalu na wenzake.
Soma hapa: Muliro awakana Makada wa CHADEMA wanaodai kuteswa, kutupwa porini
Baada ya tukio hilo, Pambalu pamoja wenzake walionekana kwenye mitandao ya kijamii wakiwa nchini Kenya.
Mpaka sasa haijajulikana Pambalu alirudi lini nchini, lakini alionekana kwa mara ya kwanza mwaka huu Oktoba 14, 2026 akiwa katika uzinduzi wa ofisi ya Kanda ya Kaskazini jijini Arusha na baada ya uzinduzi huo alikamatwa na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.
