Uchaguzi 2020 Pambazuko la kipenga cha mwisho sehemu ya pili

Uchaguzi 2020 Pambazuko la kipenga cha mwisho sehemu ya pili

Mkuu mshanar au umechungulia ile kafara ya forojo ganze hawajaienzi???kwamba kafara itafanyika kuwa anguko la ccm kufidia uzembe huo????Hebu nipe picha nishuhudie maajabu haya nije niwasimulie wajukuu wangu nikizeeka!!!
Maagizo ilikuwa kila mwaka lifanyike ili akili za watu ziendelee kulala Kama kaburi
 
IN 2020 OCTOBER YOU WILL GET THE REASON TO CHOOSE 2022!You will understand as things unfold!
 
Unafikiri kizazi cha 1995 ndo kizazi cha 2020?? Unafikiri dunia ya 1995 ndo ya 2020??

Amini maneno yangu jaribu lolote dhidi ya Lissu litaongeza sympathy zaidi kwa Lissu na ndo itakuwa hatari kuu kwa usalama wa taifa letu na CCM kwa ujumla.

Jaribu la kumpiga risasi tu limempa umaarufu mkubwa na huruma kubwa kutoka kwa watu. Nakuhakikishia, Lissu akizuiwa kugombea Tanzania tujiandae kwa yale tuliyoyaona Ivory Coast na Sudan na sidhani Kama vyombo vya dola vikibanwa vitasimama upande wa CCM.
Pingamizi pingamizi ,ni wazi CCM watamwekea pingamizi.Kwanini huwezi kusoma mchezo mchafu?
 
Halafu cha ajabu wanaojitapa kupendwa na kukubalika nchi nzima ndio ambao hawalali.
 
Tuna chini ya siku 150 kuelekea uchaguzi mkuu.
Huu utakuwa uchaguzi mkuu tofauti kabisa na chaguzi nyingine zote zilizopita
Hakuna amsha amsha hakuna shamra shamra

Hakuna kimbiza kimbiza... Kumetulia sana na kwa sehemu kuna wasiwasi, woga na sononi kwa wananchi... Lakini pia wana tashwishwi ya kutaka kuona maajabu yakitendeka.

Muda uliobaki ni mchache sana lakini ni muhimu sana kwa kila dakika inayo tiktok.. Kuna mambo yanaendelea kimyakimya... Chinichini lakini kwa haraka na wepesi wa ajabu

The race against time...! Kama kutakuwa na huo uchaguzi (achana na neno HURU na HAKI) Tanganyika inaweza kuishangaza dunia.. Kila zama huwa na kurasa zake... Na unapofika wakati wa kufunua ukurasa husika huna budi.. huna jinsi.. Huna namna.. Huna hiari... Inabidi kuufunua...!!!

Kila jambo huwa na kikomo cha kuwa... Kikomo cha zama.. Kikomo cha nyakati... MWANADAMU ni mtumwa wa muda... Achana na maneno HURU na HAKI kuna watu walivikwa ukuu wakiwa hawapo... Kuna watu walikabidhiwa majukumu makubwa wakiwa mbali uhamishoni..

Kuna baadhi ya imani ukitaka kuoa mke si lazima uwepo eneo la tukio... Ndugu yako anaweza kukuolea kwa maneno halafu vitendo ukaja kufanya mwenyewe

Hili ni pambazuko la kipenga cha mwisho.. Kila alfajiri ipitayo haitarudi tena... Nje upepo unavuma lakini unavuma na mengi... Ni alfajiri nyingine tena...

Natambua wazi jana ulilala fofofo baada ya uchovu wa kazi na mihangaiko ya siku nzima... Juma zima... Lakini wapo ambao hawalali... Hawakulala na hawatalala mpaka kipenga cha mwisho kitakapodhihiri mwangwi wake na kupotelea kwenye kadamnasi ya hadhira yenye tashwishwi kubwa ya mabadiliko

Ni alfajiri nyingine tena.. Wanaume hawajalala ni mwendo wa kuandaa mazingira ili timu pinzani isiliguse dimba.. Kisha tutangaziane ushindi mnono wa kishindo!!

Kwenye kila andishi kuna TAMATI... Kama tamati ya andiko lako imetimia funika buku lako ulirudishe kabatini kwakuwa hakuna kurasa zaidi... Huhitaji kufanya marudio ya kurasa

Kuna kitabu kipya na wasomaji wapya.. Wape nafasi kwa upendo na bila ghiliba wasome kwa utulivu na amani kurasa zao... Nao kuna siku watafikia TAMATI... Usilazimishe makhaba kama hisia zumeshakufa

Kumbuka ni wafu pekee ndio wasiokula wala kunywa... Chumvi ikiisha ladha haifai tena kwakuwa hakuna cha kuipa ladha tena..
Ni alfajiri ya kipenga cha mwisho. Pambazuko lenye tumaini jipya. Achana na maneno HURU NA HAKI.. Uchaguzi utafanyika.. Maajabu yatatokea na dunia itashangaa

Jr[emoji769]
Itakuwa hivyo, Sasa kila sehemu hakuna aliye huru. Wote hofu tu.

Lissu rudi ili tukupigie kura
 
Mara nyingi tabiri zako umekuwa ukiangukia pua..!!
Tuone mara hii nafikiri utaanguka jicho kabisa..[emoji28]
Wenyewe wanakuambia chichiemu ni ileile ooh ni ileile..

Tusubiri tuone maajabu ya huyu mlozi
giphy.gif


Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom