Pamoja na kwamba zinaenda Spidi sana na Kuua mno, ila Wanaopenda Kufa bado hupenda Kuzigombania ili wawahi Kufika

Pamoja na kwamba zinaenda Spidi sana na Kuua mno, ila Wanaopenda Kufa bado hupenda Kuzigombania ili wawahi Kufika

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace ya kubeba magazeti iliyokuwa ikitoka jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Desemba 13, 2021 alfajiri katika kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa.
Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kugonga mti uliokuwa pembezoni mwa barabara na kupinduka na kusababisha vifo vya watu 9.

Chanzo: mwananchi_Official

Kuna moja KEROZENE nimepishana nayo Kibamba ikielekea Mkoani Arusha na Mmoja wa Abiria Mpenda Kufa aliyemo ndani kasema wanatarajia kufika Arusha baadae Saa 9 na Kesho Saa 4 za Asubuhi atakuwa anakunywa Chai Nyumbani Kwake Mkoani Dar es Salaam.
 
Kufa ni kufa tu mzee.... hata kw ajali bado kufa ni kulekule....
 
Back
Top Bottom