Bess
JF-Expert Member
- Oct 4, 2016
- 547
- 656
Idara hii iliweza kuthibitisha pasi na shaka kwamba Russia itaivamia Urusi, japo ikakosea ama haikuwa na uwezo kujua muda Mrussi atakaotumia kuiteka Kyiv.
TaarifA iliyokuwepo ni Russia kumaliza operesheni yake ndani ya siku kadhaa tu ama wiki huku wanasiasa wengine wakitia chumvi kwamba itachukua masaa tu.
Kama wangeitaarifu vema serikali yao, labda na tunaweza kukisia kwamba silaha zingetolewa mapema na bila shaka kuweza kubadili upepo wa vita tangu mwanzo.
Tusisahau pia pale Afghanstan serikali iliaminishwa kwamba kwa jinsi jeshi la nchi hiyo lilivyoundwa na kufundishwa kwa miaka zaid ya 20, Waasi watachukua mda ama kushindwa kabisa kuisumbua serikali. Tulishuhudia mara tu US force walipoondoka, Taleban waliangusha serikali kwa mda mchache tu.
Kosa hili pia lilifanywa vita ya Vietnam, kwa kuitaarifu vibaya serikali, iliaminika kwa asilimia zote ile vita USA watapata ushindi bila upinzani mkubwa. Hapa wafuatiliaji wa mambo wanajua pressure ya wananchi ililazimisha vita kuisha kabla ya kufikia lengo
Kosa lingine pia ni kuwa na taarifa ama za kubuni kwamba Saddam Hussein anamiliki silaha za maangamiz, hii ilikuja kuthibitishwa sio kweli na kuaibisha serikali yao mbele ya macho ya jamii ya kimataifa.
Wanajitetea vipi: wanasema kwamba moyo wa taaluma ya intelijesia ni kukusanya habari na kutumia habari ama taarifa ilizokusanya kufanya maamuzi,
wanaongeza kuwa daftari lao la notes halina maelezo ya kutosha kueleza 'ari ya kupigana'. Kwamba hawawez ku'predict baada ya vita kuanza, morali ya wapiganaji wa pande zote utakuwa vipi; na sio tu kwenye uwanja wa vita lakini pia mtaani matokeo ya vita yataitikiwa vipi kuongeza ama kupunguza morali ya vita.
Kiongoz wao mkubwa jeshini, U.S. Marine Corps, Gen. David Berger anasema japo program ya computer ingeweza kutabiri Russia itashinda baada ya siku ngapi, lakini ingeshindwa kung'amua ni kwa namna gani Ukraine inahimili na kubaki kwennye vita.
Hapa tunaweza kusema idara hii kwa nchi yoyote ni moyo wa maamuz ambayo serikali yoyote pale dunian lazima iwategemee. Sasa linapokuja suala la kukosea, inabidi wajitafakari kabla ya kuingiza serikali yao kwenye tiftif nyingine