Wengi wa wafanyabiashara wamegoma nchi nzima na moja ya ajenda yao ni ukaguzi wa risiti za EFD zisitishwe mara moja. Mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa na asilimia 95 ya wafanyabiashara wa nchi hii hawatoi risiti halali.
Pale unaponunua bidhaa ukiomba risiti toka kwa mfanyabiashara ni mgogoro na utaambiwa mashine ni mbovu ooh nikupe risiti iliyo na upungufu wa fedha uliyotoa n.k. Ukikomaa watakuona wewe siyo mtu wa kawaida. Kwa nini ninyi wafanyabiashara hamtaki kutoa risiti halali kwa bidhaa aliyonunua mteja?
Maduka machache yanayotoa risiti halali ni kama ALAF na maduka yanayosimamiwa na wazungu. Wahindi ndo wamekuwa wajanja kupitiliza na mara anakudanganya nikikuuzia bei hii sitakupa risiti kwa sababu tayari nimekupunguzia kumbe ni upuuzi mtupu.
Ndugu zangu nchi inajengwa na wananchi wenyewe, TOENI RISITI YA EFD na wananchi DAINI RISITI HALALI YA EFD.