Malenja jr
Member
- Jul 24, 2022
- 8
- 5
Na Malenja jr
Ninapotaka kufanya jambo kubwa kwa nchi huwa nawasikiliza wanaopinga uamzi wangu, najibizana nao kwa hoja, nikiona hoja zao zina nguvu kuliko zangu naacha niliyokuwa nayo natekeleza hayo matakwa yao lakini nionapo hoja zao ni dhaifu katika kunikosoa huwa naendelea na yale ninayoyapanga. Ndivyo navyofikia mafanikio haya si kwa akili zangu pekee Ni maneno aliyoyatoa Barack Obama, Rais wa zamani wa Marekani akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa Habari aliyehoji mbinu gani alikuwa akitumia kiongozi huyo kuwa kiongozi bora na mashuhuri kiasi hicho katika taifa kubwa Zaidi Ulimwenguni.
Japo wengi hawatambui, Maisha ya mwanadamu, maendeleo ya jamii na nchi yanahitaji vitu vitatu vya lazima yaani SIASA, UCHUMI,na UTAMADUNI.Mambo haya yote hupaswa kutazamwa na kubalansiwa vema na kupuuzwa kwa lolote kati ya haya hudhorotesha ustawi wa mtu, jamii na taifa.
SIASA; Huu ni mhimili nyeti sana katika jamii na taifa, ni siasa ndiyo hutupatia wanadiplomasia, ni siasa ndiyo hutuandalia viongozi na watu wenye maono na uzalendo wa kuisemea na kuipigania jamii nan chi yetu popote. Ni wanasiasa ndio hutoa ulinzi, sheria na sera za mwelekeo wa jamii, taifa na mifumo yote ya jinsi gani watu wetu waishi, watibiwe, wasome, waenende na bidhaa zetu ziweje na kipi kitumike wapi na kwa wakati gani, kupuuza siasa ni kuangamiza jamii, Taifa.
UCHUMI; Hili ni eneo ambalo linaamua kipato na uwezo wa nchi kujiendesha na kujitoa katika minyororo ya utegemezi. Uchumi ndiyo biashara, uchumi ni ujuzi wa watu, ubunifu wa watu, juhudi za watu kutafuta, uchumi hujengwa na maarifa, teknolojia na ufundi. Uchumi ni ajira na ajira ndilo hitaji namba moja la msaka kipato, kupuuza teknolojia, kudharau eneo la uchumi hufanya mtu, jamii au nchi kushindwa kujitegemea.
UTAMADUNI; Wasichojua wengi, Utamaduni ni kada nyeti na nguzo muhimu inayojenga mustakhabali na hadhi ya mtu, jamii au taifa na utambulisho wake. Utamaduni ni Imani yaani dini na fikra, utamaduni ni michezo yote tunayoiona, soka navyote, utamaduini ni Sanaa na wasanii wote tunaowaona. Utamaduni ni burudani na utamaduni ni maadili na tabia za mtu, jamii au taifa. Kupuuza eneo la utamaduni ni kuangamiza kizazi nja taifa kwa ujumla n ahata kupoteza vipaji vya watu vinavyiongiza faida kwao na taifa.
Katika kila moja ya kada hizo hapo juu iwe siasa, utamaduni ama eneo lile la uchumi na vipera vyake kama vilivyodadavuliwa huhitaji eneo maalumu la taaluma, masomo na msisitizo ili kufikia mafanikio Zaidi.
Viongozi wabovu, madikteta na wabinafsi hufinyanga finyanga mtaala wa elimu itolewayo ili iandae jamii ambayo haitakomboleka ili wao waendelee kubaki mamlakani, ukitaka kutawala jamii vuruga mfumo wa elimu isiwakomboe watu Ni maneno aliyowahi kuyasema PAUL FREIRE mmoja mmoja wa wanazuoni wachache waliojitoa kusema na jamii ili kuchochea fikra chanya popote pale kupitia kalam una vinywa vyao bila malipo.
Wakati tunahamasishana kusoma sayansi pekee tutambue tunaandaa sekta ya uchumi pekee, Sayansi ni elimu inayopatikana katika majaribio na utafiti wa kitaalamu hivyo lengo la sayansi ni kupata wataalam wa kubuni na kuendeleza teknolojia, uvumbuzi na uendeshaji mitambo na mashine za kisomi kama injinia, matabibu, warusha ndege, na wataalamu na watafiti wa miomea, mili ya Wanyama na binadamu na dunia na mambo yake. Masomo ya sayansi ya jiografia, fizikia, baiolojia na kemia yanatujenga katika eneo hili.
Wakati huo, jamii huhitaji wanadiplomasia, nchi inahitaji wasomi wanaoijua nchi na dunia katika Nyanja za Habari na jinsi mahusiano ya mtu na mtu, jamii na hata taifa na taifa yanavyoathiri uhuru na maendeleo ya jamii na nchi husika. Bila shaka masomo ya lugha, historia na uraia yanatujenga vema katika kuijua dunia na jamii zake popote, kujua jamii zetu na nchi na jinsi wazazi na babu zetu walivyopambana hadi hapa tulipo na hivyo kutupa njia ya kuanzia kufika mbele Zaidi.*
Rais wa awamu ya tano, tofauti na wanasiasa wengi alitazama mbali na kuona uzalendo, elimu ya utaifa na itakayojenga vijana na wasomi wetu kuelekea katika siasa safi, uzalendo na maarifa ya kidiplomasia yatakayojengwa na taarifa sahihi juu ya wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tuendako inajengwa na somo la Historia ambalo huwajuza watu wapi kipi kilifanyikaje na kikaleta mchango au madhara gani.
Alipokuwa akiwaapisha Mawaziri wapya jijini Dodoma, Rais wa awamu ya tano alitangaza somo la Historia kuwa somo la lazima katika ngazi zote za elimu nchini kama ambavyo watangulizi wake walilifanya somo la uraia kuwa la lazima shule ya msingi hadi chou kikuu.
Hili ni jambo kubwa japo media na wachambuzi wengi walikaa kimya wakigubikwa na mjadala wa teuzi na nafasi za uongozi pekee ambazo kwangu mimi si jambo lenye tija sana kwani wakati mwingine tujifunze kutazama yapi yamefanyikaje na yataleta athari gani Zaidi ya kuishia kutazama nani amekuwa nani na ataweza kipi.
Rais wa awamu ya tano amekuwa Rais wa kwanza kuonesha thamani ya elimu ya Sanaa ya jamii (historia) katka kuandaa jamii yenye uelekeo wa aina Fulani kama ambavyo Mwl. Nyerere alidhamiria kuijenga elimu katika misingi ya ujamaa na kujitegemea. Jambo hili linapaswa nkutazamwa na wadau wote kwa jicho pevu na masomo mengine yote yaboreshwe ili kuendana na mitaala.

Upvote
4