Pamoja na ufafanuzi wa Dkt. Mwigulu, bado kuna shida kwenye deni la Taifa



Usiwe unaropoka mambo usiyo na uhakika nayo.

Uliyoyaongea ni uwongo mkubwa.

Yachukue haya maelezo yangu hapa chini ili siku nyingine usiseme uwongo:

1. Deni la Tanzania lilipanda sana wakati wa utawala ws Rais Mwinyi, mpaka tukawa hatukopesheki, na misaada ya kibajeti ikasimamishwa.

2. Rais Mkapa, alipoingia alikuta hazina ina zero balance, huku nchi hairuhusiwi kukopa. Mkapa akatengeneza mifumo ya kudhibiti matumizi ya pesa, na akaanzisha VAT, akaweka mifumo ya kusimamia nidhamu ya matumizi ya Serikali, na nchi ikaanza kupunguza deni.

3. Nidhamu ya matumizi na ulipaji wa deni la Taifa, Tanzania kupitia mpango HIPC, mwaka 2000 iliweza kufutiwa deni lake la nje. Tukabakiwa na deni dogo sana la ndani na kutoka kwa taasisi chache za nje. Mkapa aliondoka madarakani, hazina aliyoikuta na zero balance, akaondoka akiiacha na balance ya dollar bilioni 5 na deni la Taifa likiwa dola bilion 7.7.

4. Kikwete alipoingia na kuikuta hazina ina pesa, akanza mara moja kutapanya pesa kwa kutoa mikopo hewa iliyoitwa 'mabilioni ya Kikwete'; kiasi kikubwa cha hiyo pesa haikurudishwa na hao waliochukua. Kikwete alianza kukopa na kuanza kulikuza deni tena kwa haraka.
 
Kama wewe ulivyoongea uongo hapa.

1.Nyerere alikimbia Uongozi baada ya Hali mbaya ya Uchumi wa Nchi na Nchi ikawa haikopesheki tena baada ya kuchukua mikopo Mingi kutoka Nchi kadhaa.

Baada ya kuelemewa na Uchumi kuharibika huku kisingizio kikiwa vita akaomba Mkopo Kwa Mabeberu na taasisi zake ndio hapo wakoha Hadi Mageuzi ya kiuchumi,kifedha na kisiasa yafanyike .

Akamuachia huo msala Mwinyi ndio hapo Nchi ikapata mikopo na ku survive.

Hiyo mikopo iliiva awamu ya Mkapa,akapewa masharti ya kubinafsisha (ambayo Leo mnaita kuuza Nchi) ndipo akasamehewa,anatakiwa aanzishe makusanyo ya Kodi Ili deni liwe linapikwa Kwa vigezo vya makusanyo ya Kodi nk nk.

Mwisho ni ujinga kusema unakusanya hela harafu hakuna unachofanya in terms of maendeleo.

Sikumbuki Mkapa alifanya kipi Cha zaidi kwenye maendeleo ya institution reforms na kuanzisha hizo taasisi.

2.Mara JK alitapanya sijui nini ni propaganda za kijinga wakati wote tunafahamu kwamba maendeleo ya ukweli Nchi hii yameanza kuknekana awamu ya Jakaya kuanzia shule,Umeme wa Rea,Vyuo Vikuu ,Barabara,Afya,Maji ,viwanja vya ndege nk nk.

3.Hata Sasa kinachoitwa deni kubwa mumepewa hoja na Mwigulu Je tuache kufanya maendeleo Kwa haraka Bali tusubirie kujikongoja Kwa kudunduliza makusanyo?

Tukienda hivyo hizo Sgr zenu white elephant zitaisha mwaka gani? Je population inayozidi Kukua itahudumiwa vipi?

Mwisho natoa wito Kwa Serikali ikope pesa za kutosha kufungua Uchumi wa Nchi hii hasa Barabara ,hii Nchi Hadi Leo hii Mikoa rundo haijaunganishwa na lami.
 
Hiyo 120 trillion itoke wapi ndani ya miaka mitano ijayo.? Kwa kupabdisha bei ya Energy drinks , smart gin na beer?
Lini makusanyo na kisemwacho kwenye bajeti vikashabiana.
Ujinga wako sawa na Hekaya za alfulela ulela kisa cha Ally Nacha.
 
Hiyo 120 trillion itoke wapi ndani ya miaka mitano ijayo.? Kwa kupabdisha bei ya Energy drinks , smart gin na beer?
Lini makusanyo na kisemwacho kwenye bajeti vikashabiana.
Ujinga wako sawa na Hekaya za alfulela ulela kisa cha Ally Nacha.
Hujui kitu Mzee , average growth ya mwaka 2023 ni 5.5%*80 bln dollar

2024= Dola 85bln

2025=Dola bln 90

Sasa unadhani miaka 5 ijayo tutakuwa wapi Kwa rate hii ya ukuaji? Maana tunaenda kuongeza zaidi ya Dola bln 30.
 
Hv wewe kwa Akili ya kawaida kabisa huyu Mwigulu anaweza kutuambia nn cha maana ss watanzania,Rais SAMIA aliyeruhusu rushwa anaweza kusimamia kitu kwa maendeleo mapana ya nchi hii,jibu ni hakuna,kila kitu ni hovyo hovyo tu.
 
In less than 4 years deni limeongezeka kutoka 60 trillion to 106 trillion 😂😩, si muda mrefu makusanyo yote ya TRA yatakuwa ni kulipia madeni tuu, tunaelekea kufilisika kama nchi
Debt financing is better than equit financing. Soma finance utaelewa hilo. Bahati mbaya mitanzania inabidha bila weledi wowote kama liwewe. Unaweza kuta ulisoma history au kaiswahili halafu unabisha
 
Debt financing is better than equit financing. Soma finance utaelewa hilo. Bahati mbaya mitanzania inabidha bila weledi wowote kama liwewe. Unaweza kuta ulisoma history au kaiswahili halafu unabisha
Dogo niko vizuri in finance😂,naweza kulipia school fees na kuwanunulia nyumba ukoo wako wote, acha ujinga
 
Mwingulu ni tatizo ambalo magufuli aliligundua akampiga chini cha kushangaza raisi aliekuj ndo kampa rungu huyu ndo mshauri wa masuala ya fedha kqa rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…