Pamoja na ukongwe wa CCM, Januari Makamba ametuonesha udhaifu wa mfumo wa utawala

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Ni udhaifu sana kiongozi kutumia madaraka ya kisheria kutimiza haja zake bila kujali hisia za wananchi. Mabadiliko ndani ya Tanesco yalikuwa muhimu lakini siyo kwa aina hii ya watu wapya ndani ya shirika. Waziri Januari ameleta tena watu wale wale ambao waliiliza nchi hii kwa wizi. Siyo kwamba hafahamu, ni kiburi kwamba watanifanya nini? Kwa maana nyingine tumerudi kwenye wizi wa wazi kwa imani kwamba ni zamu yao kuiba wengine pia itafika zamu yao, lakini ni baada ya miaka 7 ijayo.

Angalia watakaoiendesha Tanesco

Mafuru Tanesco- Mtu ambaye inasemekena alifanikisha GSM kusomba pesa za NBC kununulia magari ya mizigo bila kulipa deni.

Mchechu –Aliyejinufaisha badala ya kuinufaisha NHC.

Majaar –mdanganyifu wa kisheria, Tanesco ikaingia matatani hadi leo. Kubwa zaidi, imekuwaje wote hawa kukubali uteuzi huo wakati wakijua umma wa kitanzania hauna imani nao?

Hata kama walisingiziwa, je, hawana busara za kujiondoa?

Kama tumeamua kurudi ktk siasa dhaifu kiasi hiki, basi kumbe tuna wanasiasa ambao hawawezi kuwahudumia wa-TZ. Uchungu ni kuona kwamba huyu Januari ndo timu mpya aliyoiamini rais Samia.

Mageuzi aliyoyafanya kwa haraka kiasi hiki, ni ishara kwamba ndo lengo la yeye kuteuliwa tena kushika wadhifa huo.
 
Kamwe usiamini story za wanasiasa wa Tanzania kuwa fulani ni fisadi! Nyingi huwa ni stori za kutengeneza ili kuharibiana ulaji na kutengeneza kambi zao.

Mambo yote ya kweli huwa yanaishia Mahakamani na hukumu zinaonekaga Mf. Liyumba na Marehemu Basil Mramba.

Hizo stori za Rex Attorney, Mafuru na Mchechu ni stori za kutengenezwa tu ndo mana hukuwai ona watu wanefikishwa mahakamani

Ukitaka kuamini siasa za kibongo ni za kizandiki Waulize Mbowe , Lissu, Sendeka na Lema, Je Lowassa ni Fisadi au sio Fisadi?

Alafu fananisha majibu yao na ya kabla ya mwaka 2015 na baada ya mwaka 2015
 
NA BADO.

Team anaupiga mwingi bado wana usingizi wa pono, behold, the days come, saith ..., that I will send a famine in the land, not a famine of bread, nor a thirst for water, but of hearing the words of the KING, ahahaaaa.

Watu wakisema nchi inataka kiongozi mkakamavu as late Legendary John mnaleta dhihaka, acheni watu wapige pesa.

👉🏾Nyoosha mkono uchukue kile kilicho karibu nawe, otherwise tulia ngano na magugu zikue pamoja mpaka zitakapo gawanyika.
 
Kamwe usiamini story za wanasiasa wa Tanzania kuwa fulani ni fisadi! Nyingi huwa ni stori za kutengeneza ili kuharibiana ulaji na kutengeneza kambi zao.

Mambo yote ya kweli huwa yanaishia Mahakamani na hukumu zinaonekaga Mf. Liyumba na Marehemu Basil Mramba.

Hizo stori za Rex Attorney, Mafuru na Mchechu ni stori za kutengenezwa tu ndo mana hukuwai ona watu wanefikishwa mahakamani

Ukitaka kuamini siasa za kibongo ni za kizandiki Waulize Mbowe , Lissu, Sendeka na Lema, Je Lowassa ni Fisadi au sio Fisadi?

Alafu fananisha majibu yao na ya kabla ya mwaka 2015 na baada ya mwaka 2015
Hebu ngoja kwanza, una maana ile kesi ya dowans na Tanesco ilikuwa story tu? Wala hakukuwa na kesi?
 
Mkiambiwa Nchi inahitaji Katiba mpya, mnakataa! Ila Makamba akiwateua watu anao wahitaji yeye, kwa vigezo vyake na kwa mujibu wa Katiba iliyopo, mnashupaza shingo kupinga tena huo uteuzi!
Mbona hii iliyopo inavunjwa na hakuna hatua zinachukuliwa.

Sio kwamba napinga katiba mpya. Ila nachojiuliza Katiba mpya hata ikija na ikawa nzuri italeta mabadiliko gani?

Maana wanaweza wakaivunja tu kama wanavyofanya kwa iliyopo, na wasifanywe chochote. Tatizo lililopo nadhani wananchi tumeshindwa kuilinda katiba.
 
Katiba mpya itaweka miiko kwa watawala kuwa juu ya sheria kama ilivyo sasa. Hii katiba ya sasa ilitengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuifanya ccm kuwa chama dola, na makada wake kuwa juu ya kila kitu.
 
Ni udhaifu sana kiongozi kutumia madaraka ya kisheria kutimiza haja zake bila kujali hisia za wananchi. Mabadiliko ndani ya Tanesco yalikuwa muhimu lakini siyo kwa aina hii ya watu wapya ndani ya shirika. Waziri Januari ameleta tena watu wale wale ambao waliiliza nchi hii kwa wizi. Siyo kwamba hafahamu, ni kiburi kwamba watanifanya nini? Kwa maana nyingine tumerudi kwenye wizi wa wazi kwa imani kwamba ni zamu yao kuiba wengine pia itafika zamu yao, lakini ni baada ya miaka 7 ijayo.

Angalia watakaoiendesha Tanesco Mafuru Tanesco- Mtu ambaye inasemekena alifanikisha GSM kusomba pesa za NBC kununulia magari ya mizigo bila kulipa deni. Mchechu –Aliyejinufaisha badala ya kuinufaisha NHC. Majaar –mdanganyifu wa kisheria, Tanesco ikaingia matatani hadi leo. Kubwa zaidi, imekuwaje wote hawa kukubali uteuzi huo wakati wakijua umma wa kitanzania hauna imani nao? Hata kama walisingiziwa, je, hawana busara za kujiondoa?

Kama tumeamua kurudi ktk siasa dhaifu kiasi hiki, basi kumbe tuna wanasiasa ambao hawawezi kuwahudumia wa-TZ. Uchungu ni kuona kwamba huyu Januari ndo timu mpya aliyoiamini rais Samia. Mageuzi aliyoyafanya kwa haraka kiasi hiki, ni ishara kwamba ndo lengo la yeye kuteuliwa tena kushika wadhifa huo.
Kuamini zile kauli za Jiwe ilibidi uwe na uwezo kama wake au chini yake kama wewe.
 
hivi bado kuna watu bado mnaamini kuwa wanasiasa wako kwe nafasi zilizopo kwajili ya kuwatumikia wananchi? wenzetu wa dunia ya kwanza walilitambua hili wakawekeza kwenye taasisi imara, yaani mtu avhuje jasho toka chini huko aende kwa waganga atoea makafara agombane na watu wengine ht kuua watu eti ili aje kuwatumikia wananchi loh!!
 
Mkiambiwa Nchi inahitaji Katiba mpya, mnakataa! Ila Makamba akiwateua watu anao wahitaji yeye, kwa vigezo vyake na kwa mujibu wa Katiba iliyopo, mnashupaza shingo kupinga tena huo uteuzi!

Nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Tate Mkuu
 
NA BADO.

Team anaupiga mwingi bado wana usingizi wa pono, behold, the days come, saith ..., that I will send a famine in the land, not a famine of bread, nor a thirst for water, but of hearing the words of the KING, ahahaaaa.

Watu wakisema nchi inataka kiongozi mkakamavu as late Legendary John mnaleta dhihaka, acheni watu wapige pesa.

[emoji1485]Nyoosha mkono uchukue kile kilicho karibu nawe, otherwise tulia ngano na magugu zikue pamoja mpaka zitakapo gawanyika.
Mkuu wew ulipata kujua ile 1.5tr ilienda wapi? Au huna habari nayo
 
Ni udhaifu sana kiongozi kutumia madaraka ya kisheria kutimiza haja zake bila kujali hisia za wananchi. Mabadiliko ndani ya Tanesco yalikuwa muhimu lakini siyo kwa aina hii ya watu wapya ndani ya shirika. Waziri Januari ameleta tena watu wale wale ambao waliiliza nchi hii kwa wizi. Siyo kwamba hafahamu, ni kiburi kwamba watanifanya nini? Kwa maana nyingine tumerudi kwenye wizi wa wazi kwa imani kwamba ni zamu yao kuiba wengine pia itafika zamu yao, lakini ni baada ya miaka 7 ijayo.

Angalia watakaoiendesha Tanesco Mafuru Tanesco- Mtu ambaye inasemekena alifanikisha GSM kusomba pesa za NBC kununulia magari ya mizigo bila kulipa deni. Mchechu –Aliyejinufaisha badala ya kuinufaisha NHC. Majaar –mdanganyifu wa kisheria, Tanesco ikaingia matatani hadi leo. Kubwa zaidi, imekuwaje wote hawa kukubali uteuzi huo wakati wakijua umma wa kitanzania hauna imani nao? Hata kama walisingiziwa, je, hawana busara za kujiondoa?

Kama tumeamua kurudi ktk siasa dhaifu kiasi hiki, basi kumbe tuna wanasiasa ambao hawawezi kuwahudumia wa-TZ. Uchungu ni kuona kwamba huyu Januari ndo timu mpya aliyoiamini rais Samia. Mageuzi aliyoyafanya kwa haraka kiasi hiki, ni ishara kwamba ndo lengo la yeye kuteuliwa tena kushika wadhifa huo.
Kama hauna meno ya kula keki ya taifa basi tulia pembeni ya uwanja ushangilie eidha kwa kupiga kelele za hasira au za furaha kwa waliopo ulingoni...
 
Kwani
Kamwe usiamini story za wanasiasa wa Tanzania kuwa fulani ni fisadi! Nyingi huwa ni stori za kutengeneza ili kuharibiana ulaji na kutengeneza kambi zao.

Mambo yote ya kweli huwa yanaishia Mahakamani na hukumu zinaonekaga Mf. Liyumba na Marehemu Basil Mramba.

Hizo stori za Rex Attorney, Mafuru na Mchechu ni stori za kutengenezwa tu ndo mana hukuwai ona watu wanefikishwa mahakamani

Ukitaka kuamini siasa za kibongo ni za kizandiki Waulize Mbowe , Lissu, Sendeka na Lema, Je Lowassa ni Fisadi au sio Fisadi?

Alafu fananisha majibu yao na ya kabla ya mwaka 2015 na baada ya mwaka 2015
Kwani hao waliotajwa na mleta uzi walikuwa wanasiasa?
 
This is Simba bwana,ndo Tanzania hiyo watanzania sisi kazi yetu Ni kulalamika tu.hatuchukui hatua
 
Ni zamu yao kulamba mzinga aliouacha babu!!kale kazee kajambazi Sana ,ndio maana hata Toto lake ni jambaz pia .hili taifa shida ni kwamba wazalendo wanazidiwa akili na majambazi,majambazi ni majasiri Sana hufanya Mambo waziwazi hata Kama yanaonekana kirahisi, wazalendo wa taifa hili wengi wao ni waoga na wepesi wa kukata tamaa(excepted mwal.jk,j pombe,)
 
Back
Top Bottom