Pamoja na ukongwe wa CCM, Januari Makamba ametuonesha udhaifu wa mfumo wa utawala

Pamoja na ukongwe wa CCM, Januari Makamba ametuonesha udhaifu wa mfumo wa utawala

Jamani tuache uongo,mwenye ushahudi auweke sio tuhuma za kupuuzi kama hizi

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Tuseme hakuna ushahidi. Je, kuna sababu ya kurudisha watu kwenye nafasi ya shirika watu wale wale? Mafuru alikuwa kwenye BRN, nini cha maana alichofanya? Most of these are as useless as Kapo. Kwani hakuna wa-TZ wa maana nchi hii. Unaamini hata wewe huna matumizi kuliko hao watu wa Januari?
 
Kamwe usiamini story za wanasiasa wa Tanzania kuwa fulani ni fisadi! Nyingi huwa ni stori za kutengeneza ili kuharibiana ulaji na kutengeneza kambi zao.

Mambo yote ya kweli huwa yanaishia Mahakamani na hukumu zinaonekaga Mf. Liyumba na Marehemu Basil Mramba.

Hizo stori za Rex Attorney, Mafuru na Mchechu ni stori za kutengenezwa tu ndo mana hukuwai ona watu wanefikishwa mahakamani

Ukitaka kuamini siasa za kibongo ni za kizandiki Waulize Mbowe , Lissu, Sendeka na Lema, Je Lowassa ni Fisadi au sio Fisadi?

Alafu fananisha majibu yao na ya kabla ya mwaka 2015 na baada ya mwaka 2015
Sawa wateteteeni tu, baada ya miaka 2 mtalamba matapishi yenu.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Mbona hii iliyopo inavunjwa na hakuna hatua zinachukuliwa.

Sio kwamba napinga katiba mpya. Ila nachojiuliza Katiba mpya hata ikija na ikawa nzuri italeta mabadiliko gani?

Maana wanaweza wakaivunja tu kama wanavyofanya kwa iliyopo, na wasifanywe chochote. Tatizo lililopo nadhani wananchi tumeshindwa kuilinda katiba.
Hii ya sasa ina matobo (loop holes) nyingi, ndiyo maana hata anayeivunja katiba hiyo hiyo inamlinda... Hivi mfano una katiba ambapo majaji hawateuliwi na mkuu wa muhimili mwingine, kama tulivyoona Kenya ambapo majaji wameitupilia mbali BBI ya Kenyata, unadhani haya mambo yataendelea?
 
Statement ya kusema Tanesco ianze kujiendesha kibiashara Ni neno Pana Sana ndani yake Kuna mikataba ya kibiashara mipya itaingia ambayo itazalisha kesi za kulipa mabilioni, matatizo ya kutengeneza tatizo ili solution ipatikane kwa wizi wa fedha is back. ..pia hao watu ni technically ya mtu kujinuafaishia na kujenga mtandao na Mambo ya future presidency

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
hivi bado kuna watu bado mnaamini kuwa wanasiasa wako kwe nafasi zilizopo kwajili ya kuwatumikia wananchi? wenzetu wa dunia ya kwanza walilitambua hili wakawekeza kwenye taasisi imara, yaani mtu avhuje jasho toka chini huko aende kwa waganga atoea makafara agombane na watu wengine ht kuua watu eti ili aje kuwatumikia wananchi loh!!
Asantè!
 
Kumuweka tu Maajar ambae aliisaidia Dowans kuwaliza Tanesco ni Jambo la ajabu sana.
Bado najiuliza ina maana viongozi wetu hawana kumbukumbu?
Hao viongozi ndio walikuwa nyuma yake sasa kama ulikuwa hujui
 
Halafu kuna mtu anathubutu kukwambia katiba mpya itatusaidia nini.. Yaani iwepo katiba mpya inayoruhusu kiongozi kushtakiwa akiwa madarakani au baada ya madaraka halafu wizi wa kiwango cha kutisha hivi uendelee
kuwepo!!!?

Katiba mpya ya wananchi iruhusu watu kujiorganise na kumfungulia kiongozi mashtaka, akishinda kwa kuhonga zinafuata rufaa, hata hao majaji itafika muda watajisikia aibu.

Sasa hivi viongozi wana viburi sababu wanajua hamna cha kuwafanya ndio maana mtu anaamka anawaambia mkitaka mhamie burundi, tuhamie burundi hii nchi ni ya babu yake?
 
Hii ya sasa ina matobo (loop holes) nyingi, ndiyo maana hata anayeivunja katiba hiyo hiyo inamlinda... Hivi mfano una katiba ambapo majaji hawateuliwi na mkuu wa muhimili mwingine, kama tulivyoona Kenya ambapo majaji wameitupilia mbali BBI ya Kenyata, unadhani haya mambo yataendelea?
Mmmh! Kwa upande wa Kenya Majaji wanapatikanaje mkuu?
 
Katiba mpya itaweka miiko kwa watawala kuwa juu ya sheria kama ilivyo sasa. Hii katiba ya sasa ilitengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuifanya ccm kuwa chama dola, na makada wake kuwa juu ya kila kitu.
Kwani hii iliyopo haina miiko? Tatizo sio Katiba per se bali kasumba ya muda mrefu miongoni mwa Watanzania kutoheshimu sheria. Mtu asiyeheshimu ndoa yake hawezi kuheshimu sheria za nchi. It is that simple!
 
Ni udhaifu sana kiongozi kutumia madaraka ya kisheria kutimiza haja zake bila kujali hisia za wananchi. Mabadiliko ndani ya Tanesco yalikuwa muhimu lakini siyo kwa aina hii ya watu wapya ndani ya shirika. Waziri Januari ameleta tena watu wale wale ambao waliiliza nchi hii kwa wizi. Siyo kwamba hafahamu, ni kiburi kwamba watanifanya nini? Kwa maana nyingine tumerudi kwenye wizi wa wazi kwa imani kwamba ni zamu yao kuiba wengine pia itafika zamu yao, lakini ni baada ya miaka 7 ijayo.

Angalia watakaoiendesha Tanesco

Mafuru Tanesco- Mtu ambaye inasemekena alifanikisha GSM kusomba pesa za NBC kununulia magari ya mizigo bila kulipa deni.

Mchechu –Aliyejinufaisha badala ya kuinufaisha NHC.

Majaar –mdanganyifu wa kisheria, Tanesco ikaingia matatani hadi leo. Kubwa zaidi, imekuwaje wote hawa kukubali uteuzi huo wakati wakijua umma wa kitanzania hauna imani nao?

Hata kama walisingiziwa, je, hawana busara za kujiondoa?

Kama tumeamua kurudi ktk siasa dhaifu kiasi hiki, basi kumbe tuna wanasiasa ambao hawawezi kuwahudumia wa-TZ. Uchungu ni kuona kwamba huyu Januari ndo timu mpya aliyoiamini rais Samia.

Mageuzi aliyoyafanya kwa haraka kiasi hiki, ni ishara kwamba ndo lengo la yeye kuteuliwa tena kushika wadhifa huo.
mlishindwa kumwambia baba yenu mzalendo alete katiba mpya Sasa mnahaha tu , sukuma gang, mlijua tunaishi milele . Katiba mpya ni muhimu iwe kwa chama tawala , upinzani na wananchi
 
Kama tanesco walikua na wansheria dhaifu angefanyeje
Umekuja kutetea kuwa Tanesco walikuwa na wanasheria dhaifu, hujui kuwa Maajar nae pia alikuwa mwanasheria wa Tanesco? Alikuwa anakula pande zote mbili
 
Umekuja kutetea kuwa Tanesco walikuwa na wanasheria dhaifu, hujui kuwa Maajar nae pia alikuwa mwanasheria wa Tanesco? Alikuwa anakula pande zote mbili
Huyu mama alikuwa hadi balazo marekani , mara mwenyekiti wa vodacom huko hakutosheka tu mpaka leo anataka madaraka
 
Statement ya kusema Tanesco ianze kujiendesha kibiashara Ni neno Pana Sana ndani yake Kuna mikataba ya kibiashara mipya itaingia ambayo itazalisha kesi za kulipa mabilioni, matatizo ya kutengeneza tatizo ili solution ipatikane kwa wizi wa fedha is back. ..pia hao watu ni technically ya mtu kujinuafaishia na kujenga mtandao na Mambo ya future presidency

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Akina Chenge waliiba nchi hii kwa kisingizio cha ignorance ya kuandika mikataba. Sasa ameingia waziri ambaye anaamini ana akili wakati akijua kuna watu wanamzidi uwezo mbali sana. He is not even at a half knowledge!
Ni miaka michache ijayo mtu kama Januari atakuwa kwenye kitabu cha cost of acting stupid.

Anajifanya mtu wa twitter, lakini he is believing in his hopelessness!
 
Back
Top Bottom